CosaNostra
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 382
- 139
Gazeti la mwananchi leo liliandika habari kuwa Mheshimiwa sana anataka ushahidi ili kuthibitishiwa kuwa yeye ni fasadi. Nadhani Mkapa amejenga utamaduni mbaya sana nchi hii. Utamaduni kuwa kila kitu mwananchi/wananchi wakikiona wanadaiwa kutoa ushahidi.Hii ilikuwa wakati akiwatetea watuhumiwa ufisadi miaka ya 2004/05.
Hivi kama ndIo stahili hiyo hata kutoa taarifa za uhalifu ingewezekana vp? Mfano Ukiona sura ngeni za watu na miendo ya kutia mashaka ukatoa taarifa polisi, ukidaiwa leta ushahidi utafanyaje?
Lowassa mambo mengine asiyafanye kuwatafuta watanzania ubaya bure, hivi anaweza kutuhakikishiaje namna alivyopata kumiliki mega ranch ya Mzeri kule Tanga akiwa yeye ni waziri wa mifugo. Si ufisadi huo? aliwezaje kuandika vinote huko Nishati na Madini na Tanesco na vika-copiwa na kamati ya Mwakyembe akiagiza Richmond wapewe kandarasi ya umeme, si ufisadi huo?
Kuhamisha kazi nyingi za wageni wa AICC kwa wale vijana wa kihindi kina Faisal wa EL Tours, si ufisadi huo? Hivi fedha hizo chekwa chekwa anazogawa anazipata kwa biashara gani?
Marafiki zake kama ndio wanaozitoa wanazitoa kwa nini? Kumbukeni Mwl. alisema Mtanzania wa sasa hawezi kununua watu bila yeye kwanza kununuliwa.
Circumstantial evidence zipo nyingi sana, ushahidi unatakiwa mahakamani bw, huku uraiani kesi ikiwa kwa wazee wanaangalia mazingira na kutaja ukweli, ukweli tu. Ndio ulivyo.
Samahani kwa hati chafu!