Lowassa na Makamba warudia yale yale muda mfupi baada ya kifungo

Lowassa na Makamba warudia yale yale muda mfupi baada ya kifungo

DSN

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
2,837
Reaction score
1,688
Hakika kwa watu wenye UFAHAMU ni AIBU.
Kuna nini? Hivi mpaka kutumia sytle hii amuoni hata ujenzi wa nyie mnaojiita watetezi wa Lowasa na yeye mwenyewe amuoni kuwa MNA JIALIBIA kwa makosa yale yale ambayo Kamati ya Maadili imeyasema WAMEYATENDA NA WATAENDELEA KUYATENDA.

Mfano kosa ambalo bosi wao wengi kaendelea kulitenda kama anavyo endelea kulitenda katika kuthibisha hilo, connection ya mahojiano ya muhusika tajwa, ambae muda mfupi ameachiwa na kaambiwa usipige kampeni mita chache toka kwenye kifungo analudi kwenye tatizo lile lile bila hata kukumbuka kuwa katoka kwenye huluma japo ya kumweka sehemu atafakari kwa ujio wa fyagio ambalo laweza kumfikisha sehemu asiyotalajia unalala Maskini unaamka Tajiri.Kwanini yote hayo kwa kuwa UMEPITILIZA NA KUWAFANYA WATU WAZIMA WENZIO WAJINGA.

EBU HONA HII KAULI ZA MAHOJIANO YA EDWARD NGOYAYI LOWASA NA GAZETI LA MWANANCHI
Lowassa: Safari ya matumaini
Hali ya kusubiri filimbi ya kampeni ipulizwe pia ilionekana kwa Lowassa ambaye alijitetea kuwa ni muadilifu na anayeipenda CCM kwa dhati. "Sasa ninaanza safari ya matumaini. Niliianzisha mwaka juzi kule Arusha, nilisema niungane na watu katika safari hii nashukuru wameniunga mkono," alisema waziri huyo mkuu wa zamani.

"Ninachotaka tuungane zaidi, tutaianza rasmi safari yetu niliyosema ya miba, mabonde, misukosuko na sasa tumefikia mahali… Mei 30 nitatangaza rasmi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid," aliongeza Lowassa.

Kwa mtu yoyote makini mwenye kujua mfumo unafanyaje kazi na mwenye ufahamu wa kipi ni sahihi na kipi si sahihi What is Wrong and What is Right maneno niliyobold yanatosha kumuengua mgombea kwa kuwa yamezungumza kile kile kamati ya maadili imetoka kukikataa huku ikiwa imempa tahadhali kuwa uvunjaji wa kanuni utaangalia wakati uliopita, uliopo na utakao kuja.Kisha mtuhumiwa aliye acha huru muda mchache anaruka ....anakanyaga......hivi jamani hakuna strategist na Maanalysit wa kumuongoza nini kisemwe na kutendwa na muhusika na ikibidi hata wale strategist behind the scene wafanye nini ambacho hakitausishwa na muhusika.

''MATUMIZI YA KAULI AMBAYO NDIYO UVUNJIFU WA KANUNI....

1: Unaposema ''SASA NINAANZA SAFARI YA MATUMAINI''-
Kwa kiswahili sanifu NENO SASA maana yake ni kusema MUDA ule unatamka maneno hayo basi Kampeni hiyo inaanza kufanya kazi pale pale.Neno SASA matumizi yake kwenye kauli hii kampeni inaanzia pale alipolitamka kwenye mahojiano haya na gazeti la Mwananchi.

2: Unaposema ''NILIIANZISHA MWAKA JUZI KULE ARUSHA''
Kwa kiswahili sanifu pia ''NILIANZISHA MWAKA JUZI KULE ARUSHA''hapa aitaji maelezo kutamka ni Kiswahili kipi kutafsiri muda gani mtu huyu alianza kampeni lini...ameshatamka kuwa kumbe kampeni alishainza toka mwaka juzi.Je katika kanuni zake CCM zinasema nini kuhusu Mwanachama wake anae anza kampeni za kutaka Urais toka mwaka juzi....sentensi hii IMEMALIZA KILA KITU.

