Lowassa na UKAWA wamesahau kuwa SIASA NI SAYANSI

Sep 5, 2015
80
73
Kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi watanzania wenye sifa za kupiga kura na waliojiandikisha ni milioni 23.7 katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25. Huku vyama vilivyosimamisha wagombea katika nafasi ya urais ni nane. Lakini mchuano upo baina ya Chama Tawala CCM na chama kikuu cha upinzani nchini Chadema. CCM inawakilishwa na Dkt. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI ilihali Chadema inawakilishwa na Edward Ngoyai Lowassa wakipewa upambe toka vyama vya CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD.



Wataalamu wa sayansi ya siasa,wachambuzi na wanasiasa nguli wameandika sana juu ya mambo mbalimbali yanayoweza kukipa chama au mgombea ushindi kwenye kinyang'anyiro chochote cha urais mahali popote. Kutokana na Machapisho yao yaliyotokana na tafiti pamoja na uzoefu wao katika ulingo wa siasa wanasema yapo mambo manne yanayochangia ushindi; Utambulisho na Nguvu ya chama, Kuwepo madarakani, Ufahamu wa wapiga kura na historia ya wapiga kura.



Naomba kuanza na Utambulisho na Nguvu ya chama........
Kwa mujibu wa "Club effect" ni kuwa katika uchaguzi wa rais 90% ya wanachama huwa wanakipigia kuwa chama chao na 10% husaliti. Kwa mujibu wa maelezo haya 90% ya wanachama 8,400,000 wa CCM ni 7,600,000. Sasa ili kushinda uchaguzi kwenye nchi yetu mwaka huu 2015 lazima mgombea apate zaidi ya kura milioni 12;hivyo CCM watahitaji kura milioni 5 tu kutangazwa washindi. Namna chama kinajitambulisha kwa wapiga kura kwa kumtambulisha mgombea wake kunachangia 5% ya wapiga kura wote ni 1,185,000.



Eneo la pili kuwepo madarakani kwa chama au mgombea husika "Incumbent performance" ambapo kunachangia 15-30% wapiga kura wote. Wataalamu wanasema kama serikali ya chama husika haikufanya vyema basi watapata chini ya 30% ya wapiga kura wote na kama watakuwa walifanya vizuri watapata 30% ya wapiga kura wote. Ni ukweli kuwa CCM yapo maeneo waliyofanya vizuri na yapo ambayo hawakufanya vizuri na mgombea vivyo hivyo kwa maana nyingine 15% ya wapiga kura ni 3,555,000.



Pia wanasema uelewa/ufahamu wa wapiga kura unachangia 5% ya wapiga kura wote "Dunning krugger effect". Yaani watakaochagua baada ya kuwasikiliza na kuchambua sera na kisha kutoa kura yake kwa kujiridhisha mgombea husika amemridhisha. Maana yake ni kura 1,185,000.



Ndiyo maana kwa hesabu hizo CCM wanajipa uhakika halafu wengine wanasema CCM wanakiuka demokrasia kumbe wamesahau siasa ni sayansi. Mpaka sasa CCM katika kila Mkoa,kila wilaya,kila jimbo na baadhi ya kata katika jimbo husika mgombea wao wa urais amefanya mikutano ya kampeni ambayo inakadiriwa mpaka sasa amefanya mikutano zaidi ya 115 na isiyo rasmi ya kusimamishwa kwenye vijiji na barabarani 436. Ambapo mikutano 49 imerushwa LIVE na Star TV hivyo kuwafikia watanzania karibu wote.

