mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 12,289
- 9,219
Ethiopia wana viongozi wenye uthubutuna sio hawa wa wakwetu ambao kazi ni keleletu za kutaka uraisi,Ethiopia pia wanajenga bwawa la kufua umeme katika mto Blue Nile ,ni mradi mkubwa na wanaujenga wenyewe,achana kabisa na Ethiopia sisi tumebaki kupiga siasa za kuchakachua rasimu ya katiba hiyo ndio tunaweza.Katika hao wanaogombania kuwa raisi bado sijamuona mtu ambaye kweli ana uchungu na maisha ya Watanzania na ambae ana vision ya kuwakomboa Watanzania,wote wanawaza mambo ya kujinufaisha wao na washirika wao,wanawaza kujitajirisha kwani wameshaona uraisi ni sehemu ya kuchuma na utajirisho.Siamini mtu anayechangisha marafiki(wafanyabiashara matapeli) zake michango ya harambee eti kusaidia shule,makanisa ,misikiti kama kweli atakuwa raisi bora wa nchi hii,kwani hao wanaotoa hizo fedha wana malengo yao ,wanajua wanayemtolea atakuja kulipa fadhila na kitendo cha kutoa hiyo misaada ni rushwa .Ikumbukwe kwamba mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni wala rushwa.