3:Unaposema ''NILISEMA NIUNGANE NA WATU KATIKA SAFARI HII NASHUKURU WAMENIUNGA MKONO''
Pia Kiswahili sanifu unaposema ''NILISEMA NIUNGANE NA WATU KATIKA SAFARI HII NASHUKURU WAMENIUNGA MKONO''. Watu wepi hao waliokwisha kuanza kampeni ya Urais kabla ya muda huku Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa madarakani.Ni kwa kanuni ipi CCM ina ruhusu Mwananchama wake kuanza kampeni huku muda lasmi aujaanza.Je nafasi ya Wanaccm wengine na Watanzania wengine wasio wana CCM yani CDM/UKAWA wenye nafasi na haki inayolindwa Kikatiba kupokwa nafasi yao ya ushiriki wa kufanya kampeni kama huyu ambae katamka wazi kuwa alikwisha anza safari ya kuwania URAIS toka mwaka juzi.

CDM/UKAWA kwa kauli za namna hii toka kwa mtu ambae alishapata kuwa mtu wa PILI toka kwa Rais kwa mfumo wa Tanzania BARA...kauri yake hiyo inawapa nafasi gani kwenye fikra zenu...Je mtakuwa mmeathrika vipi ?kwa kupokwa nafasi hiyo pia kwani kumbe nanyi mlikuwa na nafasi sawa toka mwaka juzi kuingia kwenye ground katika kuanza safari ya matumaini kwa namna yenu lakini lengoo likiwa ni URAIS.Na hakika kitendo cha DK SLAA kutoa viashilia vya kutaka URAIS kabla ya muda leo ingekuwa mambo mengine kabisa.

Na hakika kama ni swala la TIMING any timing kwenda kinyume na kutii kanuni za Uchaguzi za CCM na za Kikatiba uchgauzi huu utaleta Mushkeri sana.Na Mushkeri mkubwa kwa kuwa yaliyotamkwa kama haya yapo...mpaka level ya kijiji...harusi, mikutano ya kanisani, misikitini, na kwingeneko.Hakika litaepukwa ili kwa wahusika pale watakapo ona kwa faida yao na faida ya chama chao, kuwa walikwenda kinyume na Kanuni za CCM na KIKATIBA na kuwapoka wengine HAKI za MSINGI.Hivyo basi KUTOKUSHIRIKI KWAO KWA KUTOKUCHUKUA FORM ZA URAIS kutaondoa ajenda mbaya ambayo itavulumisha manenio ya kiasi kuwa CCM itaingia pabaya kabla ya kufika mbali kimalengo na kuhatalisha mikakati yao ya ushindi.

Au Pia kuwaacha waingie kwenye kinyanyiro na CCM kufanya maamuzi ya KIKANUNI kuwaengua kwa VIGEZO ambavyo mwenyekiti wao kayasemea vyenye sura ya KITU BORA KISICHO NA MAWAA kwa umma wa Watanzania walio wengi na sio kwa faida ya WANACCM kama ambavyo siku zote wamekuwa wakijitutumua Mwenzetu.Mwanaccm yoyote mwenye SURA YA DOA LA KIFISADI AU RUSHWA ni HATALI SANA kusogezwa kwenye kinyanyir hiki kwa kuwa UMMA wa Watanzania ulipofika unatka RAIS ambae RUSHWA na UFISADI ni ADUI mkubwa kwenye DAMU yake.

Na katika mahojiano hayo kila mmoja alijibu huku akiwa na weredi ambao kwa watu makini na wenye upeo wa weredi kila mmoja anaweza kuwa judge hata hulka zake kabla ya kufikisha katika kamati ya maadili na mara baada ya kufikishwa kwenye kamati hiyo.Ufahamu wa watu hao wa kutambua
NINI CHA KUSEMA, WAPI, KWA SABABU GANI,KWA NINI, NA KWA YUPI? [WHY, WHEN, HOW, WHO AND WHERE?]Watu wa mikakati wanaziita FIVE W?

Nikileje katika sehemu ya mwisho nataka nitoe tofauti ya LOWASA na wagombe wenzie walipoojiwa na gazeti la Mwananchi walijiubu nini?Na kwa kujibu hivyo walijiweka wapi na kuhakikisha hawavunji kanuni wala kuonyesha hisia zozote kuwa wao hawaheshimu kanuni zao chama chao na kuwa WAO na chama chao Cham ni ZAIDI ya wao.
TIZAMA MAHOJIANO YA WANACCM WENZIE NA LOWASA.

