MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
Uongozi bora ni msingi wa kujenga jamii yenye maadili mema, kuthamini utamaduni, uadilifu, kuheshimu utawala wa sheria na kutokuwepo na rushwa na maovu mengine.
Uwazi wa viongozi kuhusu mali zao na mienendo yao ya kiuongozi ni takwa la chini kabisa katika uongozi wenye kuzingatia misingi ya maadili, nidhamu na uwajibikaji kwa umma.
Kwa msingi huu ndiyo maana vyama vya siasa kama ACT-Wazalendo kinamtaka kikatiba kila kiongozi wake kutaja mali zake.
Umuhimu wa dhana ya uwazi umedhihirika ndani ya CHADEMA baada ya kujikuta baadhi ya wabunge wa CHADEMA wakimshambulia Lowassa bila kufahamu kutokana na kutofahamu vizuri mali zake.
Mbunge Mnyika alianza kulalamika na kulaani wale ambao wamezuia Mradi wa Maji kuwafikia wana Dar es Salaam kwa sababu wamejenga nyumba juu ya njia ya mabomba ya maji na kusababisha mradi wa maji kusimama. Bahati mbaya Mnyika hakufahamu kuwa aliyejenga hiyo nyumba ni Kaka yake na Edward Lowassa ambaye alipewa kiwanja na Edward Lowassa wakati akiwa Waziri wa Ardhi na Makazi mwaka 1993–1995.
Mbunge mwingine aliyelalamika ni Mbunge wa CHADEMA wa Jimbo la Monduli, Julius Karanga wakati akichangia majadiliano ya makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, bungeni.
Karanga aliitaka serikali iwagawie wananchi shamba la Makuyuni lenye ekali zaidi ya 380,000 ililopo wilayani Monduli kwa sababu serikali imelitelekeza. Karanga alidhani mwenye shamba kwa sasa ni serikali bila kufahamu kuwa baada ya serikali kulitaifisha kutoka kwa Mfanyabiashara Stein ili ligawiwe kwa wananchi, Edward Lowassa alijimilikisha hilo shamba.
Mbunge huyu pamoja na wabunge wangine wa CHADEMA walipigwa butwaa baada ya kuambiwa hilo shamba alijimilikisha Edward Lowassa lakini Waziri Lukuvi, akasema kuwa serikali imesikia kilio cha mbunge Karanga kwa sasa iko mbioni kuligawa kwa wananchi.
‘’Kama Mheshimiwa Mbunge, Karanga alikuwa hajui kwamba shamba hilo la makuyuni alijimilikisha Lowassa, basi imekula kwake, shamba linachukuliwa na serikali na kuligawa kwa wananchi. Najua kazi ni ngumu kwako, lakini naomba tushirikiane shamba hili liende kwa wananchi. "Ninayo hati hapa ya shamba hilo imesainiwa na Lowassa, nasema tutairekebisha ili shamba hilo ligawiwe kwa wananchi." alisema Lukuvi huku wabunge wengine wakicheka.
Lowassa anatakiwa awasaidie wana CHADEMA kwa kuwaeleza mali zake ili wasijikute wanampiga ‘’madongo’’ ya kisiasa wakidhani wanaipiga serikali bila kufahamu kutokana na ukosefu wa uwazi kutoka kwa Lowassa.
Hii inadhirihisha kuwa wanaCHADEMA wengi hawamjui Edward Lowassa pamoja na kuimba nyimbo zinazosema Mabadiliko Lowassa, Lowassa Mabadiliko.
Niliwahi kusema, katika mambo yote ambayo Lowassa amelitendea haki taifa ni kuhama CCM.
VIDEO ikionyesha nyumba ya Kaka yake Edward Lowassa ikibomolewa kwa nguvu na serikali kupisha ujenzi wa bomba la maji.
Hoja yangu haihusu CCM. Mambo ya CCM yanaingia vipi hapa?MwanaDiwani aka MsemajiUkweli,
Kauli ya Kikwete kwenye kamati kuu yenu huko CCM kwamba Lowassa bado ni tishio ni kauli inayowasumbua sana. Kutangaza mali za Lowassa sio kazi ya Chadema, kama ilivyokuwa kwa mali za Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli, hiyo sio kazi ya Chama Cha Mapinduzi. Kama ana mali ambazo mna uhakika ni mali 'haramu', zipo njia za kufuata kukabiliana na hilo, na mnazijua. Na katika njia zote, Jamififorums sio njia sahihi.
Vinginevyo kwa akili ya kawaida, tena sana, na kwa experience ya marais waliopita huko nyuma, kilicho muhimu kwa sasa ni kwa Rais aliyepo madarakani kuonyesha kile alichowasilisha kwa tume ya maadili kuhusu mali zake. Kwanini 'yaliyomo' hayajawekwa hadharani' na badala yake yana fichwa fichwa kama kweli nia ya dhati ipo?
Vipi kuhusu makato ya kodi ya mshahara wa Rais?
Onyesheni njia, ongozeni kwa mfano.
Wananchi wa Monduli wanakunywa supu sio Chai...ndio maana mbunge wao akahoji kuhusu ardhi...kumbe ni ya Laigwanani wa EAC teh teh teh!Tunataka sukari huu sio muda wa propaganda.
Mkuu, sukari nenda ukanunue dukani au kiwandani.Tunataka sukari huu sio muda wa propaganda.
