Lowassa, mazoezi ya picha ya nini na unamuonesha nani?

mkuu sio edo tu ni ccm nzima imeoza kwa ufisadi.. muhongo, maswi, tibaijuka, membe akishilikiana na shimbo kula hela za un kwa vijana wetu wanaopigania amani nchi za nje, au niendeleee.....???
Akili za kuambiwa changanya na zako kisha Tafakari
 
Ukitaka kuwa tia kiwewe CCM waambie kuhusu LOWASSA angalia makada wanatafunana wao kwa wao nimependa sana hii MEMBE & LOWASSA at 2015
 
Huu ni uongo usiokuwa na aibu. Mimi nikiwa News Editor siku ambayo gazeti lilikuwa na picha ua Lowassa akifanya mazoezi, jana yake nilishiriki kikao na hakukuwa na mjadala wowote kwenye kikao cha editorial ya Mwananchi kuhusu picha hiyo. Picha ile ilitumika kwenye gazeti kama picha ya mtu yeyote, na zaidi kwa kuwa ilikuwa newsworthy.
Mazingira anayotaka kujenga mtoa mada, ambaye sina shaka kwamba si member wa kikao hicho wala mwandishi wa Mwananchi, kwa sababu hajui kanuni, maadili wala editorial policy inayotuongoza, yanasukumwa na ushabiki na mapenzi yake kisiasa, akidhani kila mtu yuko kama yeye.
Mkuu Miruko, asante kwa kuliweka hili sawa!, tena waandishi wa kweli humu wapo, wala hawezi kujiweka wazi kihivyo na kuidhalilisha editorial ya Mwananchi kwa kuiwekea price tag kuwa ina practice "petty cash journalism!", kitu ambacho sio cha kweli!.

Naomba mkubushe mode akuwekee tag ya "verified user" ili kila ukichangia, ujulikane huo mchango ni from verified member!.

Thanks.

Pasco.
 
Hatuhitaji mtu analiwahi kuwa waziri wa maji akaishia kuanzisha DAWASA kwa manufaa yake binafsi,
Hatuhitaji mtu,ambaye amejiuzuru huku akisema yote haya ni sababu ya uwaziri mkuu tu.

Hatuhitaji mtu anayeona kuwagawia Bodaboda vijana ndio suluhisho la ajira huku akijua kuwa kutunza pikipiki,matengenezo yake ni gharama kubwa na kwa ushahidi vijana wengi wamenunua pikipiki zao lakini hazikuwasaidia.

Hatuhitaji kuwa na kiongozi atokeaye ccm ambaye ameshiriki huku akijua kuwa kuchakachua katiba ni kosa la jinai na kinyume na sheria ya mabadiliko ya katiba.

Tunajua,ni hadi ccm itakapoamua kujua kuwa ipo kwa lengo la wananchi, tutaichagua,Lakini kwa staili ya kugawana vyeo,kupanga safu,polisi kunyanyasa raia,kukamata wabunge na kupiga huku yeye yupo,sidhani kuwa mazoezi na project ya waandishi wa habari anaowanunua ndio suluhisho.

Mwisho niulize amegawa pesa mamilioni makanisani na misikitini,anagawia waandishi wa habari ili kumwandika vizuri,ameteka viongozi wa ccm kwa pesa,ameteka bodaboda kwa kuwaahidi neema,sasa akiingia ikulu na kila siku serikali hii ya ccm inasema Tanzania ni nchi maskini, je atarudishaje fedha hizo?, na mbona hata Mataifa ya nje kama marekani,ujerumani,china,india,ufaransa na mashirika ya WHO,UNICEF, UNDP,UN,UNESCO,WORLD BANK,PARIS CLUB nk
Mbona wanatupa misaada kwa masharti nafuu na mikopo ya muda mrefu?

Je,Lowassa anatukopesha tulipe kwa masharti yapi?

