ibnuislam79
New Member
- Apr 2, 2014
- 2
- 2
LUGHA YA ISHARA (BODY LANGUAE)- 1
UTANGULIZI:
Na Mummed Ibnul Islam
Kwa kadri tulivyokua tunakaribia karne ya 20, tulishuhudia uibukaji wa aina mpya wa wanasayansi jamii wajulikanao kama wanasayansi wa lugha ya ishara (non-verbalists.
Kama vile mlinzi wa ndege anapofurahi kuangalia ndege na tabia zao, basi hivyo hivyo mwanasayansi wa lugha ya ishara hurahi kuwangalia wanaadamu na tabia zao. Huwatazama sehemu za kazi, kwenye fukwe, kwenye T.V, ofisini au sehemu nyengine yoyote ile ambayo kuna wanaamiliana. Anakua mwanafunzi anayetaka kujua matendo ya binadamu wenzie. Ili mwishoe ajijue yeye mwenyewe na ajue namna ya kuimarisha mahusiano yake na wenzie.
Inaonekana ni ajabu kua katika kipindi miaka milioni moja au zaid kipengele cha mawasiliano ya lugha ya ishara kilikua kinasomwa lakini ni katika miaka ya 1960 tu ndio watu waliapoanza kujua uwepo wake, pale Julius Fast alipochapisha kitabu kinachohusu lugha ya ishara mwaka 1970. Huu ulikua ni mukhtasari wa kazi zilizofanywa na wanasayansi wa tabia za viumbe (behavioural scientists) kuhusu mawasiliano ya ishara (non-verbal communications).
Pamoja na hayo lakini mpaka leo watu hawana habari na uwepo wa lugha ya ishara (body language) ukiacha umuhimu wake kwenye maisha yao.
Charlie Chaplin na waigizaji wengine wa filamu zisizo na maongezi ya sauti ni miongoni mwa viongozi wa mawasiliano ya ishara. Wao ndio waliokua njia ya mawasiliano kwenye T.V. kila muigizaji aliwekwa kundi la waigizaji wazuri ua katika kundi la waigizaji wabaya kwa kutumia kigezo cha uwezo wake wa kutumia ishara (gestures) na ishara nyengine za mwili (body signals) katika kufanya mawasiliano kwa ufanisi zaidi. Hivyo tunapozungumzia filamu zilikua maarufu na zilizokosa umaarufu uzito mkubwa uliwekwa kwe kipengele cha kuigiza kwa kutumia mawasiliano ya ishara, hivyo waigizaji wengi wa filamu za mawasiliano ya ishara walififia kidogo kidogo na mwishowe kupotea na kutojulikana. Na wale mahiri katika mawasiliano ya mdomo walishinda.
Kitabu ambacho kilikua na ushawishi mkubwa kuhusu lugha ya mawasiliano kabala ya karne ya 20 ni cha Charles Darwin “The Expression of Emotions in Mans and Animals” kilichochapishwa mwaka 1872. Kitabu hichi kimetoa tafiti za kisasa zinazohusu maelezo ya uson (facial expressions) na lugha ya ishara, mawazo na chunguzi nyingi za Darwin zimethibitishwa na watafiti wa zama hizi duniani kote. Tangu kipindi hicho watafiti wengi wamegundua na kuhifadhi takribani na ishara za mwili milioni moja. Albert Mehrabian amebaini kua maneno huleta athari katika ujumbe kwa 7 %, na mijadala (tone of voive, inflection and other sounds) inaathiri ujumbe kwa 38 % na ishara huathiri ujumbe kwa 55 %.
Professor Birdwhistell alifanya makisio sawa na Albert Mehrabian kuhusu kiwango cha mawasiliano ya ishara yanayofanyika miongoni mwa watu. Alikisia wastani wa mtu kuwasiliana kwa maneno ni dakika 10 au 11 kwa siku na kila sentensi inachukua sekunde 2.5. kama ilivyokua kwa Mehrabian Professor Birdwhistell aligundua kua katika maongezi ya uso kwa uso mawasilano yam domo (verbal) yanatokea chini ya 35 %, na zaidi 65 ya maongezi yanafanyika kwa ishara ( nonverbal).
Watafiti wengi wa zama hizi wamekuli kua kimsingi maelezo ya mdomo hutumika kwenye kuwasilisha ujumbe wa maelezo tu na ishara hutumika kujadili mitazamo ya mtu mwenyewe, na wakati mwenigine hutumika kama mbadala wa maelezo ya mdomo. Kwa mfano mwanamke anaweza kumuangalia mwaname kwa mtazamo ujulikanao kwa lugha ya kiingereza “look to kill” na kufikisha ujumbe wa wazi kabisa bila ya kufungua mdomo.
