sbikore
JF-Expert Member
- Feb 13, 2015
- 535
- 191
Wadau wangu amani na iwe kwenu,
Siasa haina uadui, bali siasa inaweza kukujenga au kukubomoa kwa kupitia hasimu wako, na hasa unaweza kujifun mbinu chafu na nzuri kwa ajili ya kumdhoofisha hasimu wako.
Hata mm ni CCM pure, ila sina sababu ya kutompongeza mh. sana mzee lowassa.
Na hii haimaanishi kwamba atanihamisha CCM ili nikamuunge mkono hapana ila hapa kanifurahisha na zaidi amenijenga kisiasa na kwa kupitia hili niwashauri wanasiasa wengine wa vyama vyote kujifunza mbinu za upambanaji katika siasa.
Lowassa ana madhara makubwa sana dhidi ya chama pinzani kama hatodhibiwa, na nyote mtakubali kwamba bila uwepo wake CHADEMA kwa sasa isingekuwa dili. Ukweli ni kwamba hofu yote ya chama chetu katika siasa ni kwa sababu ya huyu nguli.
Tunashudia matamko mengi ya serikali na hata vyombo vya usalama. Yote haya hayamlengi Mbowe wa Lissu, hapa mlengwa ni Lowassa.
Kuhamia kwake CHADEMA kumekifanya chama kuwa kipya kabisa ukiachilia awali ambapo kina Mbowe waliruhusiwa kuzunguka nchi nzima usiku na mchana na wasiwe na madhara yoyote kwa chama hili kongwe.
Kubwa zaidi hapa ni mbinu aliyoitumia nguli huyu kujijenga upya japo sitarajii akaongoza nchi hii, maana tayari Rais Magufuli alishakuwa agenda ya watanzaia wote na hasa wanyonge. Nyote mtakumbuka chadema walimtumia mzee lowasa kama ngazi ya kujijenga kisiasa.
Simaanishi kwamba kweli ni fisadi au siyo maana ushahidi mpaka jana haujadhihirisha. Lakini wanasiasa wa vyama vyote na hasa CHADEMA wakifanikiwa sana kujijenga kwa kupitia jina la nguli huyu.
Kwa kiwango walichomchafua tusingetaraji leo wamtumie tena kama dira ya chama. Kwa maana kwamba kwa maneno yao waliyoyatamka dhidi ya Lowassa, leo wanaamua kuwa chini ya mamlaka ya fisadi kama walivyomwita awali.
Je, hapa ni nani fisadi kati ya CHADEMA na Lowassa?
Nguli huyu kwa kutumia uwezo wake mkubwa wa ushawishi na amefanikiwa kuwalaghai CHADEMA kumsafisha kwa gharama yoyote na kuwasahaulisha kwamba wao ndio walitumika pia kumnadi vibaya.
CHADEMA wamekubali kutumika kama punda, na hatutashangaa sana hata ikatokea leo wakamuhitaji zaidi mzee Kikwete kuliko mzee Magufuli wakati wao haohao walimwita Kikwete kwamba ni kiongozi dhaifu.
Hivi hawa ndugu zetu ni usahaulifu unawasumbua au ni kwa sababu wanafikiria zaidi kwa kutumia matumbo kuliko vichwa? Ujio wa Mh. Lowassa CHADEMA licha ya wao kuuona wenyenye mafanikio, lakini umewazalia madhara makubwa sana.
Kwanza amefanikiwa kuwachafua sana na yeye kujijenga sana, kiasi kwamba ikitokeo leo huyu mzee akajiengua na CHADEMA, chama hiki kitakosa ladha na mwelekeo kwa maisha yake yote.
Maana hakuna tena mtanzania mwenye timamu ataweka akili kwenye chama hiki. Na hata ukiangalia kwa sasa watu wengi ndani ya CHADEMA mvuto wao ni Lowassa ni si vinginevyo.
Hivyo wanapaswa kumlinda kwa gharama yoyote ili kuendelea kunusuru uhai wa chama chao. Amekipasua chama kwa kiasi kikubwa na kupelekea kuwatawanya viongozi waliokuwa na mvuto mkubwa ndani ya CHADEMA Mf. Dr. Slaa, Kabwe na wengine wengi.
Amepelekea kutoaminiwa kwa kiongozi mwingine yeyote ndani ya chama isipokuwa yeye tu na Mbowe kwa mbaali. Amefanikiwa kuivunja ukawa na kuwaacha wanalumbana kila uchao na kumegeka kwa nguvu nyingine kumfuata aliko.
NCCR imekosa mwelekeo, na usishangae M/kiti hivi karibuni akatangazwa kuwa mwanachama halali wa CHADEMA, CUF, NLD hoi kabisa na matokeo sasa viongozi wakubwa ndani ya vyama hivyo wameanza kujiengua na kumfuata nguli huyu.
Zaidi ameibeba dhamana ya CHADEMA kwa asilimia zote, na ikitoke hayupo hata kesho ni dhahiri CHADEMA kutabaki giza totoro kwa kukosa mwelekeo na kuambulia dhihaka na aibu kubwa kwa kukosa misimamo.
Kwa kufaulu yote hayo juu, sasa mzee Lowassa ataenda kung'atuka katika siasa akibaki na heshima zake zote kuliko vile alivyochafuliwa na hawa wabeba mzigo, angekaa kimya angeng'atuka kwa aibu sana.
Hongera sana mzee Lowassa kwa umahiri wako wa siasa, hongera sana kwa kutupunguzia nguvu ya upinzani (utakapong'atuka).
CCM inaenda kuongoza zaidi ya miaka hamsini ijayo.