Inashangaza wagombea hawa, wanaoshabikiwa na kundi kubwa la Watanzania, Walikuwa serikalini, wakiwa kama wasimamizi wakuu wa shughuli za Serikali, leo wanaongea utafikiri wao ni wapya, tunawashangilia eti kwasababu tumeichoka CCM.
Mimi ni mmojawapo kati ya walioichoka CCM, lakini kuniletea waliokuwa mawaziri wakuu ambao wanasimama majukwaani na kuikosoa serikali ambayo kwa miaka 13 wao wamekuwa ni viongozi wakuu katika shughuli za Serikali ni mchezo wa kuigiza.
Sumaye miaka 10 umeshau nini huko serikali, huyo unayemnadi Lowassa amesahau nini kama sio njama za kuwahuumu watanzania.