CCM ikiwa imefanikiwa pia kuungwa mkono na wasanii wote maarufu kwenye maigizo na muziki hivyo kuteka kura nyingi sana za rika zote vijana,wanawake na wazee.
Kete nyingine ni utamaduni wake wa kampeni za ustaarabu zisizo na fujo wala vurugu ambazo zimewavutia wengi kama inavyooneka hapa. Hivyo CCM kushinda kwa zaidi ya 62% ukikataa utakuwa unaendeshwa kwa hisia na mihemko na si uhalisia.Utamaduni wa CCM kuamini ahadi ni deni kwa kutekeleza ahadi walizozitoa kwa watanzania kupitia ilani zao na ahadi binafsi za wagombea urais ndio siri ya kuaminiwa zaidi.....Jioneee!!!!!!!!!!!

ITIGI-SINGIDA

magufuli itigi singida.jpg

DODOMA
magufuli dom.jpg

DAR

MAG DAR.JPG

KIGOMA2.jpg

MOROGORO
nyomiii.jpg

TANGA

View attachment 293809

ISIMANI IRINGA

DODOMA1.jpg


NB: Mpiga kura wajibu wake ni kupiga kura, ulinzi wa kura ni jukumu la wakala wa kila chama. Nakusihi Ukishapiga kura rejea nyumbani kusubiri matokeo usiwe chanzo cha vurugu.
 
Umeongea sana na mapicha yako ila nimeambulia pumba tupu. Hizo picha wagombea wanasombwa kwa malori na mafuso na mabasi ili picha ikipigwa ionekane wako wengi. Pia takwimu zako nnazipingaa sana, unadhani mwaka huu ni kama 2010? Una takwimu za waliohama CCM kuja upinzani? Una takwimu za waliobaki CCM kimkakati, japo wanavaa nguo za kijani lakini watampigia Lowasa? Kam huna hakika usijisemee hovyo hovyo kama vile umekula maharage ya Mbeya.

Unajua kuwa Lowasa amewateka vijana ambao ni kundi kubwa sana? Endelea kubaki na takwimu zenu feki za Twaweza sijui na nani mwingine tena vile. Umekuja kubwabwaja na takwimu zako ili mkija kuchakachua muwe na justification? Mwaka huu mmeshikwa pabaya
 
Nakubaliana na wewe sehemu kubwa sana, nina mifano mingi sana huwa naongea na watu mbalimbali mtaani kwetu nilichokigundua ni kwamba watu wengi linapokuja swala la kupiga kura huwa hawabadiliki wataonyesha ushabiki wa hapa na pale lkn ukimbana na kumuuliza sasa utamchagua nani atakwambia mimi ni CCM tu ingawaje kuna hili na lile lkn namkubali Magufuli, na wale waliokuwa wanapenda chadema au cuf watakwambia hivyo hivyo hawabadiliki sana hivyo mwenye hazina ya wanachama wengi ndiye atakayeshinda uchaguzi na CCM wana hazina kubwa sana vijijini!

Hivyo naweza kusema ingawaje ukawa hawataki kukubali lkn matokeo yaliyotolewa na twaweza ndiyo yatakavyokuwa kwenye Uchaguzi Mkuu labda kutakuwa na +- hapa na pale lkn hayata tofautiana sana!
 
kushinda kwao itabaki kua ndoto isiotimia, milele, wanahitaji kujipanga upya, ccm inamiziz yake ya muda mrefu ya kudumu, wametengeneza chama chao mwisho wa siku wamekibomoa wenyewe bila kujua nini wanafanya.......nilikua nafikiria baadae chadema watakuja kuwa chama pinzani chenye ngufu, lakini kwa wanayoyapitia kipindi hiki nimeona kinaenda kufa kifo kibaya saana .......hata mama wa ACT kashawakalisha, propaganda nyingi, mahubiri mengi, vitendo ni zero, ccm lazma washinde tena kwa mwendo wanaoenda nao, ukweli ndo huo
 
ukweli wanashindwa kuamini kwa picha wanazoziona kweli ni vipofu mapovu yatawatoka pale tutakapo mmpeleka magufuli ikulu kwa wingi wa kura zote!