MAHOJIANO YA JANUARY MAKAMBA:
Makamba: Safari ya ushindi
"Nimefurahishwa na uamuzi wa Kamati Kuu.Safari ya ushindi sasa inaanza," alisema Makamba alipohojiwa kuhusu tamko hilo la Kamati Kuu. "Sijashangaa hata kidogo (kusikia uamuzi huo) kwa kuwa sijawahi kukiuka maadili ya chama. Sasa nasubiri muda wa kampeni kutangazwa ili nianze kufanya hivyo kwa kuzingatia kanuni za chama kwa sababu najua wakati wa mchujo wa wagombea, CCM itaangalia tena jambo hili."
Huyu anafahamika uwezo wake wake wa kufikilia nae kidogo alichemka na kutaka kujisahau nae akapelekea kulopoka.Mfano huo wa kauli tata ni kama ifutavyo

1: Aliposema ''SAFARI YA USHINDI SASA INAANZA'''
Hapa hurka ya kijana huyu ambae kwa sehemu hii namlaumu kukurupuka na kwenda kwenye kinyanyiro ambacho kwa weredi wanamuona kama ni kijana mwenye tamaa ya makuu na si mwenye usikivu wa kufuata nyayo za watu wazima mpaka pale watu wazima watakapo muitaji kuwa sasa ANATOSHA kukaa sehemu za kuongoza watu wa kila rika wakiwa na familia zao.Akiona anazungukwa na watu wa aina ya corporate level basi akajiona anaweza kuongoza Watanzania.Kama ni RAIS wa kada ya Corporate people basi its OK.

Sentensi hiii SAFARI YA USHINDI SASA INAANZA ina maana na yeye kampeni kesha ianza kabla ya Muda....kwa kutokujitambua yeye mwenye na kushindwa kujua FIVE W ni kudhihirisha kuwa AJUI umuhimu wa ANAZANI ANAWEZA KUPEWA.Kauri hii nayo imemchinja Dodo huyu kumfanya apotee kwenye dimbwi la kujiandaa na kuludi sekta binafsi kuwatumikia watanzania wenzie kwenye sekta binafsi

MAHOJIANO YA NGELEJA:
Ngeleja: Nasubiri muda
Ngeleja, ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini, aliishukuru Kamati Kuu kwa kufikia uamuzi huo akisema imezingatia misingi yote ya haki na kwamba kilichobaki ni kusubiri muda wa kampeni. "Hatua inayofuata ni kuhakikisha kwamba nafuata kanuni, taratibu na miongozo ya chama katika kugombea nafasi nitakayoiomba," alisema mbunge huyo wa Sengerema...

Good .ujuzi wa sheria umemfanya kujua FIVE W, hivyo kumfanya ajue kuwa kanuni zinaitaji kipenga kilie.Huyu amejitambua na kujua safari yake ni nini...Kidogo anamwelekeo wa kujua Kanuni ya Maadili inamaanisha nini katika mwongozo mara baada ya kifungo.Ingawa kwa kufunguliwa huko sio kuwa kunamfanya waliokuwa kifungoni sasa wako huru na waendelee na michezo watoto wa mjini wanaita Michongo/Mishemishe ya Mjini kujifanya kundi fulani liko mbele kuupata URAIS kuliko wengine...kumbe ukiwa mbele kuna watu washafika KITUONI saa nyingi wanakusubilia utelemke na mabegi yako wakupokee na kukupa Pole ya Ya SAFARI.

Membe: Idumu CCM
Naye Membe alipotafutwa kwa simu kuhusu hatua hiyo ya Kamati Kuu ya CCM, simu yake iliita bila kupokewa lakini alipotumiwa ujumbe mfupi, alijibu: "Kidumu Chama cha Mapinduzi
Bravooooooo na execellent jibu yani huyu FIVE W zimemkaa mpaka zikapitiliza...anajua CCM Wanataka nini wasikie toka kwa Mwanaccm wenzie.Hili ndio jibu sahihi la Mwanaccm yoyote makini mwenye ufahamu wa Chama Chake na TAIFA lake linafanya kazi vipi...kwa ujumla anajitambua na kujua mfumo unafanyaje kazi.

MAHOJIANO YA SUMAYE:
Sumaye: Tunasubiri maelezo
Sumaye, ambaye alikuwa waziri mkuu wa Serikali ya awamu ya tatu kwa kipindi chote cha miaka 10, alisema kimsingi kifungo kilikwisha tangu Februari mwaka huu, lakini anashukuru kwamba CCM imekaa na kufikia uamuzi huo hivyo anasubiri kupata taarifa rasmi na taratibu za kufuata kwa wagombea wote wa chama hicho.

"Nimeona tu kwenye vyombo vya habari lakini naamini kutakuwa na maelekezo kwa wagombea wote wa urais kwa maana sasa tupo kundi moja," alisema Sumaye. Aliongeza kwamba kwa kuwa wamefunguliwa ikiwa imebaki miezi mitano kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, itabidi wagombea wanaodhani wamechelewa kujinadi kwa wananchi watumie nguvu ya ziada..

