Lubuva: Mgombea mmoja UKAWA sawa

Lubuva: Mgombea mmoja UKAWA sawa

msemakweli

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
1,627
Reaction score
880
Mkuu MwanaDiwani sijui kama umepata fursa ya kulisoma gazeti la mwananchi la leo. Nakumbuka thread yako hapa ukisema kwamba kwa sheria za sasa UKAWA hawawezi kusimamisha mgombea mmoja. Nadhani suali lako limejibiwa vyema.[

=======================

mbowe_lipumba.jpg

Viongozi wa vyama vya upinzani nchini kutoka kushoto: James Mbatia(NCCR Mageuzi)
Freeman Mbowe (Chadema) na Profesa Ibrahimu Lipumba(CUF)

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva amesema mpango wa vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wa kusimamisha mgombea mmoja katika Uchaguzi Mkuu mwakani ni halali kisheria.

Vyama vinavyounda Ukawa ni NCCR-Mageuzi, CUF, Chadema na NLD.

Jaji Lubuva alisema hayo jana mjini Dodoma katika semina ya siku mbili ya Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania ya kuwahamasisha wadau wa siasa kudumisha amani na utulivu ambayo ilihudhuriwa na vyama vyote vyenye usajili wa kudumu nchini isipokuwa Chadema na CUF.

"Wanaposema katika wilaya fulani wanasimamisha mgombea wa chama fulani hawaundi chama, ni kwamba pale wanaachia chama fulani, wanakiunga mkono kwa hivyo hapo sheria inaruhusu kabisa," alisema Jaji Lubuva na kuongeza:

"Nadhani huo ndiyo ukweli wao siyo lazima waende wakaandikishe chama. Wanasema chama X kule Iringa tunamsimamisha fulani na wengine wanamuunga mkono, hilo si tatizo."

Jaji Lubuva alisema hayo baada ya Mwenyekiti wa Baraza hilo, Peter Mziray kusema sheria hairuhusu Ukawa kuungana.

"Hawa wanataka kuvunja sheria... wanawaambia uongo Watanzania kwamba watasimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi," alisema Mziray ambaye pia ni Rais Mtendaji wa Chama cha APPT Maendeleo na kuwataka wanasiasa kufuata sheria za nchi ili kuepuka machafuko nchini.

Akichangia katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa NCCR- Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema kitabu cha maadili ya vyama katika uchaguzi kinaruhusu vyama kushirikiana na ndiyo sababu walipokuwa wanazunguka nchini, chama kimoja katika umoja huo ndicho kilikuwa kikiomba kibali cha kufanya mkutano.

Amani na Utulivu

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula alisema uvunjifu wa amani katika uchaguzi unachangiwa na tofauti kubwa za kimapato. Alisema jinsi pengo kati ya maskini na tajiri linavyozidi kuwepo, amani haiwezi kuwepo.

Akifungua semina hiyo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha - Rose Migiro, alivitaka vyama vya siasa nchini kufahamu kuwa kujenga amani na utulivu ni lengo lao la kudumu.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha, Gaudence Mpangala alisema yapo mambo matatu; ujenzi wa demokrasia kitaifa, ushiriki wa jamii katika siasa, uchumi na maendeleo ya jamii ambayo yanatakiwa kufuatwa ili kudumisha amani na utulivu.

Mwanasiasa mkongwe, Getrude Mongella alisema nchi imefika mahali mtu anatoa matamshi ya uvunjifu wa amani lakini hachukuliwi hatua.

Makamu Mwenyekiti wa UDP, Issack Cheyo alivishutumu vyama vikubwa vya siasa kwa kuwa vyanzo kuvunja makubaliano ya maadili ya uchaguzi... "Tulikubaliana kuwepo kwa nafasi sawa katika kutangaza sera kwenye vyombo vya habari lakini chama kimoja kinapewa nafasi kubwa katika vyombo vya habari."

Chanzo:Mwananchi
 
Hapo hakuna cha akidi wala 2/3 wala mambo ya kupiga kura kwa Facebook au tweeter, Chezea UKAWA wewe......................
 