Kwani alikopa hiyo pesa ? Mpaka useme ataludishaje? Tambua pesa ya misaada inatoka kwa marafiki,jamaa na vyama ndugu wala hakutakuwa na mtu ataidai iludishwe, hata kule America wapiga kura huwa hawataki mtu masikini sana awe Rais kwani wanajua Kuwa akiwa Rais atautumia mda mwingi kujitajirisha badala ya kuwatumikia wananchi.,kugawa boda boda Kutoa misaada ni Haki ya kila Mtanzania hata wee ni ruksa kufanya hivyo usiwe na Ubahiri mwenzio lowasa kaamua kula na ndugu zako , lakini wewe umewekeza kwenye michepuko na fitna za kupikwa na Membe, ebu nenda kamuulize Membe ni kwa nini haitumii ile Pesa ya Gadafi kujenga miundo mbinu na Hosptal pale kijijini kwao? Mwambie Kuwa Walibya watakuja kuichukua kabla hajaitumia Kama Rushwa ya kusaka Urais.
 
Mtoa mada ni sahihi ulivyosema,generally kujionyesha hakunaga maana.ila naomba nishuudie mara kadhaa nimewahi muone lowassa akifanya mazoezi wakati anaishi obey,na tena watu wakaribu nae walisema alikua prescribed kufanya mazoezi na daktari.ni hayo tu
 
Du! Lowassa anawakosesha usingizi kichizi, mbona hoja hiyo inaibuka sasa hivi wiki kiasi mbili toka picha hiyo itoke.Mwenye uzi angedadisi basi na kwenye magazeti mengine waliyotumia picha Kama hiyo tena akiwa katika mavazi na eneo tofauti(kwa maana kuwa ni siku nyingine).Hiyo picha kihabari ilikuwa na maana kwasababu mtu aliyekuwa anakimbia(Lowassa) inasemekana ni mgonjwa hata kutembea hawezi, sasa vipi mtu huyu(tena kiongozi) anafanya mazoezi ya kukimbia na kutembea namna hii?Swali hili limemfanya mpiga picha na wahariri kuitumia.Tafuteni sababu nyingine jamaa yuko fiti na watanzania wanamsubiri kwa hamu kumrithi JK,Msitake kutuondoa katika mjadala wa Escrow account na IPTL
 
Mkuu, kwa kawaida Ugonjwa wa Rushwa huwa hautibiki kwenye hospitali za kawaida. Tulijenga hospitali ya rufaa kwa ajili ya wagonjwa wa rushwa ambayo ni PCCB. Hata hivyo inaonekana kuwa inazidiwa na wagonjwa na hatuna madaktari bingwa a kuwatibu wagonjwa sugu kama Lowasa.
Hao PCCB wenyewe wana njaa Kama ulivyo wewe, Membe kahifadhi Pesa za Marehemu Gadafi ili aje kuzitumia Kama Rushwa na tayari Lizaboni kala Rushwa amejitoa Fahamu kabsa haambiwi hasikii la Mtu yeye hamjui Mungu anaamini Membe ni Mungu kila analosema analiona Kama limetoka kwa Mungu wake Membe.Lizaboni tambua kupakaziana Maradhi ni kumbeep Mungu, Ugonjwa hauna hodi na mwakani ni mbali sana una Uhakika na afya ya boss wako membe? Kila mmoja aweza kuugua mda wowote usiwanyooshee kidole wenzako wakati wewe si Mungu unaweza ukaugua zaidi.
 
Lakini picha haionyeshi kama Lowassa alikuwa ana act hayo mazoezi; labda kama ali kuwa ana act na akachukuliwa pic wakati yuko kwenye peak

hiyo mikono na body language na huyo mtu wa nyuma anayemfuatia havionyeshi kuwa ana act!!!

