Lugha ya Kiswahili ni fursa

Nasryhamdan

New Member
Dec 19, 2022
3
1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amezitaka wizara na taasisi za serikali kuendelea kutekeleza maagizo ya serikali ikiwemo kutumia lugha ya kiswahili katika mikutano na semina.

Ameyasema hayo Leo wakati wa ufunguzi wa kongamano la sita la la kiswahili la Kimataifa ambalo limefanyika Pemba.

Rais Dk.Mwinyi amesema lugha ya kiswahili inatakiwa kutumika kuandaa Sheria,sera,kanuni,mikataba,uandishi wa majina ya mitaa, majina ya Barabara,mabango,nembo na vifungashio vya bidhaa.

Amesema lazima lugha ya kiswahili ipewe nafasi ambayo itatumika na watu wengi.

Katika maelezo yake Rais Dk Mwinyi amesema anawasisitiza waandishi na wahariri wazingatie matumizi fasaha na sanifu ya kiswahili na kuacha kuchanganya na kingereza kutokana na kuwa inadhoofisha maendeleo ya kiswahili.

Amesema lugha ya kiswahili ni hazina muhimu inayoweza kutumika katika kukuza uchumi wa nchi na mtu mmoja hususani kwa nchi za Afrika ya Kusini na nchi za Afrika ya Mashariki.

Pia,amesema Kwa wazanzibari hawapaswi kudharau na kufumbia macho fursa muhimu iliyopo ya lugha ya kiswahili.

Rais Dk.Mwinyi ameyataja maeneo mbalimbali ambayo lugha ya kiswahili inaweza kutumika kwa soko la fursa za ajira ikiwemo ufundishaji wa kiswahili Kwa wageni.

Ameyataja maeneo mengine ni tafsiri na ukalimani,uhariri na uchapishaji vyombo vya habari na kazi nyingine za ubunifu.
 
Back
Top Bottom