Bravoooo and execellent ..hawa ndio wale wale wenye kujitambua majibu yao ni ishara ya kutambua usahihi wa jambo...kumbuka ni miaka mingapi Mh Sumaye ametambua na kuwa na ufahamu wa hayo ambayo amejibu kwayo hapo juu.Ni muda mlefu sana sana..na kuna kundi kubwa uko juu ambalo halikutambua majibu ya sasa ya Ngereja, Membe na Sumaye kuwa ndio majibu daima ya Chama CHA MAPINDUZI [CCM] na ya KIKATIBA yalipaswa kuwa midomoni mwao sehemu mbalimbali toka uchaguzi ulipoisha mwaka 2005 kuelekea Nov 2015, hadi kipenga cha uchaguzi kitakapolia mezani.

Sasa kama una Mwanachama wa CCM ambae wewe unamjua alianza harakati mapema na kila alipokutaa na Magazeti, Luninga aka television na akiulizwa URAIS alijibu Kikampeni kampeni baada ya kutoa majibu kama waliyotoa wakina Ngereja, Membe na Sumaye.
 
LOWASA NI fisadi mkubwa,marafiki zake wote ni mafisadi,hakika nawaambia jumapili ya leo lowasa akishika nchi lazima chenge awe waziri mkuu na rostam awe waziri wa nishati na madini,wengine mtamaliziaga mie ngoja niende kanisani kabla alshabaab hawajatupata
 
Uwa nacheka sana kuona pro-Chadema ndiyo wanafanya kazi ya kuwajadili wagombea wa CCM.

Toka juzi nakuambia unachanganya matumizi ya R na L.

Hebu fanya mazoezi ya matumizi ya hizi herufi.
 
Mleta uzi wewe ni raia wa nchi gani? maana nchi imejaa wakimbizi na tunawajua tu kwenye kuandika Kiswahili,

Mnajialibia===mnajiharibia
Analudi ===anarudi
Fyagio == fagio
Asiyotalajia== asiyotarajia

Hivi walimu wa somo la Kiswahili ndio hakuna kabisa huko mashuleni?
 
LOWASA NI fisadi mkubwa,marafiki zake wote ni mafisadi,hakika nawaambia jumapili ya leo lowasa akishika nchi lazima chenge awe waziri mkuu na rostam awe waziri wa nishati na madini,wengine mtamaliziaga mie ngoja niende kanisani kabla alshabaab hawajatupata

Wivu kwa watu wenye maendeleo. Kuna mtu alimwambia baba yako acheze bao wakati watubwanatafuta hela?
 
Mkuu DSN urais siyo ajali kwamba utaupata from no where na zama za kuamini kuwa ccm ikimteua mtu asiyejulikana asiye na makundi imeshapitwa na wakati. Kutengeneza timu ya watu wanaokuunga mkono si dhambi. Makundi ndani ya chama ni ruksa kuelekea uchaguzi na ndivyo inavyofanyika kote duniani. Hizi jitihada za kumchonganisha mzee yt hea na chama chake hazijengi. Acheni mziki uendelee
 
Last edited by a moderator:
Alianza safari yake mwaka juzi Arusha ya kuanza kugawa rushwa na mwaka jana akaingia awamu ya kupanga makundi ya watu na kuwapa fedha ili waende kumshawishi ili hatimaye ashawishike kwenye media mwaka huu. Kafikia mahala sasa pa kutumia fedha, kuwashawishi wajumbe wateuzi wa ccm wamteue ili amalizie safari yake ya matumaini. Matumaini ya kumalizia taifa.

Lowasa hawi raisi wa Tanzania!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Uwa nacheka sana kuona pro-Chadema ndiyo wanafanya kazi ya kuwajadili wagombea wa CCM.

Toka juzi nakuambia unachanganya matumizi ya R na L.

Hebu fanya mazoezi ya matumizi ya hizi herufi.
Ritz nshakwambia ntoka bara man...R na L ni viungo.
 
Mleta mada,

Mambo ya Lowassa yanakuhusu kweli? Au unataka kuungana na timu ushindi? Fanya fasta, wakati ni sasa.

Lakini kabla ya kujiunga, fanya kwanza alichokushauri Ritz.
 
Unatuharibia Lugha yetu adhimu...
Mother tongue muraaa mhaya anasema ngombe badala ya Ng'ombe sio kosa lake..ukizingatia siitaji mhariri wa habari hiki si chombo lasmi kama gazeti la TAIFA.
 
Back
Top Bottom