Cathode Rays
JF-Expert Member
- Nov 3, 2011
- 1,738
- 1,495
Siku zote huwezi kukata tawi la mti uliokalia, Lowassa alipokuwa CCM asingeweza kwa vyovyote kwenda kinyume na matakwa ya chama hata kama moyoni mwake akiona hayafai. Ila kwa sasa kwa vile hayuko huko anaweza kabisa kubadilika na kufanya kile umoja wa UKAWA unakitamani kukifanya. Elewa kwamba hapo hafuati matakwa yake anafuata matakwa ya Umoja huo. Tuondoe wasiwasi kama tumeamua kubadilika tusonge mbele bila kuogopa.
Tanzania mpya inawezekana!
Sidhani kama Lowassa alikuwa muumini wa serikali tatu.
Hebu msikilize hapa anavyopinga serikali tatu!
Ng'wamapalala, I can tell you kuna wengi ndani ya CCM ambao walipigania Serikali mbili kwa sababu ni Msimamo wa chama lakini wenyewe wakiwa waumini wa Serikali 3....
Changamoto kubwa ilikuwa huu ni mwaka wa "maamuzi" na kudefect msimamo wa Chama kungemuweka mwanachama mahali pagumu kudhihirisha msimamo wake
Kama nitakuwa nimemnukuu vema Polepole kwenye moja ya mazugumzo yake, ni kuwa katika hatua za awali Lowassa alikuwa mfuasi mzuri wa Mtazamo wa Serikali tatu
If that is the case, swali kubwa hapa ni nini kilisababisha akapiga U-turn toka kuwa muumini wa Serikali 3 hadi 2??
Usishangae hilo, hata Tibaijuka alisema alipotumuliwa uwaziri kuwa wabunge wasiwe mawaziri. Kuna nguvu nyuma iliyokuwa inawalazimisha kusema yasiyokuwa yao!
watamnyang'anya kadi ya uanachama.
Popularity of a politicians grows as a result of their long standing views and social principles they held high.
Mtu yeyote anaye badilika kimsimamo haraka namna hiyo siyo wa kuaminiwa kabisa Lowassa kwa sasa atasema chochote kuwavutia wafuasi wa UKAWA if anything anaonyesha ni mwanasiasa muongo, asiye na morals na pengine kweli ana agenda binafsi za kulifilisi taifa.
You are very right...Ila kwa muda wa miaka zaidi ya 50 tumewaweka madarakani wanasiasa tulioamini hawabadiliki, tulioamini sio waongo, tulioamini hawalifilisi taifa. Je, Taifa liko kwenye hali gani?
Tunahitaji kubadilisha mfumo na sio wanasiasa.
Popularity of a politicians grows as a result of their long standing views and social principles they held high.
Mtu yeyote anaye badilika kimsimamo haraka namna hiyo siyo wa kuaminiwa kabisa Lowassa kwa sasa atasema chochote kuwavutia wafuasi wa UKAWA if anything anaonyesha ni mwanasiasa muongo, asiye na morals na pengine kweli ana agenda binafsi za kulifilisi taifa.
Vyote vinahitaji mabadiliko. . . .Mfumo na sehemu kubwa ya wanasiasa wanatakiwa watoke kabisa kama kweli lengo ni kwenda mbele. . . . .
wataanzaje?
Mtu anapoamua kubadili mawazo juu ya jambo linalohusiana na msimamo au kanuni fulani ni lazima awe na sababu za msingi za kumfanya kubadili mawazo. Kubadili mawazo kwa sababu ya sababu fulani za msingi ni jambo la kawaida na ni sehemu ya maisha, na hasa katika siasa. Kwa mfano, mtu akiamua kubadili mawazo juu ya suala la Muungano kwa mfano ni lazima ana sababu; kwamba alichokuwa anaamini kilikuwa hakina msingi na sasa ameona mwanga fulani. Lowassa anaweza kweli amebadili mawazo kwa sababu sasa ameona mwanga.
Lakini katika mazingira ya siasa za sasa ni vigumu kuona jinsi gani ameweza kugeuza mawazo baada ya kupewa nafasi ya kugombea isipokuwa amekubali kubeba mawazo ya wale ambao sapoti yake anaihitaji ili kuweza kwenda Ikulu. Kwa sababu hiyo itambidi aibeze CCM, aseme kinyume na yale aliyoyasema akiwa CCM na itabidi ajioneshe kuwa sasa amevaa joho jipya la upinzani. Kama hili ni suala la moyoni au la kisiasa tu hakuna anayejua. Isipokuwa angalau kama ametamka kwa kauli yake basi inabidi tukubali kwa kauli yake hiyo. Ila akishinda au kushindwa ndio tutajua anasimama wapi hasa kwani akishinda halafu akaamua kutokutoa full autonomy na akasimamia suala la Serikali Mbili kama alivyofanya akiwa CCM CDM watamfanya nini?
Mkuu kama kuna kosa basi ni kuamini mwanasiasa huyu wa leo akishika dola atakusikiliza kama afanyavyo leo. . . . . .Gravious mistake!!!Kweli kabisa mkuu..ila kuna msemo unasema "Safari huanza na hatua". Hatua ya kwanza tuondoe mfumo (CCM) baada ya hapo tupambane na wanasiasa katika mfumo mpya.
Tutamhitaji Dr. Slaa kusimamia misingi na Ilani na nidhamu ya utendaji wa wa Chama. Sioni mtu mwingine atakayeweza kusimamia hilo, hakuna kabisa, tunaweza kujikuta tumegeuka babeli.
Hebu niwaulize watu mlio na macho lakini hamuoni, mna masikio lakini hamsikii, which is the the bigger u-turn, kuachana na chama chake cha awali alichokitumikia kwa miaka yote hiyo au kuachana na msimamo wake wa awali kuhusu muundo wa Muungano. Watu wale wale tuliowaambia Lowassa hawezi kuwa juu ya chama na kubadili msimamo wa UKAWA ndio hao hao sasa wanalalama wakidai Lowassa kapiga u-turn kimsimamo. Hivi mlitakaje hasa? Yaani mlitaka ajiunge na UKAWA huku msimamo wake ukibaki ule ule unaopingana na wa UKAWA, kweli akili hizo?
Vivyo hivyo alipokuwa CCM, mara ngapi tulisikia wabunge kutoka CCM wakionywa kutanguliza maslahi ya chama kwa kutetea msimamo wa chama. Mara ngapi watu walioonesha msimamo tofauti na chama waliitwa vikaoni na kukaripiwa kwa kwenda kinyume na chama? Kwa mbali namkumbuka aliyekuwa katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, alipowatahadharisha wabunge wote wa CCM kutetea maslahi ya chama mbele ya taifa. Acheni upuuzi wenu, Lowassa sasa ni mwana UKAWA na atatekeleza wajibu wake kulingana na sera za UKAWA, CCM kwake ni historia.
Sidhani kama Lowassa alikuwa muumini wa serikali tatu.
Hebu msikilize hapa anavyopinga serikali tatu!