Kwa hiyo Lowasa anaamini Babu seya kaonewa? au kaona ni mtu muhimu sana hadi aachiwe? Kila siku tunawangisha vichwa kuangalia namna gani tutawalinda watoto wetu dhidi ya ukeketaji, ubakaji, mimba za utotoni, ukosefu wa elimu na ajira, halafu mshenzi mmoja anasema atamwachia huru mbakaji, kweli?
Watanzania tumekuwa wayahudi mara hii? leo hii wayahudi wanajutia kumsulubu yesu na kumwachia balaba, sie tunashangilia mtu anayetaka kumwachia mbakaji, kweli? Nimesikitika sana siko tayari kumuunga mkono Lowasa kwa namna yeyote ile nasimama peke yangu.