Mahakamani hatuendi ila tunashukuru kwamba yanayosemwa juu yake kumbe anayapata yote, ajiulize ni kwanini asemwe yeye?,kwani ana uzuri gani? na kama haridhiki basi atueleze ni kwanini amezunguka mitaani anagawa pesa hovyo hovyo ili iweje? huo si ufisadi? Biblia Takatifu inasema wazi asiye fanya kazi na asile, yeye kwenda kuwalipa watu 20,000 aliwapa kwa kumfanyia kazi gani? unampaje pesa mtu ambaye hauna makubaliano naye, kwa jambo gani? make hata Mungu anakataza, unampaje mtu pesa nyingi kiasi hicho bila ya yeye kufanya kazi yoyote na wakati imesema ni lazima kwanza huyo mtu afanye kazi, sasa ni malipo kwa kazi gani?
Najua watu wake watasema ilikuwa ni zawadi kwa vijana kuja kumpokea, sasa kumpokea tu? mbona akiwa waziri mkuu hakuwa anatoa hiyo zawadi wakati anapokelewa sehemu alizokuwa anaenda? Unamiliki mgodi kiasi gani wa pesa mpaka unaamua kuwapa zawadi wanaokuja kukupokea? na je, utaendelea kufanya hivyo hata ukipigwa chini kwenye NEC?