Lowassa na genge lake Vs gesi yetu!

Lowassa na genge lake Vs gesi yetu!

Mkuu kama unayajua yote haya na una ushahidi si uende kwenye vyombo husika kwa hatua zaidi?
Tatizo watanzania wengi waliopo humu wana msimamo huo mmoja tu wa kuiingiza UKAWA mjengoni.
SIdhani kama itakuwa mahala sahihi hapa kuendesha mjadala wako huu.
Kusanya data zako nenda KISUTU pale mahakamani.

Baada ya kujimilikisha Migodi yetu yote ya TanZania na kuwaachia wenyeji mashimo sasa fisadi Lowasa na Genge lake wamegeukia Gesi yetu, hii Gesi ndiyo inayowapeleka puta, hizi kelele zote, huku kutafuta Uraisi kwa gharama yoyote ile kwanza kulianzia ndani ya CCM kukashindikana na sasa kumehamia chadema kuna lengo moja tu nalo ni Gesi yetu iliyogunduliwa kwa wingi huko Pwani ya Kusini mwa nchi yetu!

Mafisadi wakiongozwa na Lowasa baada ya Wazalendo wa CCM kuwashtukia na kuwanyima Uraisi sasa wamehamishia nguvu zote upande wa Upinzani dhidi ya Chama Dola rejea watu walio kwenye Genge la Fisadi Lowasa ni Mengi huyu anajulikana kwa ugomvi wake na Waziri Muhongo baada ya kunyimwa kitalu cha Gesi kwa kuwa hakuwa na uwezo wa kukiendeleza, Rostamu Aziz huyu ndiye mwizi mkubwa wa Rasilimali zetu rejea nani anatenda ya Migodi yote ya dhahabu nchini, Karamagi huyu ndiye aliyeuza Migodi yetu hotelini huko nchini Uingereza, Rugemalira huyu ndiyo King maker wa Escrow na saga lote la Richmond n.k

Hivyo kama MtanZania na mpenda nchi yangu naishukuru sana Kamati ya maadili kwa kuliona hilo na kulikata jina la fisadi Lowasa, ikumbukwe kwamba Kamati ya maadili inajumuisha maraisi wetu wastaafu na watu wetu wa Usalama hivyo kuna mambo waliyoyaona ambayo sisi watu wa kawaida hatuna uwezo wa kuyaona ila ni jukumu letu kuwaelimisha Manyumbu ambao wananunuliwa viroba na fisadi Lowasa ili walete fujo!

Hongereni Kamati ya Maadili ya CCM!
 
ufisadi... kwanini anakuwa mgumu kuongelea ufisadi...?

Asingeweza kwa sababu waliomfadhili kukamilisha adhma yake ya ufisadi nao ni mafisadi.
Angeweza kukosa ahadi alizoahidiwa. Naendelea kutafakari
 
Back
Top Bottom