Lowassa: Nataka kuwa Tajiri zaidi ya hapa!

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,312
Wakati sisi wananchi kigezo cha uongozi ni Uadilifu, Kwa Lowassa kigezo cha uongozi ni utajiri tena mkubwa zaidi.

=================================

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amesema anachukizwa na viongozi wenzake wanaoshabikia umasikini kuwa moja ya kigezo cha uongozi, akisema binafsi anatamani zaidi Mungu amwongezee utajiri.

Katika mahojiano maalumu aliyofanya wiki hii na Raia Mwema, nyumani kwake, Area C mjini Dodoma, aliweka bayana pia kwamba anavutiwa zaidi na wanasiasa wawili, aliowataja kuwa ni Mwalimu Julius Nyerere na Kwame Nkrumah wa Ghana.

"Hapa nilipo, natamani Mungu anipe uwezo wa kifedha zaidi ya nilionao sasa kwani umasikini ni mbaya na si kitu ambacho mtu anapaswa kukiringia.

"Mimi nachukia umasikini na ndiyo maana nataka uongozi ili nami niweze kuwasaidia Watanzania waweze kujikwamua na hali hii. Nawataka Watanzania wenzangu kuondokana na dhana ya kuwachukia matajiri."

"Nasikia kuna baadhi ya viongozi wenzangu ambao wanajisifu kwa umasikini. Kwangu mimi, umasikini si sifa nzuri kwa kiongozi. Mimi si tajiri sana," alisema Lowassa katika mahojiano hayo yaliyochapishwa katika kurasa za katikati za gazeti hili.

Lowassa ni nani?

Edward Lowassa alizaliwa Agosti 26, mwaka 1953 na aliteuliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Waziri Mkuu mwishoni mwa mwaka 2005. Alibaki katika madaraka hayo kwa miaka mitatu tu, kuanzia mwaka 2005 hadi 2008, chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.

Lowassa alisoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutunukiwa Shahada ya Sanaa na kisha alitunukiwa Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Bath, nchini Uingereza.
Alisoma shule ya sekondari katika Sekondari ya Ilboru na kisha Sekondari ya Milambo mkoani Tabora, mwaka 1977.

Amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi, katika ngwe yake ya pili kama Rais wa Awamu ya Pili.

Aliwahi kujaribu bila mafanikio kuwania kuteuliwa kusaka urais kwa tiketi ya CCM mwaka 1995 na jina lake kuenguliwa katika hatua za awali, chini ya usimamizi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Inadaiwa kwamba Nyerere ni kati ya watu waliokuwa wakiamini, wakati huo wa mchakato wa kusaka mgombea urais wa CCM, kwamba Lowassa hakuwa na sifa jambo ambalo analikanusha katika mahojiano hayo.

Mwaka 2000, wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa, Lowassa aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo. Mwaka 2005 alitangaza kutoingiza jina lake katika kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM na badala yake, alimuunga mkono Rais wa sasa, Jakaya Kikwete.

Lowassa alijiuzulu uwaziri mkuu Februari 7, mwaka 2008 baada ya kushauriwa na iliyokuwa Kamati Teule ya Bunge kupima kama anastahili kuendelea na wadhifa huo, baada ya kubainika uhusika wake wa kuingia mchakato wa utoaji zabuni kwa kampuni ya kufua umeme ya Richmond. Anasema katika mahojiano kwamba sakata hilo la Richmond ni kati ya fitina kubwa alizofanyiwa.

Amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), kuanzia mwaka 1989 hadi 1990 na mwaka 1990 hadi 1993 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, anayeshughulikia masuala ya Mahakama na Bunge. Mwaka 1993 hadi 1995 aliteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na mwaka 1997 hadi 200 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mazingira.

Chanzo: Raiamwema
 
1993-1995 ndipo viwanja vya masaki na maeneo ya wazi vilivyopigwa dili za kufa mtu
 
Hao ccm wanaowadanganya umaskini ni sifa wao ni matajiri, nenda chato ukaone Magufuli alivyo tajiri ana bonge la ranchi anafuga mang`ombe na manguruwe kibao. Wanawadanganya umaskini ni sifa halafu wao wanatibiwa India, endeleeni na ujinga wenu wa kuona umaskini. Sisi tuliojitambua tunafuata nyayo za Lowassa kwa kupambana na umaskini kwa vitendo ili tuwe matajiri
 
1993-1995 ndipo viwanja vya masaki na maeneo ya wazi vilivyopigwa dili za kufa mtu

Huo utajiri fake alipjipatia kwa kujichukulia mali zetu unaanza kuyoyoma soon na tayari tumeanza kumnyonyoa manyoya yake taratibu ..atajuta kutuibia
 
Rais msaka utajiri badala ya kuboresha maisha ya wananchi.!
Nani anayependa umaskini!!? anasaka utajiri wa watanzania. mbona hujaongelea hapo aliposema anataka kuongoza watanzania waondokane na umaskini? wawe matajiri. hata Mungu muumba ni tajiri, na anapenda waja wake wawe matajiri. au utajiri kwako una maana gani? tuanzie hapo.
 
