figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais Kupitia Chama kikuu cha Upinzani nchin Tanzania CHADEMA/UKAWA 2015, amesema hawezi Kurudi CCM kamwe. "Mimi nitafia Upinzani" amesema Mheshimiwa Lowassa.
Lowassa bado amewasihi wale aliowaacha CCM waende UKAWA ili waunganishe nguvu. Ndugu nzangu wanaoniunga Mkono ambao wapo ndani ya CCM, huu ndio wakati wa kunifuata kwa Uwazi ili tuunganishe nguvu.
Lowassa alishawahi kunukuriwa akiwaambia wanahabari kuwa kasi ya ufanyaji wa siasa itaongezeka kuliko ilivyokuwa awali na kwamba 2015 anaweza akawa “amepoteza pambano lakini siyo vita.” Mapambano yanaendelea tena kwa Siasa za Kisasa kabisa zisizo na matusi, wala Mimi sifanyi siasa za Maji taka.
Kila mmoja ajipange.