Lowassa na bomu lijalo

Mazoko

JF-Expert Member
Jul 10, 2009
674
184
Naomba kuleta hoja hii mbele yenu tuijadili hoja kama hoja na sikumjadili Lowassa au nafasi aliyokuwa nayo kama waziri mkuu.

Kuna vitu twaweza kubeza na kunavitu nilazima vifanyiwe kazi kwa faida ya Taifa ili tuendelee kuhubiri amani

Mh.Lowassa mara kwa mara ameonekana kuguswa na vijana ingawa nibaada yakuenguliwa uwaziri mkuu kuwa nilazima kuwaangalia vijana na kuwasikiliza hasa wasiokuwa na ajira rasmi lasivyo nibomu lijalo ambalo likilipuka hakuna atakayeweza kulizima.

Nimefanya ziara fupi isiyo rasmi kuzunguka katika baadhi ya maeneo hapa Dar-es-Saalam kuangalia vijana wenzangu wana fanya nini na nini wamekosa na mawazo yao niyapi juu ya mstakabari mzima wa maisha yao.Kwa kweli inasikitisha hasa ukiona jinsi walivyokata tamaa ya maisha yao ningumu kupata kujuwa wanafikiri nini hapo baadaye.

Sehemu nilizo kwenda ni Kariakoo,Tandale,Ubungo mataa na Tandika sokoni.Kwa wale wazoefu au waliokwisha wahii kupita maeneo hayo wanaweza kukubaliana na mimi kuwa taifa linapoelekea si salama tena.Kwa nini nasema hivyo nikwakuwa watu hawa wanafanya shugulizao katika maeneo yasiyo rasmi na salama kwao na watumiaji wengine wa maeneo hayo.

Mfano eneo la Kariakoo utakuta vijana wamepanga vitu vyao barabarani sehemu ambayo gari linatakiwa kupita lakini wao wanaona ndiyo sehemu yakupata mkate wao wasiku.Juzi nilishuhudia gari likishambuliwa na vijana hao eti gari limekanyaga biashara zao.nilijaribu kuongea na baadhi yawaliokuwa wanafanya vurugu majibu niliyoyapata nikuwa hivi ndivyo wanataka tuishi kwa kufanya biashara barabarani wao na magari yao watajuwa niwapi pakwenda hatuogopi mtu tuko tayari kwa vita huku mwingine akiwaambia mgambo kuwa hapa hamnipeleki wala kuchukua mali zangu labda mniuwe maana mwenzeni kaisha chukua hela (RUSHWA) ilikuwa nipatashika.

Eneo la UBUNGO hapo sasa ndiyo panatisha zaidi kwanza hakuna eneo lakutosha kufanya biashara yoyote kwa kuwa sisalama kwa wao wenyewe kutokana na mitambo iliyopo pale na hata kwa watumia barabara maana kuna njia za watembea kwa miguu na mageti yakuingia kwenye ofisi za mitambo hiyo ya umeme.

Najaribu kujiuliza hivi siku akatokea mwehu mmoja akaamua kujitoa muhanga na bomu si nchi nzima inakuwa gizani na taifa kupoteza vijana ambao ndiyo nguvu kazi wanaofanya biashara eneo hilo ambao wanafikia elfu mbili nakuzidi??

Najiuliza viongozi wa nchi hii nao wamekata tamaa kama vijana hawa na kuruhusu kila mtu afanye anavyotaka au wao hawawaoni?? yawezekana Kariakoo hakuna anayekwenda huko maana viongozi wetu wasasa huduma zote ni SUPERMARKETS.Je ubungo mbona nasikia mawaziri wanatembelea mitambo hiyo hawaoni?

au wanapoenda Dodoma hawapiti hapo kwa kweli naona wamechoka kama hawa vijana bora siku zipite.Vurugu zilitokea Mbeya vijana wakakubali kumsikiliza mbunge wao Mbilinyi wakatulia ikitokea kwa taifa zima watamsikiliza nani ili watulie??????? HILI NI BOMU linalipuka mda wowote
 
Hili la Lowassa kuguswa na vijana limeanza baada ya uchaguzi wa 2010. Data zote walizo nazo CCM na tume ya uchaguzi zinaonyesha kuwa vijana kwa idadi kubwa hawakuipigia CCM katika uchaguzi huo. Ukizingatia kuwa watoto waliokuwa na umri wa miaka 13 mwaka jana watakuwa ni vijana wanaoweza kupiga kura 2015 hauhitaji mtaalamu wa sayansi kukuonyesha ni kwa nini Lowassa ameanza kuzungumzia ajira ya vijana. It is purely political opportunism.
 
Lowasa ndilo bomu zaidi ya vijana kwa nchi hii. Alimpenda zaidi Kikwete kuliko watanzania. akaacha atutapeli na RICMOND/DOWANS zao na leo watanzania tunadaiwa bilions 111 kwa sababu ya mapenzi ya Lowasa kwa JK. angetupenda watanzania na vijana anaojifanya kuwazungumzia leo angetuokoa katika hilo ambalo alikuwa na uwezo nalo. kwa nini alikaa kimya juu ya utapeli wa RICHMOND/DOWANS kama kweli anawapenda vijana wa nchi hii bilion 111 zingeweza kuwekezwa zingetoa ajira kwa vijana wangapi?
aache unafiki na mbinu za kijinga. CCM wote wameoza hizo ni mbinu tu kujifanya leo anawaonea huruma vijana.
 
Namkubali sana EL coz ni mchapa kazi na anaguswa na matatizo.

Aliguswa na RICHMOND/DOWANS akamuonea huruma JK akakaa kmya kumuokoa na kuacha watanzania masikini wabebe mzigo wa utapeli wao Bilions 111. JK alisema hamjui DOWANS. anayetakiwa kulipwa ni RA rafiki yao mkubwa. Akili ya kawaida kabisa inonyesha hawa wote ni matapeli na ni BOMU zaidi kwa nchi hii, tena sio bomu la baadaye ni bomu linalotulipukia leo.
 
duu inabidi tuendeleee kuwa wajinga hivi hivi ilituje kufa bila ya wananchi kuwa na maisha yanayoeleweka..
 
acheni kujadili watu,kila siku Rostam,lowassa na jk tangu mmeanza mipasho mmwaathiri nini? mmezuia wizi gan?kwenye masanduku ya kura wanapita (iwe kwa wizi au ushindi wa kimbunga), MLALAHOI ANALALAMIKA NA GREAT THINKER NAE ANALALAMIKA sasa tofauti yenu ipi? au nyie ndo mloingia JF fungulia mbwa!!!!,anzeni kuleta mijadala tofauti na ya vijiweni,niambieni nchi gan imekombolewa kwa style ya mipasho??
 
... Nimefanya ziara fupi isiyo rasmi kuzunguka katika baadhi ya maeneo hapa Dar-es-Saalam...
Sehemu nilizo kwenda ni Kariakoo,Tandale,Ubungo mataa na Tandika sokoni...
Ungetembelea pia maeneo ya Kisarawe, Chanika, Pugu, Bagamoyo, Mlandizi na mengine ya pembezoni uone jinsi ardhi kubwa iliyo na rutuba ikiwa haina cha kufanyiwa... ni mawazo ya nyongeza tu
 
acheni kujadili watu,kila siku Rostam,lowassa na jk tangu mmeanza mipasho mmwaathiri nini? mmezuia wizi gan?kwenye masanduku ya kura wanapita (iwe kwa wizi au ushindi wa kimbunga), MLALAHOI ANALALAMIKA NA GREAT THINKER NAE ANALALAMIKA sasa tofauti yenu ipi? au nyie ndo mloingia JF fungulia mbwa!!!!,anzeni kuleta mijadala tofauti na ya vijiweni,niambieni nchi gan imekombolewa kwa style ya mipasho??
Tunashindwa kukujibu kwa kuwa hueleweki unaongelea nini. ipi ni mpasho katika yaliyoongelewa? eleza kwa ufasaha uelimishwe. maana ujinga si kosa dawa yake ni kuelimishwa tu.
 
acheni kujadili watu,kila siku Rostam,lowassa na jk tangu mmeanza mipasho mmwaathiri nini? mmezuia wizi gan?kwenye masanduku ya kura wanapita (iwe kwa wizi au ushindi wa kimbunga), MLALAHOI ANALALAMIKA NA GREAT THINKER NAE ANALALAMIKA sasa tofauti yenu ipi? au nyie ndo mloingia JF fungulia mbwa!!!!,anzeni kuleta mijadala tofauti na ya vijiweni,niambieni nchi gan imekombolewa kwa style ya mipasho??

Wewe hapo unajadili nini kama siyo watu pia?
 
Back
Top Bottom