47pro
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 1,204
- 332
LOWASSA ACHA KUPOTOSHA UMMA, PUMZIKA AU TIMIZA AHADI YA KUCHUNGA. Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chadema, Ndg. Edward Lowassa siku ya jana akihutubia mkutano wa hadhara kata ya Mto wa Mbu alitoa tuhuma kadhaa kwa chama cha mapinduzi na serikali yake.
Baadhi ya madai ambayo ameyasema, ni kuwa wapo watu wanaozunguka kutaka kuwahonga madiwani wa chadema milion ishirini(20,000,000/=). Tungependa atumie jukwaa kuwataja hao anaodai kuwa wanapita kuwahonga hizo pesa. Tungependa kumwambia kuwa chama cha mapinduzi hakina huo muda wa kuwahonga hao madiwani. Atuambie hao madiwani wanahongwa kwa lengo lipi? Na hizo pesa zinatoka wapi? CCM imeshinda madiwani na wabunge wengi kuliko chama chochote kile. Sisi tunaamini alichokifanya Lowassa ni siasa uchwara za majukwaani.
Kwani anajua fika hakuna jambo kama hilo. Huo ni mwendelezo wake wa maigizo ambayo tayari watanzania washayajua tayari. Watanzania wanajua dhamira ya dhati ya serikali ya awamu ya tano katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi, uzembe na udanganyifu. Kwa hali ya nchi ilivyosasa hizo pesa zote anazodai zitatoka wapi? Ni vema akawa mkweli mana utamuweka huru.
Pia, Lowassa anadai Chama chake kilishinda uchaguzi mkuu wa 2015 ni dhuluma ilifanyika dhidi yake. Tungependa kumhakikishia kuwa CCM ilishinda kihalali kuanzia madiwani, wabunge na rais. Ushindi wa rais ni 62% ya kura zote. Waangalizi huru wa ndani na nje walithibitisha kwa ripoti zao bila shaka yoyote. Pia, awali tuhuma hizi zilitolewa na Chadema kuwa wanaushahidi wa kutosha kuuthibitishia umma kuwa waliibiwa kura, lakini mpaka sasa wameshindwa kuonyesha hjo ushahidi wao. Hivyo basi, tunaamini anachokifanya lowassa ni muendelezo wake wa maigizo.
Tunapenda aseme ukweli kwa wanachama wao na watanzania sababu ya wao kushindwa. Ni dhahiri kuwa sababu kubwa ya kushindwa kwa chadema ni kutoaminika na watanzania walio wengi na mambo mengi ambayo ni dhahiri ilipelekea wao kushindwa. Kauli aliyoitoa jana kudai kuwa Chadema imeishika pabaya CCM ni uongo uliopitiliza.
Sisi tunaamini kazi ya kutafuta ushindi wa 2020-2025 imeshakamilika tayari. Kasi ya serikali ya awamu ya tano katika kuwahudumjia watanzania na dhamira ya dhati aliyonayo Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli ni kielelezo tosha cha ushindi. CCM ina kazi moja tu ya kuhakikisha inasimamia utekelezwaji ea ilani yake ya 2015-2020. Tunapenda kumhakikishia watanzania wanajua ukweli ni upi na maigizo ni yapi. Tunamhakikishia 2020 ushindi utakuwa zaidi ya 80%.
Lowassa amejinasibu jana kuwa kitendo chake cha kukaa kimya ndicho kilichopelekea nchi kuwa katika amani tulinayo sasa. Tunapenda kumkumbusha kuwa hiyo sifa anazozitaja ni kwasababu tu ya malezi bora yaliyotukuka aliyoyapata akiwa CCM tangu alipozaliwa mpaka hivi sasa. Kwanza wanapaswa kuipongeza CCM, lakini pili anapaswa kutambua kuwa amani iliyopo imetokana na mungu kuzidi kuipenda Tanzania yetu.
Mhimili mwingine wa amani ya Tanzania ni waasisi wa taifa hili Hayati Baba wa taifa Julius Nyerere na Abeid Karume. Hivyo, kitendo cha yeye kujitukuza ni muendelezo wa siasa zake maigizo. Lakini tunampongeza pia kwa kutambua na kuwaeleza ukweli Chadema si chama cha kisiasa bali ni chama cha kiuanaharakati ambacho hakina dira ya kuliongoza taifa letu.
Kwakuwa ameliona hilo na kuamua kuwabadilisha kimfumo tunamsihi sana chama chao kijikite zaidi katika siasa za maendeleo na sio majungu na vurugu ambazo zimewafanya kutokuaminika kwa miaka yote 24. Mwisho, tunapenda kuwasihi watanzania wote kupuuza aina yoyote ya uchochezi ambao unafanywa na chadema.
Kwakuwa muda wa uchaguzi umekwisha, muda uliopo ni wakufanya kazi tu ili tulete maendeleo yetu. Vijana wa Chama cha mapinduzi hatutakubali kumvumilia yeyote ambaye atataka kulivuruga taifa letu. Tunamwambia tutakula naye sahani moja.
Tufanye kazi kwa bidii kuunga jitihada za rais wetu.
Hapa kazi tu