Lubuva: Mgombea mmoja UKAWA sawa

Lubuva: Mgombea mmoja UKAWA sawa

mbowe_lipumba.jpg
lubavu_clip.jpg

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva amesema mpango wa vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wa kusimamisha mgombea mmoja katika Uchaguzi Mkuu mwakani ni halali kisheria.

Vyama vinavyounda Ukawa ni NCCR-Mageuzi, CUF, Chadema na NLD.

Jaji Lubuva alisema hayo jana mjini Dodoma katika semina ya siku mbili ya Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania ya kuwahamasisha wadau wa siasa kudumisha amani na utulivu ambayo ilihudhuriwa na vyama vyote vyenye usajili wa kudumu nchini isipokuwa Chadema na CUF.

“Wanaposema katika wilaya fulani wanasimamisha mgombea wa chama fulani hawaundi chama, ni kwamba pale wanaachia chama fulani, wanakiunga mkono kwa hivyo hapo sheria inaruhusu kabisa,” alisema Jaji Lubuva na kuongeza:

“Nadhani huo ndiyo ukweli wao siyo lazima waende wakaandikishe chama. Wanasema chama X kule Iringa tunamsimamisha fulani na wengine wanamuunga mkono, hilo si tatizo.”

Jaji Lubuva alisema hayo baada ya Mwenyekiti wa Baraza hilo, Peter Mziray kusema sheria hairuhusu Ukawa kuungana.

“Hawa wanataka kuvunja sheria... wanawaambia uongo Watanzania kwamba watasimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi,” alisema Mziray ambaye pia ni Rais Mtendaji wa Chama cha APPT Maendeleo na kuwataka wanasiasa kufuata sheria za nchi ili kuepuka machafuko nchini.

Akichangia katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa NCCR- Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema kitabu cha maadili ya vyama katika uchaguzi kinaruhusu vyama kushirikiana na ndiyo sababu walipokuwa wanazunguka nchini, chama kimoja katika umoja huo ndicho kilikuwa kikiomba kibali cha kufanya mkutano.


Amani na Utulivu
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula alisema uvunjifu wa amani katika uchaguzi unachangiwa na tofauti kubwa za kimapato. Alisema jinsi pengo kati ya maskini na tajiri linavyozidi kuwepo, amani haiwezi kuwepo.

Akifungua semina hiyo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha - Rose Migiro, alivitaka vyama vya siasa nchini kufahamu kuwa kujenga amani na utulivu ni lengo lao la kudumu.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha, Gaudence Mpangala alisema yapo mambo matatu; ujenzi wa demokrasia kitaifa, ushiriki wa jamii katika siasa, uchumi na maendeleo ya jamii ambayo yanatakiwa kufuatwa ili kudumisha amani na utulivu.


Mwanasiasa mkongwe, Getrude Mongella alisema nchi imefika mahali mtu anatoa matamshi ya uvunjifu wa amani lakini hachukuliwi hatua.

Makamu Mwenyekiti wa UDP, Issack Cheyo alivishutumu vyama vikubwa vya siasa kwa kuwa vyanzo kuvunja makubaliano ya maadili ya uchaguzi... “Tulikubaliana kuwepo kwa nafasi sawa katika kutangaza sera kwenye vyombo vya habari lakini chama kimoja kinapewa nafasi kubwa katika vyombo vya habari.”

Chanzo: Mwananchi



 
Mpango wa kuachiana wagombea katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi ilishatokea mara kadhaa kama uchaguzi mkuu uliopita Chadema walimwachia jimbo la Kyera Makiembe. NI jambo la kawaida na si Tanzania tu, hayo hutokea katika nchi mbalimbali duniani kwa vyama vya siasa vinavyokuwa na uhusiano mzuri kwa manufaa ya taifa.
 
Mpango wa kuachiana wagombea katika baadhi ya majimbo ya uchaguzi ilishatokea mara kadhaa kama uchaguzi mkuu uliopita Chadema walimwachia jimbo la Kyera Makiembe. NI jambo la kawaida na si Tanzania tu, hayo hutokea katika nchi mbalimbali duniani kwa vyama vya siasa vinavyokuwa na uhusiano mzuri kwa manufaa ya taifa.

Tehe tehe, CHADEMA hawana ubavu wa kuweka mgombea jimbo la MWAKYEMBE acha kutudanganya wewe, tangu lini CCM na CHADEMA wakashirikiana?
 
ni kitu kile kile wala sijaona jipya, hivi tuchukulie mfano, ARUSHA mjini CUF na NCCR walikuwa wanapata kura ngapi mpaka ziathiri matokeo kwa CCM?
 
Nilimuona Jaji Mstaafu Lubuva akiwa anamjibu Bwana Peter Kuga Mziray kuhusu UKAWA kusimamisha mgombea mmoja kwenye chaguzi. Mziray alikuwa akidhani kwamba wagombea watasimama kwa tiketi ya chama kinachoitwa UKAWA!! Akasema hakuna sheria inayoruhusu hivyo.

Alikuwa haelewi kwamba mpango ni kuachiana majimbo/Urais na wagombea watasimama kwa tiketi za vyama vyao. Kama makubaliano ni kwamba CHADEMA inamsimamisha Halima Mdee Kawe basi vyama vingine ndani ya UKAWA havitasimamisha mtu jimboni Kawe bali vitamuunga mkono Halima Mdee.

Vivyo hivyo, kama UKAWA watakubaliana kumsimamisha Prof. Ibrahim Lipumba kwenye Urais basi Prof. atagombea kwa tiketi ya CUF na CHADEMA, NCCR- MAgeuzi na NLD havitasimamisha mgombea Urais
.

Tatizo ni kwamba huenda watu wakawa wanamtafuta mgombea kwa tiketi ya UKAWA wakawa hawamuoni!!!
 
''Mziray ambaye pia ni Rais Mtendaji wa Chama cha APPT Maendeleo''

Kumbe....................
 
Wakuu tunazunguka mbuyu tu...sheria ilipaswa kuruhusu coalition...kuna tofauti kubwa sana kuachiana majimbo na kumuweka mgombea mmoja akiwakilisha coalition
 
Back
Top Bottom