Lowassa: Nimeshawishika, Nitagombea urais...!

tusipokuwa makini huyu masai ataingia ikulu huku tunaona.
 
Sara yangu ya Leo. E Mungu tuondolee kikombe hiki sisi Waja wako Watanzania. Hii timu itatuacha watupu.
 
jamani hebu tuweni wakweli,hivi katika CCM ya sasa kuna mtu anaweza kugombea ubunge ua urais bila kumwaga pesa?? sema wanatofautiana mbinu za kuhonga/kutoa rushwa ila wote ndani ya CCM wanatumia hela nyingi sana kusaka vyeo,iwe ubunge au urais na hata udiwani
 
Mzee mamvi na Profesa tezi tunajua hamkukutana vichororoni, Mungu sikia kilio chetu tumesulubika kwa miaka 10, pls God tuokoe na hili jinamizi lilojaa mamvi uso mzima ili hiyo miaka mingne 10 tupumue baada ya kusota kwa muongo mzma.
 
Baba wa taifa hayati Nyerere alishasema Lowasa hafai kuwa raisi huu wosia wa umuhimu sana kwa vijana wote.
 
tusipokuwa makini huyu masai ataingia ikulu huku tunaona.

Hata mie nimeanza kuogopa mkuu kuna watz wengi wanaoendekeza shibe ya siku 1 inavoonekana watatuangusha hili jitu na mamvi yake hela lilizonazo zinalibeba aiseee!
 
Baba wa taifa hayati Nyerere alishasema Lowasa hafai kuwa raisi huu wosia wa umuhimu sana kwa vijana wote.


Hila anazotumia Lowassa kuingia Ikulu ni za kutilia mashaka na wote wanaoitakia mema nchi yetu wanatakiwa kuwa makini na mbinu hizo
 
CCM imeingia mtegoni. Bila EL naiona kama vipande vipande. Wachague kusuka au kunyoa. Hapa panahitajika POTELEA MBALI LIWALO NA LIWE kumuacha huyu ndugu.
 
Huyu bwana anatupa mashaka maana anatumia nguvi nyingi sana kutaka kuingia Ikulu.

Ninawashangaa sana wanaomuunga mkono huyu bwana bila kujiuliza ana nia gani hasa na hii nchi.

Ukitaka kitu inabid utumie uwezo na assets zako kukipata.
Asingetumia hiyo nguvu, watu wangesema aah huyu hana nguvu hafiki popote.
Tunamsapoti coz there is no other better choice.
 
CCM imeingia mtegoni. Bila EL naiona kama vipande vipande. Wachague kusuka au kunyoa. Hapa panahitajika POTELEA MBALI LIWALO NA LIWE kumuacha huyu ndugu.

Muda wa kumuacha alikuwa zamani, too late now.
 
Baba wa taifa?Kwa yeye ndio nani?
Aende zake huko.

Mtu anayesaka madaraka kwa kutumia pesa hafai kupewa uongozi anatakiwa kuogopwa kama Ebola.Baba wa taifa wewe na upeo wako mdogo huwezi kumjua .
 
WanaJF,

Ni vizuri kuwa OBJECTIVE kama unataka kutoa hukumu kwa mtu. Kila mwanadamu ana mapungufu yake lakini kwenye suala la uongozi lazima tuangalie uwezo wa mtu hasa katika kusimamia TARATIBU, SHERIA na KANUNI. Lakini lililo kuu kabisa ni kuwa na mtu mwenye MAAMUZI au anayeweza kufanya MAAMUZI lakini siyo maamuzi magumu. Maamuzi magumu ni kushindwa kufikiri na kuwa na strategic thinking. Maamuzi magumu ni pale ambapo hakuna mbadala wa jambo fulani. Kwa mfano, hakukuwa na jinsi yoyote ambayo Mwl Nyerere angeacha kuamuru Jeshi la Tz kumpiga Idd Amini Dada.

Tutafakari kwa kina ila kama kuna watu ambao wanafikiri Lowassa hatakuwa Rais basi ni vizuri wakamrudia Mungu awaongoze sawa sawa maana mzee huyu kuliko aache kugombea na possibly kuwa Rais maisha yake yatakuwa mafupi sana kwa sababu amedhamiri. Binafsi naona ana sifa za kuwa Rais haya mengine ni vionjo tu vya kibinadamu ambavyo wewe na mimi pia tunavyo.
 
Sara yangu ya Leo. E Mungu tuondolee kikombe hiki sisi Waja wako Watanzania. Hii timu itatuacha watupu.

Umenena vyema mkuu watanzania siyo wajinga wa kusahau kama Lowasa anavyotegemea raisi ajaye atatoka nje ya ccm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…