Tangia anyofelewe kwenye Uwaziri mkuu kwa kashfa kubwa ya kuliingiza taifa gizani kwa mikataba ya kilaghai Bw E Lowasa amekuwa akionekana kwenye madhehebu mbalimbali na kitita cha fedha kuwasaidia ama kununua vinanda, madirisha, matofali, redio, viwanja, sherehe nk huku akiaambatana na kundi kubwa kumsaidia kuchangia hizo harambee.
Ameifanya ili kujitakasa na kile alichokifanya akiwa madarakani.
JK alitumia nyumba za ibada kuingia ikulu madhara yake wote tunayaona. E Lowassa kajikita kwenye nyumba za ibada kujitakasa na kuomba kura.
Madahara yake ni makubwa sana, viongozi wote wa dini wanaoshabikia haya nao ni majanga ya kitaifa. Huwezi kumsafisha mchafu kwa fedha. Tanzania tufike mahali tumuogope Mungu. Hili swala la watu kutaka kuonekana wasafi wakati hawataki kutubu dhambi zao na kurudisha vyote walivyopata kwa ulaghai kwa masikini ndio wamfuate Mungu ni kebehi sio tu kwa madhehebu husika bali kwa viongozi wote wa dini wenye tamaa ya fedha chafu.
Kiongozi wa dini wajibu wake ni kukemea maovu na kufundisha kuhusu toba na kuwa mfuasi wa Mungu kwa matendo. Sidhani kama ni kazi yao kushamirisha matendo maovu kwa kupokea vipande vya dhahabu vya Yuda baada ya kumuuza Yesu.
Kesho watu hawa wanaotumia nyumba za ibada wakiingia Ikulu watakuwa viongozi wa nani?
Matumizi ya nyumba za ibada kwa vipande vya dhahabu ni dhihaka kwa Mungu. Kuhonga kanisani/Msikitini ni dhambi kubwa sana. Naomba wote wenye tabia hii chafu waache mara moja.
Udini ni zao la umasikini, wizi wa mali ya umma siasa chafu na tamaa ya madaraka. Viongozi wabovu duniani kote wanatumia kete ya kutenga na kutawala kwa gharama hata ya machafuko ya kidini, kikabila nk.
Ni wajibu wa viongozi na waumini wa dini zote kujua mbinu chafu za wanasiasa mufilisi. Nyumba za ibada sio sehemu ya kumtakasa mchafu kisiasa ili akubalike, kumbukeni wengi wamevaa ngozi ya kondoo na sio kondoo.