Centrehalf
JF-Expert Member
- Jun 9, 2013
- 509
- 145
Salaam wana jamvi.nimefurahishwa sana na mwenendo wa vigogo ndani ya CCM jinsi wanavyohangaikiia nafasi ya mgombea urais wa CCM mwaka 2015?
Nimesikia majina mengi ya wenye nia ya nafasi hiyo nyeti akiwemo mzee Sitta,Benard Membe,January Makamba,Edward Lowassa,na wengine wengi tu.
Katika mbio hizi wapo wanaofanya harakati zao kwa kificho sana,pia wapo ambao wanafanya harakati zao bila kificho akiwemo makamba,Sitta na Lowassa.
Katika kundi hili naweza kusema Lowassa kawapiga bao wenzie kwa staili yake yakuchangia na kuongoza harambee nyingi makanisani,misikitini na hata kwa waendesha bodaboda ametua.
Kwa upande wa chama Lowassa anawafuasi wengi kwenye vikao vya maamuzi ikiwemo nec na mkutano mkuu.kwa hayo machache niliyoeleza ni dhahiri kwamba lowassa ndiye mwenye nafasi kubwa kuliko wenzie wote kaitka mbio za kuwania urais mwaka 2015 kupitia ccm,kwa hiyo basi ili CCM itulie ni lazima Lowassa apewe nafasi hiyo.
Vinginevyo hata akishindwa lazima ahakikishe ameshindwa kwa haki.Na hata akishinda sidhani wakina Sitta,Membe na wengineyo kama watakuwa tayari kumpa ushirikiano.
kwa kifupi ni kwamba matokeo yoyote lazima yatakiacha chama cha ccm kwenye mgogoro mkubwa utakaokua na faida kwa wapinzani.
Nasema hivyo kwa sababu wapinzani wanafuatilia kwa karibu sana mchakato wa kumtafuta mgombbea urais kupitia CCM.
Na ni kwa maana hiyo upinzani unasema unauhakika wa kutwaa dola mwaka 2015 ni kwasababu lowassa akishinda wao wanasema hawatakua na kazi kubwa ya kuwaeleza madhaifu na madhambi ya lowassa na Lowassa akishindwa atakuwa amewasaidia kuisambaratisha CCM.
Kwa mantiki hiyo lowassa ni mtaji wa CCM na upinzani pasipo yeye kujua wala chama chake kujua.Lowassa ni mtego ndani ya mtego na wasilisha.