Lowassa zingatia ushauri huu kama utaachwa kwenye uteuzi

Lowassa zingatia ushauri huu kama utaachwa kwenye uteuzi

magode

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2014
Posts
2,204
Reaction score
3,340
Wanabody,
Salaam;

Kwa sasa macho na masikio yapo Dodoma kwenye vikao vya uteuzi wa mgombea urais kupitia CCM.

Katika kundi la wagombea 38 Mh. Edward Lowassa ndiye mgombea pekee anayeonekana kuihitaji sana nafasi hiyo kuliko wagombea wote akifuatiwa na Bernad Membe. Lowassa ni Muathirika wa kisaikolojia kutokana na kashfa iliyomfanya aachie uwaziri mkuu, anachofanya kwa sasa ni kama kutafuta tiba ya tatizo lake.

Kwa mtazamo wake anaamini akipata Uongozi wa juu wa nchi itakuwa nafasi ya kutakasika kwake.

Nachukua fursa hii kumpa ushauri muhimu wa maisha yake na Familia yake.

→Iwapo atateuliwa kupeperusha bendera ya CCM, ajiepushe na visasi, asijibu tuhuma dhidi yake na wala asijaribu kufanya kampeni za kupakana matope. Asimamie msingi wa kampeni kwa kunadi Ilani atakayopewa na chama chake.

→Iwapo CCM watamuacha asijidanganye kuhama chama, akifanya hivyo athari zake ni kubwa sana kwake ingawa wapambe wake wanaweza kumpotosha..! Akienda chama kingine, kwanza hatashinda na baada ya uchaguzi atakuwa hana tena mahali pa kujificha na ataanza kutengeneza mgogoro wa kutaka madaraka katika chama chake kipya.

Maisha baada ya uchaguzi yatakuwa mabaya zaidi kiuchumi, kisiasa na hata kiafya kutokana na athari za kisaikolojia.
Asipokuwa na utulivu na kuzingatia ushauri huu, baada ya uchaguzi tunaweza hata kumuimbia nyimbo za huzuni akiwa mbele ya haki.

Wapambe wa Lowassa kazi kwenu kumhabarisha huyu kiongozi.

Nawasilisha.
 
Ushauri mzuri..naona vijana mmepangwa kumuandaa mzee kisaikolojia
Hakuna aliyetupanga mkuu,mitazamo yake jinsi ilivyo ni muhimu ashauriwe na asipokuwa makini na kuchukua ushauri km huu,baada ya uchaguzi ntakuja kuufufua huu uzi ili watu wajue kwa nn tulimshauri mapema.
 
hatutaki ushauri wako lowasa ndio chaguo la wantanzania hata ukawa wanamugwaya sana
 
magode, akiingia UKAWA hatashinda sio? Unacheza wewe..! Yaliyotokea Nigeria yapo mbioni kwetu tena uzuri ni kwamba atakayewekwa na CCM atakuwa mgombania Urais mpya
 
ilani ya chama ipi wakati jamaa ana ilan yake kabisaaaa kasema kipaumbele chake elimu sasa kama ilani itasema inataka kilimo kwanza hapo mgogolo utakuwa tayari
 
Acha ukanjanja hakuna asieutaka urais ndomaana wote wamechukua form hata yule mkulima anautaka pia sio lowassa pekeyake mkuu
 
magode, akiingia UKAWA hatashinda sio? Unacheza wewe..! Yaliyotokea Nigeria yapo mbioni kwetu tena uzuri ni kwamba atakayewekwa na CCM atakuwa mgombania Urais mpya
Mkuu Geza Ulole sidhani km ukawa wanaweza kukubali kumsimamisha Lowassa wakati kuna watu wanaokubalika na wasafi kuliko yeye. Anaweza kupokelewa ukawa km mwanachama lkn hawezi kuteuliwa kugombea. Akihama ccm,sidhani km anaweza kwenda ukawa kwa watu wanaomzidi kila kitu,nadhani anaweza kwenda act. Huko atapokelewa lkn hatashinda na baada ya uchaguzi atataka awe kiongozi mkuu na zitto hatakubali hasa km nae atapoteza ubunge.
 
Last edited by a moderator:
Hata mama yako agombei urais lakini pia tunaweza tuka muweka mbeye ya haki,na tukaimba mbio za uzuni..
 
Acha ukanjanja hakuna asieutaka urais ndomaana wote wamechukua form hata yule mkulima anautaka pia sio lowassa pekeyake mkuu
Mkuu hebu rudi usome vizuri bandiko langu,urudi usome na ulichokiandika..! Au ntakupa kazi usiyo na uwezo nayo?? Sijachanganya na neno hata moja la kisukuma lkn bado hujaelewa..!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom