Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,428
LUCY MAYENGA AAMINIWA NA WAJUMBE KWA KURA 7,814 JIMBO LA KISHAPU
Ndugu Lucy Mayenga ameibuka kinara katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge wa Jimbo la Kishapu baada ya kushinda kwa kupata kura 7,814.
Matokeo hayo yaliyotangazwa na CCM Wilaya ya Kishapu yanaonesha Mayenga akiwapiku kwa mbali wagombea wengine sita waliokuwa wakichuana naye kwenye mchakato huo.
Aliyemfuata kwa kura ni Bonda Nkinga aliyepata kura 1,730, akifuatiwa na Boniphace Butondo mwenye kura 1,290. Wengine ni Dotto Kwigema (597), George Jimisha (590), Madaha Chabba (503) na John Nhyamah (432).
Ushindi huo unampa Mayenga nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba endapo atapitishwa na vikao vya juu vya chama hicho.