Hakuna jipya! Alipoongea na watz kupitia waandishi wa habali wilayani Monduli, alisema wazi kwamba hataki kuzungumzia swala la Richmond na muda wa kuzungumzia kugombea urais bado haujafika. Sasa utazungumzia kuvua gamba na Lowasa ukaacha kuzungumzia Richmond!?
Hao star tv watakuwa wamepewa mashari makali kuhusu maswali ya kuuliza na hata simu zitakuwa screened kabla hazijaenda hewani kama wakati ule wa JK. Ful usanii.
Utasikia mtu anasema "napiga simu kutoka kijiji cha mota, tarafa ya kibakwe, wilaya ya Mpwapwa, mkoani dodoma" kumbe ni katibu wake na yupo nyumba ya studio na maelezo/maswali ya kupangwa! Si ajabu kusikia kwamba wanampongeza sana kwa ujasiri!