Wakati sisi wananchi kigezo cha uongozi ni Uadilifu, Kwa Lowassa kigezo cha uongozi ni utajiri tena mkubwa zaidi.

=================================

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amesema anachukizwa na viongozi wenzake wanaoshabikia umasikini kuwa moja ya kigezo cha uongozi, akisema binafsi anatamani zaidi Mungu amwongezee utajiri.

Katika mahojiano maalumu aliyofanya wiki hii na Raia Mwema, nyumani kwake, Area C mjini Dodoma, aliweka bayana pia kwamba anavutiwa zaidi na wanasiasa wawili, aliowataja kuwa ni Mwalimu Julius Nyerere na Kwame Nkrumah wa Ghana.

“Hapa nilipo, natamani Mungu anipe uwezo wa kifedha zaidi ya nilionao sasa kwani umasikini ni mbaya na si kitu ambacho mtu anapaswa kukiringia.

“Mimi nachukia umasikini na ndiyo maana nataka uongozi ili nami niweze kuwasaidia Watanzania waweze kujikwamua na hali hii. Nawataka Watanzania wenzangu kuondokana na dhana ya kuwachukia matajiri."

“Nasikia kuna baadhi ya viongozi wenzangu ambao wanajisifu kwa umasikini. Kwangu mimi, umasikini si sifa nzuri kwa kiongozi. Mimi si tajiri sana,” alisema Lowassa katika mahojiano hayo yaliyochapishwa katika kurasa za katikati za gazeti hili.

Lowassa ni nani?

Edward Lowassa alizaliwa Agosti 26, mwaka 1953 na aliteuliwa na hatimaye kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Waziri Mkuu mwishoni mwa mwaka 2005. Alibaki katika madaraka hayo kwa miaka mitatu tu, kuanzia mwaka 2005 hadi 2008, chini ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.

Lowassa alisoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutunukiwa Shahada ya Sanaa na kisha alitunukiwa Shahada ya Uzamili katika Masuala ya Maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Bath, nchini Uingereza.
Alisoma shule ya sekondari katika Sekondari ya Ilboru na kisha Sekondari ya Milambo mkoani Tabora, mwaka 1977.

Amewahi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi, katika ngwe yake ya pili kama Rais wa Awamu ya Pili.

Aliwahi kujaribu bila mafanikio kuwania kuteuliwa kusaka urais kwa tiketi ya CCM mwaka 1995 na jina lake kuenguliwa katika hatua za awali, chini ya usimamizi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Inadaiwa kwamba Nyerere ni kati ya watu waliokuwa wakiamini, wakati huo wa mchakato wa kusaka mgombea urais wa CCM, kwamba Lowassa hakuwa na sifa jambo ambalo analikanusha katika mahojiano hayo.

Mwaka 2000, wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa, Lowassa aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo. Mwaka 2005 alitangaza kutoingiza jina lake katika kuwania kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM na badala yake, alimuunga mkono Rais wa sasa, Jakaya Kikwete.

Lowassa alijiuzulu uwaziri mkuu Februari 7, mwaka 2008 baada ya kushauriwa na iliyokuwa Kamati Teule ya Bunge kupima kama anastahili kuendelea na wadhifa huo, baada ya kubainika uhusika wake wa kuingia mchakato wa utoaji zabuni kwa kampuni ya kufua umeme ya Richmond. Anasema katika mahojiano kwamba sakata hilo la Richmond ni kati ya fitina kubwa alizofanyiwa.

Amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), kuanzia mwaka 1989 hadi 1990 na mwaka 1990 hadi 1993 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, anayeshughulikia masuala ya Mahakama na Bunge. Mwaka 1993 hadi 1995 aliteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na mwaka 1997 hadi 200 aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mazingira.

Chanzo: Raiamwema

Hata Marekani Kigezo cha Kwanza Kuogombea Urais Uwe Tajiri.
 
Hivi JF sasa hivi kuna jini linalokula comment zetu badala ya damu? uzi nilicomment 2 comments sizioni, itabidi tutawaachie wafuasi wa Padre mzinzi na maccm sasa hili jukwaa.
 
Back
Top Bottom