You presented it as a partisan issue, so you cant claim impartiality katika hili. CCM ni chama kama ilivyo kwa CHADEMA.Hoja yangu haihusu CCM. Mambo ya CCM yanaingia hapa?
Nani amekuambia nataka CHADEMA itangaze Mali za Lowassa? Soma vizuri mada yangu na uelewe.
Tatizo likitamkwa jina la Edward Lowassa mnaibuka haraka kutoka kwenye mapango bila hata kuelewa msingi wa hoja na matokeo yake mnaanza kujenga hoja za nguvu badala ya nguvu za hoja.
Hivi vitisho vya jina la Lowassa havikumzuia Mangula THE SLAYER kufanya yake...kwi kwi kwi!!You presented it as a partisan issue, so you cant claim impartiality katika hili. CCM ni chama kama ilivyo kwa Chadema.
The inference is quite clear. Lowassa doesn't exist in a Vacuum.
Likitamkwa jina la Lowassa hata ndani ya Kamati Kuu ya CCM, matumbo yanawasokota. Msingi wa hoja yako ni kwamba Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Kikwete ameendelea kutoa tahadhari kwamba Lowassa bado ni Mwiba kwa CCM, na 2020 anaweza kuwapiga mweleka kama alivyowapiga mweleka 2015 mkaiba kura. Naomba nisaidie majibu kwa swali hili:
Kwanini Rais Magufuli hajatangazia CCM na umma kwa ujumla kuhusu mali zake?
Hata mimi ninashangaa kwa sababu hata wabunge wa CHADEMA ambao ni wajumbe wa Kamati Kuu inaonekana hawamjui Edward Lowassa.Ina maana hawakumhoji kuhusu mali zake siku ile inayosemwa alitoa ufafanuzi wa kina ndani ya kamati kuu ya Chadema??
Ha ha ha ....kweli ile ilikuwa gia ya angani haswa!
Sukari bei juu halafu unkuja na hoja ya kutupotezea maboya.Mkuu, sukari nenda ukanunue dukani au kiwandani.
Kumbuka siyo wote wanatumia sukari.
Lowassa anatakiwa awasaidie viongozi wa CHADEMA kwa kuwaambia mali zake ili kuepuka aibu ya kisiasa wanayoipata kwa sababu ya kukosekana uwazi wa mali zake.Uko sawa CHADEMA ilipotea baada ya kumuuzia chama Lowasa!
Mkuu mimi mwenyewe situmii chai ila nawatetea majority.Uko hapo.Wananchi wa Monduli wanakunywa supu sio Chai...ndio maana mbunge wao akahoji kuhusu ardhi...kumbe ni ya Laigwanani wa EAC teh teh teh!
MsemajiUkweli,
Kauli ya Kikwete kwenye kamati kuu yenu huko CCM kwamba Lowassa bado ni tishio ni kauli inayowasumbua sana. Kutangaza mali za Lowassa sio kazi ya CHADEMA, kama ilivyokuwa kwa mali za Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli, hiyo sio kazi ya Chama Cha Mapinduzi. Kama ana mali ambazo mna uhakika ni mali 'haramu', zipo njia za kufuata kukabiliana na hilo, na mnazijua. Na katika njia zote, Jamiiforums sio njia sahihi.
MsemajiUkweli, Kuonyesha nyumba ya mdogo wa Lowassa ikibomolewa inaweza kuwa ni sawa tu na kuonyesha ile nyumba ya Kikwete Masaki inayojengwa na Lugumi. Haitatui tatizo lililopo.
Vinginevyo kwa akili ya kawaida, tena sana, na kwa experience ya marais waliopita huko nyuma, kilicho muhimu kwa sasa ni kwa Rais aliyepo madarakani kuonyesha kile alichowasilisha kwa tume ya maadili kuhusu mali zake. Kwanini 'yaliyomo' hayajawekwa hadharani' na badala yake yana fichwa fichwa kama kweli nia ya dhati ipo?
Vipi kuhusu makato ya kodi ya mshahara wa Rais?
Onyesheni njia, ongozeni kwa mfano.
Hivi vitisho vya jina la Lowassa havikumzuia Mangula THE SLAYER kufanya yake...kwi kwi kwi!!
Kipi muhimu kwa taifa hivi sasa kati ya umma kujua mali za lowassa na mali za rais aliyepo madarakani? Kwanini yaliyowasilishwa na JPM tume ya maadili hayawekwi hadharani na badala yake mmeyaficha kwenye mkoba?Ina maana hata wewe siku hizi hutaki kuhoji mali za viongozi???
Hata wataalam wanasema matumizi ya sukari ya kutengeneza ni hatari kwa afya.Wananchi wa Monduli wanakunywa supu sio Chai...ndio maana mbunge wao akahoji kuhusu ardhi...kumbe ni ya Laigwanani wa EAC teh teh teh!
Mkuu kwa jinsi nilivyoilewa hii mada ni kwamba Lowasa awatangaze mali zake wabunge wa Chadema ili kuondoa mkanganyiko kwa wabunge wake huko Chadema isije kuonekana wanamsaliti bosi wao bila kujua.
Mimi Mwenyewe nilicheka sana baada ya kuona Lukuvi anaonyesha hati iliyosainiwa Na Lowasa kuhusu shamba linalolalamikiwa Na kijana wake....