Birdwhistell anasema bila ya kuzingatia utumaduni, mtu aliyefundishwa vizuri anaweza kuelezea nyenendo za mtu kwa kusikiliza sauti yake. Vile vile Birdwhistell alijua namna ya kuwelezea lugha inayozungumzwa na mtu kwa kuangalia ishara (gesture) tu.
Jambo la kuvutia mwanadamu hua hana habari na mikao (postures), nyenendo, ishara (gestures) ambayo inaleza mengine wakati sauti yake inasema mengine.
INAENDELEA……..
LUGHA YA ISHARA -2
Na Muhammed Ibnul Islam
Tunandele tulipoishia jana kuhusu lugha ya ishara.
Leo tutangalia vipengele viwili, navyo ni uelewa wa lugha ya ishara na ishara za kuzaliwa nazo, ishara za urithi na ishara za kitamaduni.
Lakini mzungumzaji asiyemuelewa atapuuzia na hatojali.
Katika hili la uelewa wa lugha ya mwili wanawake wanaufahamu nalo kuliko wanaume.
Wanawake wana uwezo wa asili wa kupokea na kufumbua ishara za mwili na maana waume wachache wanaweza kudanya wake zao na kusalimika. Lakini waume wengi hukamatwa pale wake zao wanapowaangalia waume zao machoni tu bila ya wao wenyewe kujua kua washagundulika kama wanadanganya.
Ufahamu huu wa lugha ishara kwa wanawake ni ushahidi kwa wale wanawake waliolea watoto wadogo. Kwa miaka michache ya mwanzo mara nyingi mama hua anategemea lugha ya ishara kuwasiliana mwanawe, na inaamika kua hii ndio sababu wanawake wanakua wanajadili kwa uelewa hali ya juu kuliko wanaume.
Majibu ya tafiti hizi zinaonesha kua baadhi ya ishara zinaingia katika kila kundi. Kwa mfano watoto wachanga wote wanapozaliwa tu wanakua na uwezo kunyonya maziwa kutoka kwa mama zao, hii inaashiria kua uwezo huu ni wa kuzaliwa nao au unatokana na urithi. Mwanasayansi wa kijerumani Eibl-Eibesfeldt aligundua kua tabia ya kutabasamu kwa watoto walizaliwa na ulemavu wa masikio na macho hakutemei kusoma au kukopi popote, hii nayo inamaanisha kua hili ishara ya kuzakiwa nayo. Ekman Friesen and Sorenson wamekubaliana baadh ya imaan za Darwin kuhusu ishara za kuzaliwa (inborn gestures) walipofanya utafiti utafiti kuhusu (facial expression) za tamaduni tano mbalimbali. Baada ya utafiti wao waligundua kua taaduni zote hizo zinatumia ishara zinazofanana kuonesha hisia (emotion). Matokeo haya yaliwapelekea kuhitimisha hizi ni ishara za kuzaliwa nazo.
Kwa mfano unapofunga mikono yako kifua je! Wakulia unakua jua kushoto au kinyume chake? Watu wengi hawawezi kulielezea hili kwa kujiamini mpaka wafanye kwa vitendo. Katika namna mbili hizo za kufunga mikono kifuani, moja inamaanisha kua mtu yupo vizuri na nyengine inamaanisha kua mtu amekosewa. Ushahidi unaashiria kua hali hii mbili ni za urithi (genetic) na haziwezi kubalishwa.
Mjadala bado upon a unaendelea kuhusu je! Baadhi ya ishara ni zinatokana utamaduni au ni za urithi? Kwamfano wanaume wengi wanapovaa koti huanza na mkono wa kulia wakati wanawake wengi huanza na mkono wa kushoto. Vile vile mwanamme anapopita alipo mwanamke humuelekezea mwili wake wakati mwanamke anapopita alipo mwanaume hukwepesha mwili wake dhidi ya mwanaume. Suali la kujiuliza hapaa je! Hii ni silika ya mwanamke kufanya ili kuficha kifua chake? Je! Reaction hii mwanawake amezaliwa nayo au hua amejifunza kutoka kwa wanawake wenzake?
Tabia zetu za ishara nyingi zao tumejifunza na maana ya nyenendo na ishara nyingi zinatokana na tamaduni zetu.
ITAENDELEA…..

- UFAHAMU NA UELEWA WA LUGHA YA ISHARA

- ISHARA ZA KUZALIWA, ZA URITHI, ZA KUJIFUNZA NA ZA KITAMADUNI