Lowassa na wamaasai: anataka kurudisha ukabila katika jamii? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa na wamaasai: anataka kurudisha ukabila katika jamii?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by masopakyindi, Sep 3, 2012.

 1. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,495
  Likes Received: 1,834
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Nimefuatilia matamshi ya kiongozi huyu wa CCM aliyelazimika juiuzulu Uwaziri Mkuu, na sijapendezwa na matamshi yake yanayoendelea kusikika katika vyombo vya habari, hata leo.

  Mwalimu alifanya kazi kubwa kuondoa dhana ya kufikiri"kikabila" ili waTanzania tuwe na umoja.
  Hivyo basi kumsikia kiongozi aliyewahi kushika wadhifa wa pili wa juu kabisa katika Taifa letu akipigia debe kabila lake -kiitikadi na kimkakati, basi nafikiri there is something seriously wrong hapa.

  Kwa siku kadhaa sasa Lowassa amekuwa akipigia debe wazi wazi kabila lake(wengine wanasema si lake) la kimasai ili waingizwe katika katiba ya JMT.

  Hii ni hatari.

  Wachagga nao wakitaka waingizwe kwenye katiba, Wahaya je? na Wanyakyusa au hata Wagogo itabidi lipigwe debe ili kila kabila litambuliwe kikatiba.

  Gazeti la Mwananchi la leo linasema Lowassa anataka kuongoza ujumbe wa wamasaai kumwona Rais JK!!
  Huo nafikiri hautakuwa ujumbe wa mwisho maana kutakuwa na ujumbe wa Wachagga, wa Wasandawe na Wadigo kumwona Rais kwa mustakabali wao!!

  Hatujasahau hata kidogo spidi aliyotumia Lowassa kuwaweka "wa kwao" katika sehemu nyingi na nyeti alipokuwa Waziri Mkuu.
  Utetezi wa Ole Naiko wa TIC ulijieleza katika hili wakati Lowassa akijiuzulu uwaziri Mkuu.


  Mlolongo huu wa mawazo ndiyo hata Mwalimu aliwahi kusema mtu kafilisika kisiasa, mtu huyo hana political base, anatafuta unyasi ili apate uhalali wa kisiasa.

  Mbaya zaidi ni matokeo yake katika siasa za jamii ya kiTanzania.

  Lowassa I did not think that you stoop so low!!
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 12,965
  Likes Received: 889
  Trophy Points: 280
  Huyo ndio Lowasa, Rais mtarajiwa wa Tanzania. Huyu bwana anaamini yeye ndio Musa wa kutuvusha bahari ya shamu ingawa kila dalili zinaonyesha mambo hayako hivyo.
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 12,965
  Likes Received: 889
  Trophy Points: 280
  Anajua vizuri ukubwa wa kuingiza hoja ya kabila fulani specific kwenye katiba mpya? I doubt!
   
 4. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,539
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Ah!mwacheni tu ninampenda ni kwamba haangaiki na viongozi wa chadema bize na harakati zake kimpango sio mpuuzi sita na siasa za kinafiki........
   
 5. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lowasa ni kiongoz wa kimila wa wamasai hvyo kukutana ni utaratbu waliojpangia na wamasai ndio kabila apa tanzania lenye mila zao za kipekeee na hoja kubwa alikuwa anawahamasisha wamasai kushrki ktk mchakato wa katba mpya ili na wafugaji watambuliwe cz katba ya sasa inatambua wakulma na wafanyakazi,,,,jamani siasa za kuelekea 2015 zisitumike kupotosha watanzania rais ajaye ambaye Mungu amepanga awe rais ni lazma awe
   
 6. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  lowasa yupobze na wananchi wake na apigi blablah za siasa za maji taka kama wanaokashfu viongozi wa vyama vngne...huyu ni mzeewa mikakat pia atishiwi nyau na ni mtendeji
   
 7. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,495
  Likes Received: 1,834
  Trophy Points: 280
  Mkuu toa maoni yenye kwenda shule kidogo.
  Kwa hiyo Wamasaai wakitambuliwa kikatiba na wengine kwa nini waitambiliwe kwa makabila yao?

  Ni ufinyu wa mawazo kifikiri watu wengine au makabila mengine hawana mila zao ambazo zinaweza kutambulika kisheria.
   
 8. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,107
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  usimtumie mungu kuleta kampeni kuwa makini kijna
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,090
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Sijaelewa Lowassa anaamisha nini kusema (kama ni kweli amesema hivyo) kabila ya wamasai liingizwe kwenye katiba? Katiba ni ya watanzania, na wote (watanzania) wanaingizwa kwenye katiba. Wamasai sio watanzania?

  Kwa sasa tuna matatizo ya udini na ukanda, na haya yote yaliletwa na wanamtandao Lowassa akiwa ni mmoja wa vinara wa mtandao. Sasa hivi wamesambaratika lakina kila mmoja anaendeleza mbinu zile zile za kugawa watu. Na ndio maana cabinet ya kwanza 2006 ilikuwa kubwa sana maana kila kona walikuwa na 'mwakailishi'. Ni mbinu za Kenya na wote tunajua jinsi ukabila unavyoitesa Kenya.
   
 10. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,495
  Likes Received: 1,834
  Trophy Points: 280
  Mkuu wameisambaratisha CCM kwa tamaa yao ya madaraka na sasa wanataka kuisambaratisha nchi kwa tamaa hiyo hiyo
   
 11. N

  Nali JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2012
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 765
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 60
  Katika hili naamini kabisa wewe ndio una ukabila tena mbaya sana!Lowassa hajawai himiza wamasai kuingizwa kwenye katiba maana jambo kama hilo haliwezekani kabisa!! Hakuna katiba yoyote duniani inayozungumzia matakwa ya kabila fulani! Kitu kama hicho hakiwezi kutokea Tz yenye makabila zaidi ya 135!Alichofanya Lowassa, wanaharakati na wadau wengine ni kuhakikisha Wafugaji nao matakwa yao yaingizwe kwenye katiba maana Katiba hii ya sasa haijawazungumzia hata kidogo. Labda hilo ndo unaingiza mambo ya ukabila hapa! Kama hilo ndo limekugusa basi utabaki na sumu yako mbaya maana hilo la "Wafugaji" limeelezwa na kusisitizwa sana na kwa bahati nzuri hata wajumbe wa tume ya katiba wameliona hilo kuwa ni hoja nzito kwa wafugaji!!Acha ukabila, wewe piga siasa zako za umakundi na siasa za maji taka!!
   
Loading...