...ccm hawasomi nyakati,watashangaa wasira kule,lukuvi kuleeeeee,kwa hali ilivyo waage tu.
 
Nimefedheheka sana kwa kauli ya mtu niliyekua namuheshimu kwa kiasi fulani japo kidogo kama huyo anayejiita Rais Mtendaji wa APPT-Maendeleo.

I'm very disappointed !

Msomi mzuri kama huyu anapojipendekeza na kupotosha kiasi cha kuchimbia taaluma na weledi wake mchangani si jambo la kheri kwake na wala chama chake.

Hivi 1995 tulipomuunga mkono mgombea wa NCCR-Mageuzi au 2000 tulipowaunga Mkono CUF tulivunja chama chetu?

Na ni nani alimwambia UKAWA ni chama cha Siasa?

Tukifanya ushirikiano tutakua tumevunja sheria ipi?

Nonesense ! ! !
 
Kuna mwalimu wa chuo kikubwa anaitwa Dr. Bana, hapendi kabisa kuisikia hii.
 
Jambo zuri nimkwamba tunazidi kupata kundi la waigizaji wengi,tulikuwa na comedi baadaye tukapata futuhi na sasa ukawa safi sana tunasonga mbele.
 
Kuna mwalimu wa chuo kikubwa anaitwa Dr. Bana, hapendi kabisa kuisikia hii.

Mkuu wasomi wetu elimu zao zipo mifukoni mwa viongozi ,wanabakia kama magarasha tu achana nao.
 
Nimefedheheka sana kwa kauli ya mtu niliyekua namuheshimu kwa kiasi fulani japo kidogo kama huyo anayejiita Rais Mtendaji wa APPT-Maendeleo.

I'm very disappointed !

Msomi mzuri kama huyu anapojipendekeza na kupotosha kiasi cha kuchimbia taaluma na weledi wake mchangani si jambo la kheri kwake na wala chama chake.

Hivi 1995 tulipomuunga mkono mgombea wa NCCR-Mageuzi au 2000 tulipowaunga Mkono CUF tulivunja chama chetu?

Na ni nani alimwambia UKAWA ni chama cha Siasa?

Tukifanya ushirikiano tutakua tumevunja sheria ipi?

Nonesense ! ! !
Vipi mzee,
kaa kwenye vijiwe vya kahawa na wazee wenzako haya mambo ya vijana huyawezi waambie bavicha waje tujadiliane siyo wazee kama wewe ushachoka.
 
Sasa ikitokea wakakorofishana huko mbele hali itakuwaje?
 
Nimefedheheka sana kwa kauli ya mtu niliyekua namuheshimu kwa kiasi fulani japo kidogo kama huyo anayejiita Rais Mtendaji wa APPT-Maendeleo.

I'm very disappointed !

Msomi mzuri kama huyu anapojipendekeza na kupotosha kiasi cha kuchimbia taaluma na weledi wake mchangani si jambo la kheri kwake na wala chama chake.

Hivi 1995 tulipomuunga mkono mgombea wa NCCR-Mageuzi au 2000 tulipowaunga Mkono CUF tulivunja chama chetu?

Na ni nani alimwambia UKAWA ni chama cha Siasa?

Tukifanya ushirikiano tutakua tumevunja sheria ipi?

Nonesense ! ! !

Au 2010 Dovutwa alipojitoa kugombea uraisi na kutangaza yeye na chama chake wanamuunga Kikwete katika mbio za Uraisi!!
 
wanacheza mbwa kachoookaaa mgombea wa ccm ndiye rais na wanafahamu hili basi tu wanachechetuuukaaa
 
Jambo zuri nimkwamba tunazidi kupata kundi la waigizaji wengi,tulikuwa na comedi baadaye tukapata futuhi na sasa ukawa safi sana tunasonga mbele.

Hekima ya mjinga ni kukaa kimya, sasa wewe naona hata hiyo hekima ndogo tu umekosa. Nawasikitikia sana wazazi waliokuzaa.
 
Back
Top Bottom