Lowassa njoo Tunduru

Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa, baba wa uendeshaji wa harambee, huku kwetu Namasakata Tunduru kuna kanisa la Anglikana mbalo hatuna kanisa, tunasali chini ya mkorosho na tuna waumini wapato 48. Tumeandaa nyimbo na risala za kukusifu. Tuna ngonjera za kuwatukana akina Sitta, Mwakyembe, Nape, Mwandosya, Membe na Makongoro Nyerere.

Tumeandaa pia watu watakaozimia kwa furaha ya kuwakomboa kutokana na kuwapatia nyumba ya ibada na tutudhihirishia umma kwamba wewe si fisadi na kwamba makelele ya ufisadi si tu kwamba ni wivu wa kike, bali pia ni siasa za makundi zenye muelekeo wa urais wa 2015. Karibu baba, karibu Namasakata, Tunduru, tukupokee kishujaa. Utakapokuja uongozane na Serukamba, Beatice Shelukindo, Januari Makamba, Masha, Mahanga, Nchimbi, Guninita na Mgeja, kwa sababu hawa huwa tunawasikia tu kwenye vyombo vya habari. Mshawishi na Kilumbe Ng'enda ili tumfariji baada ya uonevu aliotendewa. Karibu Namasakata shujaa wetu!

Serikali ni moja tu. Unataka kumtukana nani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom