Lowassa ndani ya Kigoma

Lowassa ndani ya Kigoma

Supervisor

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2010
Posts
559
Reaction score
208
Waziri Mkuu Mstaafu EL amewasili Mkoani Kigoma hv punde. Amealikwa kuja kuendesha Harambee kanisa la PENTEKOSTE ..............
Mengi Tutawajuza.

UPDATE:

Lowassa achangishia kanisa mamilioni

Zaidi ya Shilingi milioni 125 zilipatikana katika harambee ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Kidingo mkoani Kigoma iliyoendesha na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.

Lowassa na marafiki zake walichangia Sh. nilioni 65 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo iliyoko Kata ya Mwandiga wilayani Kigoma.

Uchangiaji huo ulifanyika jana katika Kanisa la FPCT na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wabunge wa mkoa wa Kigoma na madiwani.

Akizungumza katika hafla hiyo, Lowassa alisema watu wengi wanapenda kuitumia nguvu ya maaadamano badala la nguvu ya kuleta maendeleo katioa ujenzi wa shule.

Alisema kuna vijana wengi waliokosa ajira, ambao alisema ni bomu linalosubiri kulipuka. Alisema vijana wengi wanamali za shule na vyuo, lakini wanakosa ajira.

Aliiomba serikali na wadau mbalimbali nchini kukaa chini kupanga mikakati ya namna ya kuwasidia wapate ajira.

Aidha, aliwataka watu waliomali za masomo wasisubiri ajira za serikali badala yake wajiunge katika vyuo vya ufundi stadi ili wajiajiri.

CHANZO: NIPASHE (Jan 10, 2012)
 
...ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu linalosubiriwa kulipuka....
 
Lowasa anampenda sana mungu na sasa ameamua kufanya kazi ya kulieneza neno kwa kuwawekea waumini miundombinu mbadala. Kazi kwenu waumini mshindwe wenyewe kuhudhuria ibada. Lowasa ubarikiwe sana
 
Siyo waziri mkuu staafu,ni waziri mkuu alijiuzulu!Huyu mzee kahamia makanisan sa hivi!kampeni zake zimekuwa makanisani!kwanini asialikwe mwingine kuchangisha?yeye ni kama nani!?

Huo ujumbe tutawafikishia wanaomwalika. Si tatizo lake.
 
EL viva sana kwa michango unayotoa kusaidia jamii na hakika Mungu yuko pamoja nawe. Kuhusu urais 2015 we are together with you, the hard working and creative man
 
Sema waziri mkuu aliejiuzuru kwa kashfa ya Richmond sio waziri mkuu mstaafu,hana lolote na ule ugonjwa cjui itakuaje kwake
 
Mbingu igeuke huyo Mafia atapita ule mlango wa IKULU ya Tanzania mwambie ashinde makanisani lakini sisi wananchi sio Mazezeta
 
I have always been positive of this man.

Lowassa tukisema ukweli is very visionary, sifa ya kiongozi ni kuwacna maono, anayependa umoja, mwenye ujasiri katika kutoa maamuzi sahihi kwa wakati anayewajibika, mwadilifu, msikivu na mwenye majibu katika kuwaongoza watanzania, Lowassa kwa CCM, anakijua chama chake na historia yake,ndo maana kwa watu wasioelewa mambo wanalazimisha eti ajivue gamba kwa kuondoka sababu eti ametajwa tajwa Richmond, loooh.

Unajua kwa mwanasiasa yeyote makini lazima ujiulize unapotka kufukuza mtu ambaye anasupport kubwa kiasi hiki,na watu tumeona nini amelifanyia hili taifa unakua haueleweki. Jamani, mimi sijawahi kupewa hata kumi moja na huyu Mzee, tukiwaambia watu kuwa huyu jama hata kama mnasema ni tajiri, Lakini anazo sifa zisizo na mashaka katika kuongoza hili taifa
 
Kosa lipo wapi kualikwa kwenye fundraising... Ni kiongozi wa kitaifa, stateman.
 
EL amelifanyia nini taifa zaidi ya kuiba fedha za tz na kusimamisha wakurugenzi majukwaani?
 
Waziri Mkuu Mstaafu EL amewasili Mkoani Kigoma hv punde. Amealikwa kuja kuendesha Harambee kanisa la PENTEKOSTE ..............
Mengi Tutawajuza.

Hapo kwenye bold blue, huyo fisadi alistaafu lini na wapi?
 
Sasa ni wazi hatuna makanisa,ni takataka tu.
Waziri Mkuu Mstaafu EL amewasili Mkoani Kigoma hv punde. Amealikwa kuja kuendesha Harambee kanisa la PENTEKOSTE ..............
Mengi Tutawajuza.
 
Back
Top Bottom