Lugha hiyo inaunganisha lugha ya asili za asili za Afrika kusini hasa ya kabila la kina bushmen na lugha ya kiholanzi. Makaburu walifanya vile ili iwe rahisi kuwasiliana na watu weusi na kuwatawala kwa urahisi zaidi. Kimsingi hii lugha ya kiafrikana haipo Uholanzi na inasemekana kuwa ukiongea kiafrikana ukiwa Uholanzi hakuna mholanzi atakayekuelewa kabisa kwa sababu lugha ya kiholanzi yenyewe ilishatoholewa sana hadi lugha mpya ya kiafrikana ikazaliwa na mholanzi mwenyewe wa Afrika kusini akiamua kuongea lugha yake tupu bila kuongea kiafrikana,anayejua kiafrikana hawezi kung'amua chochote kile kilichoongelewa. Hivyo makaburu walipokuwa wanataka kuwateta watu weusi walikuwa wanaongea kiholanzi origino na wanafanya mambo yao. Lugha ya kiafrikana inasemekana ni ngumu sana kujifunza tofauti na lugha zingine za Afrika ya kusini.
Source: Kwa msaada wa vijana wa kitanzania wanaokimbilia Afrika kusini kutafuta maisha