Ndugu utakuwa unajifariji tu ccm huu uchaguzi ni magumu kweli kweli mnasomba watu kwa malori muonekane mmejaza uwanja? Da kweli mna hali mbaya sana tukutane 25/10
 
Tatizo la UKAWA mgombea wao amefuzu usanii wakati CCM mgombea wao ni mwanasayansi kitaaluma. Sishangai kuona hawa wakawa wanakuwa wavivu kufuatilia uchambuzi wowote wa kisayansi. Lakini shauri yao, matokeo yake watayaona baada ya uchaguzi.
 
Ukweli unauma, ila tunajua kua ukweli ni mmoja na haugawanyiki na siku zote ukweli ukisemwa huegemea upande mmoja ambao unahitaji kupia. Siasa ni sayansi tena inayohiyaji ukae utulie ili uweze kutoa maamuzi yenye tija..

Ningependa kuongezea kitu kimoja kwenye maelezo yakoambacho ni VOTER'S BEHAVIOUR, hapa lazima tujue kwanini mpigakura anaamua kumchagua mpigakura X na siyo mpiga kura Y? Wengine hua wananmchagua kwa vile mgombea wanatoka nae sehemu moja, au wananshirikiana kwenye mambo mengine ya kijamii, wengine humchagua kwa vile wanawasikia wengine wakimsifia, wengine humchagua kwa vile kuna watu wanamchagua mfano shabikia anempenda Diamond anauwezekano mkubwa wa kumchagua magufulia kwa vile Diamond atamchagua.
 
Hiyo sayansi ni marekani na ulaya.
Watanzania walichofanyiwa na CCM hawatamani hata kukisikia hiko chama.
Na CCM wanajua hilo ndio maana wanataka kuchakachua kura.
Kama wangekuwa wanajiamini na hesabu zako feki wasingepoteza muda kuichakachua NEC.
 
pita pita zangu nimeshakaa na watu wengi wenye busara zao, nikijaribu kuwahoji juu ya uchaguzi majibu mengi ni magufuli, haswa wanafunzi wa chuo, nilifarijika saana maana pia nilijaribu kuwahoji kwanini sio mamvi, majibu niliyopewa kwanza, wamekubali ,magufuli ni mchapakazi, pili wanatazama maslahi yao ya sasa na vizazi vijavyo, mamvi akikabidhiwa nchi lazma ataanza kurudisha fadhila zake kwenye kundi kubwa linalo mtizama nyuma, pili afya yake (hatumkosoi tunattambua ugonjwa humpata yeyote yule hata sisi ) lakini kwa sasa tunatazama afya yake vile anayoteseka, leo mkampe nchi ni kumtesa sio kumpenda, tunaimani afya ina influence kubwa saana katika kazi na ndio maana huaga tunaomba ruhusa kazini, shuleni, vyuoni, pale tunapopatwa na ugonjwa ili tukajitibie tuweze pata nguvu ya kufanya kazi, hivyo wakiwa waaminihivyo kushinda uchaguzi sio swala rahisi kama wanavyochukulia, hayo mafuriko wanayojisifia ya dar .....wasiamini.....wakazane kutafuta ilani, na kumnadi mgombea wao kuliko kupoteza muda kuwasema ccm kwenye mitandao gap waliloachwa na ccm ni kubwa ............maneno yaliozungumza hapo juu ni ya ukweli kabisa , tukiacha ushabiki pembeni......tukutane oktoba !! magufli ataapishwaa hadharani kweupe
 
uongo unafanania ukweli
umesahau idadi ya waliopiga kura CCM 2005, 2010 !
rudi ukasome tena

Wewe kweli mbumbumbu mzungu wa reli. Hivi unadhani kwa sababu hatukupiga kura miaka iliyopita basi unadhani hata mwaka huu hatutapiga? Ngoja nikueleze: kadri mnavyoipiga vita ccm ndivyo tunavyokusanyana full squad wooooote ambao hatukupigaga kura! Subutuuuu wenyewe tupo tena tupo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom