LUGHA YA ISHARA

LUGHA YA ISHARA

ibnuislam79

New Member
Joined
Apr 2, 2014
Posts
2
Reaction score
2
LUGHA YA ISHARA (BODY LANGUAE)- 1
UTANGULIZI:
Na Mummed Ibnul Islam

Kwa kadri tulivyokua tunakaribia karne ya 20, tulishuhudia uibukaji wa aina mpya wa wanasayansi jamii wajulikanao kama wanasayansi wa lugha ya ishara (non-verbalists.
Kama vile mlinzi wa ndege anapofurahi kuangalia ndege na tabia zao, basi hivyo hivyo mwanasayansi wa lugha ya ishara hurahi kuwangalia wanaadamu na tabia zao. Huwatazama sehemu za kazi, kwenye fukwe, kwenye T.V, ofisini au sehemu nyengine yoyote ile ambayo kuna wanaamiliana. Anakua mwanafunzi anayetaka kujua matendo ya binadamu wenzie. Ili mwishoe ajijue yeye mwenyewe na ajue namna ya kuimarisha mahusiano yake na wenzie.
Inaonekana ni ajabu kua katika kipindi miaka milioni moja au zaid kipengele cha mawasiliano ya lugha ya ishara kilikua kinasomwa lakini ni katika miaka ya 1960 tu ndio watu waliapoanza kujua uwepo wake, pale Julius Fast alipochapisha kitabu kinachohusu lugha ya ishara mwaka 1970. Huu ulikua ni mukhtasari wa kazi zilizofanywa na wanasayansi wa tabia za viumbe (behavioural scientists) kuhusu mawasiliano ya ishara (non-verbal communications).
Pamoja na hayo lakini mpaka leo watu hawana habari na uwepo wa lugha ya ishara (body language) ukiacha umuhimu wake kwenye maisha yao.
Charlie Chaplin na waigizaji wengine wa filamu zisizo na maongezi ya sauti ni miongoni mwa viongozi wa mawasiliano ya ishara. Wao ndio waliokua njia ya mawasiliano kwenye T.V. kila muigizaji aliwekwa kundi la waigizaji wazuri ua katika kundi la waigizaji wabaya kwa kutumia kigezo cha uwezo wake wa kutumia ishara (gestures) na ishara nyengine za mwili (body signals) katika kufanya mawasiliano kwa ufanisi zaidi. Hivyo tunapozungumzia filamu zilikua maarufu na zilizokosa umaarufu uzito mkubwa uliwekwa kwe kipengele cha kuigiza kwa kutumia mawasiliano ya ishara, hivyo waigizaji wengi wa filamu za mawasiliano ya ishara walififia kidogo kidogo na mwishowe kupotea na kutojulikana. Na wale mahiri katika mawasiliano ya mdomo walishinda.
Kitabu ambacho kilikua na ushawishi mkubwa kuhusu lugha ya mawasiliano kabala ya karne ya 20 ni cha Charles Darwin “The Expression of Emotions in Mans and Animals” kilichochapishwa mwaka 1872. Kitabu hichi kimetoa tafiti za kisasa zinazohusu maelezo ya uson (facial expressions) na lugha ya ishara, mawazo na chunguzi nyingi za Darwin zimethibitishwa na watafiti wa zama hizi duniani kote. Tangu kipindi hicho watafiti wengi wamegundua na kuhifadhi takribani na ishara za mwili milioni moja. Albert Mehrabian amebaini kua maneno huleta athari katika ujumbe kwa 7 %, na mijadala (tone of voive, inflection and other sounds) inaathiri ujumbe kwa 38 % na ishara huathiri ujumbe kwa 55 %.
Professor Birdwhistell alifanya makisio sawa na Albert Mehrabian kuhusu kiwango cha mawasiliano ya ishara yanayofanyika miongoni mwa watu. Alikisia wastani wa mtu kuwasiliana kwa maneno ni dakika 10 au 11 kwa siku na kila sentensi inachukua sekunde 2.5. kama ilivyokua kwa Mehrabian Professor Birdwhistell aligundua kua katika maongezi ya uso kwa uso mawasilano yam domo (verbal) yanatokea chini ya 35 %, na zaidi 65 ya maongezi yanafanyika kwa ishara ( nonverbal).
Watafiti wengi wa zama hizi wamekuli kua kimsingi maelezo ya mdomo hutumika kwenye kuwasilisha ujumbe wa maelezo tu na ishara hutumika kujadili mitazamo ya mtu mwenyewe, na wakati mwenigine hutumika kama mbadala wa maelezo ya mdomo. Kwa mfano mwanamke anaweza kumuangalia mwaname kwa mtazamo ujulikanao kwa lugha ya kiingereza “look to kill” na kufikisha ujumbe wa wazi kabisa bila ya kufungua mdomo.
Birdwhistell anasema bila ya kuzingatia utumaduni, mtu aliyefundishwa vizuri anaweza kuelezea nyenendo za mtu kwa kusikiliza sauti yake. Vile vile Birdwhistell alijua namna ya kuwelezea lugha inayozungumzwa na mtu kwa kuangalia ishara (gesture) tu.
Jambo la kuvutia mwanadamu hua hana habari na mikao (postures), nyenendo, ishara (gestures) ambayo inaleza mengine wakati sauti yake inasema mengine.

INAENDELEA……..
 
Brother ibnuislam79, tunataarifiwa kwamba "kitabu kile" hakikubakiza kitu kwa mambo yote yahusuyo maisha ya mwanadamu na hata dunia yetu hii. Naomba kufahamu kama uliyoelezea kwenye mada yako hii yamefafanuliwa ndani ya "kitabu cha zama zetu" na ni mistari ipi.
 
Kila jambo lina mahala pake.
 
LUGHA YA ISHARA (BODY LANGUAE)- 1
UTANGULIZI:
Na Mummed Ibnul Islam

Kwa kadri tulivyokua tunakaribia karne ya 20, tulishuhudia uibukaji wa aina mpya wa wanasayansi jamii wajulikanao kama wanasayansi wa lugha ya ishara (non-verbalists.
Kama vile mlinzi wa ndege anapofurahi kuangalia ndege na tabia zao, basi hivyo hivyo mwanasayansi wa lugha ya ishara hurahi kuwangalia wanaadamu na tabia zao. Huwatazama sehemu za kazi, kwenye fukwe, kwenye T.V, ofisini au sehemu nyengine yoyote ile ambayo kuna wanaamiliana. Anakua mwanafunzi anayetaka kujua matendo ya binadamu wenzie. Ili mwishoe ajijue yeye mwenyewe na ajue namna ya kuimarisha mahusiano yake na wenzie.
Inaonekana ni ajabu kua katika kipindi miaka milioni moja au zaid kipengele cha mawasiliano ya lugha ya ishara kilikua kinasomwa lakini ni katika miaka ya 1960 tu ndio watu waliapoanza kujua uwepo wake, pale Julius Fast alipochapisha kitabu kinachohusu lugha ya ishara mwaka 1970. Huu ulikua ni mukhtasari wa kazi zilizofanywa na wanasayansi wa tabia za viumbe (behavioural scientists) kuhusu mawasiliano ya ishara (non-verbal communications).
Pamoja na hayo lakini mpaka leo watu hawana habari na uwepo wa lugha ya ishara (body language) ukiacha umuhimu wake kwenye maisha yao.
Charlie Chaplin na waigizaji wengine wa filamu zisizo na maongezi ya sauti ni miongoni mwa viongozi wa mawasiliano ya ishara. Wao ndio waliokua njia ya mawasiliano kwenye T.V. kila muigizaji aliwekwa kundi la waigizaji wazuri ua katika kundi la waigizaji wabaya kwa kutumia kigezo cha uwezo wake wa kutumia ishara (gestures) na ishara nyengine za mwili (body signals) katika kufanya mawasiliano kwa ufanisi zaidi. Hivyo tunapozungumzia filamu zilikua maarufu na zilizokosa umaarufu uzito mkubwa uliwekwa kwe kipengele cha kuigiza kwa kutumia mawasiliano ya ishara, hivyo waigizaji wengi wa filamu za mawasiliano ya ishara walififia kidogo kidogo na mwishowe kupotea na kutojulikana. Na wale mahiri katika mawasiliano ya mdomo walishinda.
Kitabu ambacho kilikua na ushawishi mkubwa kuhusu lugha ya mawasiliano kabala ya karne ya 20 ni cha Charles Darwin “The Expression of Emotions in Mans and Animals” kilichochapishwa mwaka 1872. Kitabu hichi kimetoa tafiti za kisasa zinazohusu maelezo ya uson (facial expressions) na lugha ya ishara, mawazo na chunguzi nyingi za Darwin zimethibitishwa na watafiti wa zama hizi duniani kote. Tangu kipindi hicho watafiti wengi wamegundua na kuhifadhi takribani na ishara za mwili milioni moja. Albert Mehrabian amebaini kua maneno huleta athari katika ujumbe kwa 7 %, na mijadala (tone of voive, inflection and other sounds) inaathiri ujumbe kwa 38 % na ishara huathiri ujumbe kwa 55 %.
Professor Birdwhistell alifanya makisio sawa na Albert Mehrabian kuhusu kiwango cha mawasiliano ya ishara yanayofanyika miongoni mwa watu. Alikisia wastani wa mtu kuwasiliana kwa maneno ni dakika 10 au 11 kwa siku na kila sentensi inachukua sekunde 2.5. kama ilivyokua kwa Mehrabian Professor Birdwhistell aligundua kua katika maongezi ya uso kwa uso mawasilano yam domo (verbal) yanatokea chini ya 35 %, na zaidi 65 ya maongezi yanafanyika kwa ishara ( nonverbal).
……..
Nakubaliana na wewe katika hilo. Lugha ya ishara inachukua % kubwa sana katika mazungumzo kwa sababu mtu anavyofikiri ndivyo anavyoishi au anavyofikiri ndivyo anavyotenda/ kuongea. Na naamini(ikiwa nimekosea nirekebishe) ishara huwa zinatokana na hisia, na hisia ndiyo inayozalisha ishara katika yale mtu anayoyazungumza. Kwa maana nyengine yanakuja" automatic ". Na katika ishara ndiyo tunajua mtu analolizungumza lina u' serious wa namna gani. Wakati mwengine kwa ishara tu anazozionesha mtu unafahamu mantiki ya kinachomsibu/uzito wa anachokizungumzia wala uhitaji ziada ya maelezo marefu.
 
Back
Top Bottom