Lowassa: Sina shaka na umaarufu wangu .

Lowassa: Sina shaka na umaarufu wangu .

assadsyria3

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
6,909
Reaction score
4,057
Lowassa: Sina shaka na umaarufu wangu .


Jumanne, Mei 28, 2013 03:41 Na Eliya Mbonea, Monduli
.

MBUNGE wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amesema hana shaka na umaarufu wake Monduli wala Tanzania kwa ujumla. Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana wakati akifungua kampeni za udiwani wa Kata ya Makuyuni huku akikishangaa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kupeleka mgombea wake katika Kata hiyo.
“Eti hawa wanathubutu kujinadi na kujigamba kushinda udiwani Monduli ya Lowassa wakisema watapata kura kwa asilimia 90 jamani haya ni kweli,” alihoji Lowassa na kuongeza:

“Ndugu zangu sina shaka na umaarufu wangu Monduli wala Tanzania.”

Katika mkutano huo, aliwaambia wananchi kwamba anahitaji kuona wakikiadhibu CHADEMA kwa kukipa pigo ambalo hawajawahi kulipata mahali popote nchini.

“Ndugu zangu atakayewapa kura hawa CHADEMA wana wa Makuyuni atakuwa amenichoma kisu mimi, naomba msiwape kura hata moja, naomba muwafundishe adabu,” alisema Lowassa.

Akikishambulia chama hicho kwa kutumia helikopta katika Kata hiyo, alisema siku zote vita vya kiafrika vinapiganwa kwa kutumia askari wa miguu na si helikopita.

Alisema CCM inatumia askari wa miguu kuhakikisha inashinda vita vyake, hivyo haitatishika na helikopita hiyo.

Alikirushia kombora chama hicho kwa kukitaka kisimame hadharani na kujipapanua kama hakihusiki na vurugu

zinazoendelea nchini.

Alisema kama kweli hakihusiki na vurugu zilizopo nchini basi viongozi hao wanapaswa kujihoji ndani ya nafsi zao kama kweli hawahusiki.

“Nawaomba hawa CHADEMA wajihoji ndani ya nafsi zao kama kweli hawahusiki na vurugu hizi, je wanaifanyia nchi yetu mema au mabaya,” alihoji Lowassa.
 
Huyu fisadi na yeye sasa ameanza kuweweseka baada ya kusikia kuna makundi mengine ya urais ndani ya ccm yameanza kujipambannua. Atulie anyolewe
 
Lowassa ni kama kuchi dume aliezeeka meno yote domoni hakuna
 
Tusubiri tuone wananchi wanajua cha kufanya.
 
hivi lowasa bado anaamini ataweza kuwa risi bongo kweli watu wana roho ngumu
 
Umaarufu wa scandal za kifisadi hauna tija kwa taifa!
 
ha ha ha anajikakamu na kutetemeka, hv anaye leta fujo kwa maslai ya taifa na anayeiba mali za wananchi kwa maslai yake binafsi nani ni mwema?
 
Mbona sijaona sera ya chama ikitangazwa?wamefanyiwa nin?na watarajie kufanyiwa nin ndo nilipenda kusikia

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Mzee kajificha weee hatimaye kachomoka pangoni, chezea LEMA WEYEEEEEEEEEEEEEEE. Lazima utoke ulikojificha, sas subiri kichapo kama ARU MASHARIKI
 
Wewe na tembo dentist mlitakiwa muwe kwenye concentration camp. Umaarufu wa wizi?
 
Hii ndio tz . Jamaa kaibaaaaa kafisadiiii. Leo anasimama jukwaani kunadi sera za chama chake, tukisema chama cha mafisadi mnang'aka. LAKINI ARUMERU SI ALIJISIFIA HIVYOHIVYO TENA KWA MUME WA MWANAYE?
 
Kama kuchagua CDM ni kumpiga kisu, mbona yeye aliwapiga kisu wa tanzani kwa mkataba feki wa RIchmond?
 
utachomwa kisu subiri muda si mrefu kama sio katika uchaguzi huu ata katika chaguzi zinazokuja.
 
Lowasa aka Richmond akiwa Rais naukana utaifa natafuta nchi nyingine nikaishi
 
Back
Top Bottom