Lowassa, Sumaye wametumwa, Mbowe ni adui wa mabadiliko

Naambiwa Mzee Edward Lowassa mwamba wa siasa za Tanzania amerejea CCM.

Huu ni ushindi mkubwa kwa Lowassa mwenyewe na vyama vya Upinzani.

Lowassa atapata posho zake za uwaziri mkuu bila mizengwe.

Lowassa kwa umri wake na hadhi yake si mtu wa kushinda mahakamani au gerezani kwa mapambano ya kidemokrasia.

Mkwe wake Sioi Sumari kama sijajosea jina yupo ndani kwa kosa la uhujumu uchumi tangu 2016.

Kwa kipindi chote hicho,binti wa Lowassa anaishi kama mjane kwa kumkosa mume wake,

Kurejea kwa Lowassa CCM ni fursa kwa mwanae kumpata mume wake mapema ndani ya miezi mitatu ya mwanzo.

Hivi mlitaka Lowasa abaki upinzani huku akijua chaguo la Upinzani ni Lissu au Zitto halafu abaki huko kwa faida gani wakati mkwe wake anateseka gerezani?

Mzee Lowassa kajitendea haki yeye,familia yake pamoja na mkwe wake.

Mzee kaamua kuzichanga na kubani kuwa kurudi CCM kuna faida nyingi kuliko kubaki upinzani ambako si chaguo lao tena kwenye uchaguzi mgumu saana wa 2020.

Kwa upande wa upinzani nako ni sherehe.

Kuondoka kwa Lowassa kumetoa fursa kwa upinzani kujipanga mapema.

Upinzani ungeumizwa endapo Lowassa angejiondoa Upinzani katikati ya kampeni za mwaka 2020.

Kuondoka kwa Lowassa kwa hiyari yake kumeunusuru upinzani na Migogoro ya ndani ambayo kwa sasa ipo ndani ya CCM kuliko upinzani.

Kama wangemuengua Lowassa kwa nguvu na yeye kuamua kuwavuruga kama anavyofanya Lipumba,hakika upinzani ingebidi usubiri hadi 2025.

Lakini kwa kitendo cha kiungwana alichofanya Mzee Lowassa kutotaka usumbufu na kuvunjiwa heshima,ameamua kujiondoa mwenyewe .

Kurejea kwa Lowassa CCM ni sawa na kuamua kustaafu siasa akiwa ndani ya chama kilichomlea. Hii ni faida kwake binafsi kwakuwa ataendelea kunufaika na mfumo ikiwa CCM itadumu nadarakani.

Familia yake haitataifishwa mali zao hata siku Lowassa akiaga Dunia siku mwenyezi mungu akimuita.

Vijana wa upinzani sitegemei mumtukane ,kumzodoa na kumkejeli Mzee wetu huyu ambae ameusaidia upinzani kupata viti vingi bungeni kutokana na ushawishi wake.

Siasa ni wakati,Mzee amesoma vizuri alama za nyakati.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi sio mwanachama wa chama chochote lakini kwa elimu yangu ndogo niliyo nayo nimeanza kuwa na mashaka na uwepo wa Lowassa CHADEMA. Baada ya kufatilia kauli zake nyingi nimegundua anaibadilisha taratibu CHADEMA kuwa kama CCM.
CHADEMA ni chama chenye wafuasi wenye nembo ya uaminifu,utiifu,ukweli na uwazi not double standard.

Kwa kauli hizi
1:Nachukia umasikini..

Hivi kweli ni nani hachukii umasikini awe Magufuli, Kikwete, Mkapa, Mbowe wote wanauchukia umasikini hata mimi nauchukia umasikini kwahiyo kauli ile nilikuwa ni kauli dhaifu kabisa kuwashawishi watu wakupigie kura ingawa labda nyuma yake ulikuwa na lengo zuri.

2:CHADEMA ni chama cha wanaharakati:

Kitendo cha kusema CHADEMA ni chama cha uanaharakati ni kuwakatisha tamaa wanachama karibu robo tatu na wafuasi wao waliokuwa wanapigania mabadiliko ya kweli watu kama Lema,Sugu,Mnyika,Lissu unafikiri hii kauli wanaichukuliaje?

3:Uwezi pambana na wafanyabiashara;

Unaeza sema kwa maana nzuri lakini ukajikuta unaaribu maudhui na maana halisi ya unachokimaanisha hapa mi najua hakuna taasisi,watu mtu aliye juu ya sheria kila kitu inabidi kizibitiwe!!

4: Pigeni kura mimi nitazilinda;

Mimi nilisafiri kutoka masomoni nje na kuja nyumbani kumupigia kura kwakujua atazilinda kinyume chake akaja na sababu ya kuibiwa kura najua aliwakatisha tamaa mamilioni ya watanzania.

Ukweli mchungu najua kuna watu watakuja kunishambulia lakini nina uhakika kama CHADEMA wasingempokea Lowassa wangepata vitu zaidi vya ubunge na kingeimarika zaidi.

Kujiondoa kwa Dr slaa:
Dr slaa alitakiwa abaki CHADEMA kwa gharama yeyote kuliko kuondoka
Ni aibu kama Dr slaa asiye na chembe ya ufisadi kuondoka ndani ya chama alafu watu wakaja hapa na kusema hakuna athari? Nimekaa nikajifikiria hivi tulikuwa serious tunataka mabadiliko au tunatania?

Lowassa huyu aloyekataa katiba ya Warioba??
Lowassa huyu huyu tajiri Mwenye kilakitu duniani?

Lowassa huyu huyu ambaye wamekuwa na tuhuma kibao kama walivyo magamba wenzie waliobaki CCM? Lazima kama taifa tufike sehemu tukubali ukweli tuanze upya kwani kwanza upya kuna gharama gani?

Sio lazima Lowassa aondoke CHADEMA la hasha ila asipewe nafasi ya kuwa na nguvu kama wanavyotaka kufanya sasa kama anakifadhiri chama afanye kama mwanachama wa kawaida naamini CHADEMA bado ni chama cha upinzani chenye watu wengi na lakini ila ili kiendelee kuaminika lazima watu wenye makandokando kama Lowassa,Sumaye, na wengine wasipewe nguvu ndani ya chama.

NB;
Mtu ambaye CHADEMA ilimchukua kwa umakini ni Ester Bulaya tu.
Kiukweli tuanze upya tumeshindwa kupata mabadiliko tunayoyataka nina uhakika tukijipanga 2025 tunaweza kuwaangusha magamba lakini sio kwa kuwatumia Lowassa,Sumaye, masha, etc

Angalizo ndani ya UKAWA pia wamulikeni Sumaye, Mbatia, Lipumba kama akirudi na Zitto kama akirudi.

Nawasilisha!
Bablai, unatumalizia bando, aisee yaani umeandika uzi mrefu sana alafu Ni utumbo mtupu. Aghh
 
Mbowe ni adui wa mabadiliko, Slaa was right

Mbowe yupo kimaslahi zaidi ngoja aiue Chadema taratbu
 
Back
Top Bottom