plz come with another story
 
UKWELI KUHUSU "MAZOEZI" YA LOWASSA

Mimi ni Mwandishi wa gazeti la Mwananchi. Wiki mbili zilizopita tulikuwa na mjadala mkali sana kwenye kikao cha uhariri cha kuamua habari kuu za gazeti. Mjadala ulikuwa juu ya picha iliyotumwa na mpiga picha wetu kutoka Dodoma. Kuna baadhi ya wenzetu walitaka picha hiyo iwekwe ukurasa wa mbele wa gazeti. Kuna wengine hawakutaka kabisa iwekwe gazetini kwani gazeti lingeonekana ni nyenzo ya propaganda za siasa za Urais ndani ya CCM. Muafaka ukafikiwa kwamba iwekwe nyuma kwenye ukurasa wa michezo, ingawa nako kulikuwa na mjadala kwamba Lowasa ni mwanamichezo tangu lini. Wengine wakahoji kwamba tukiulizwa kwamba ilikuwaje gazeti letu likawa kwenye mazoezi ya Lowassa tutasemaje kwani huwa hakuna taarifa kwa umma kuhusu lini Lowasa anafanya mazoezi na anapitia njia zipi.

Baada ya mzozo kuisha, baadhi yetu tukaamua kufanya uchunguzi wa kina kwamba ilikuwaje mpiga picha wa gazeti akawa sehemu ya mazoezi ya Lowasa? Je alialikwa? Je alikutana naye kwa bahati mbaya? Pia wakati tunajadili kuhusu hii picha, kulikuwa na presha kubwa sana kutoka Kwa Mzee Lowasa mwenyewe kuja kwa viongozi wetu wakuu kwamba kwa gharama yoyote ile (wengine walisema milioni 10) picha hiyo lazima itoke ukurasa wa mbele. Bahati nzuri mantiki ikashinda na tukaliokoa gazeti kutoka kwenye aibu ambayo tungeipata.

Katika uchunguzi wetu ilibainika kwamba Bwana Abubakari Liongo, mbeba hela za Lowasa kwa waandishi, aliwatafuta wapiga picha wetu na kuwaambia kwamba kuna tukio muhimu la dakika 10 kwa Lowassa. Akatuma gari kumpeleka mpiga picha alipokuwa anatembea Mzee. Akapiga picha ya kutembea. Washauri wa Mzee wakamuomba akimbie kidogo, ikapigwa picha ya kukimbia. Mpiga picha akaambiwa arudishwe lakini akaamua kubaki kwakuwa ilikuwa ni karibu na mahali anapoenda. Akashuhudia Mzee akipanda gari na kuondoka. Ukitazama picha kwa makini utaona Landcruiser iko kwa nyuma.

Swali ni kwanini hadaa yote hii? Sababu ni kwamba ni kweli afya ya Mzee Lowassa imedhoofika. Kila mwezi anaenda kutibiwa Ujerumani, mikono inatetemeka na jicho moja linakaribia kufunga kabisa. Sababu ya kutaka picha hii itoke kwa gharama kubwa ni kujaribu kuuonyesha umma kwamba yeye ni mzima. Wapi wazee wengi wanaofanya mazoezi kila siku lakini hawahangaiki na kupigwa picha. Mzee Mwinyi ana miaka 89 na anatembea na kukimbia kila siku. Dr. Salim anakimbia kila siku. Jenerali Mirisho Sarakikya ana miaka 80 na anapanda Mlima Kilimanjaro kila mwaka kwa mwaka wa 30 sasa. Hatuoni wakihaha kupiga picha na kuzisambaza mitandaoni. Mazoezi magumu kwa Lowasa ni kushika kikombe cha chai kwa dakika 3.

Binafsi nimepata woga. Nimepata woga kutokana na uroho mkubwa wa madaraka ulioonyeshwa na timu ya Lowassa. Wako tayari kufanya chochote kupata madaraka. Bahati nzuri hadi sasa mambo mengi wanayoyafanya ni maigizo tu, ikiwemo hili la kutengeneza mazoezi feki na kuitengea bajeti picha ili ichapwe gazetini ni kusambazwa mitandaoni. Mungu Ibariki nchi yetu.

Mbona hukutueleza wakati mlivyoandika makala kuthibitisha kifo cha Balali na trip zote za marekeni mlipewa shs ngapi, kwa sababu watanzania tunajua mlitumiwa kutuhadaa
 
Akili za kuambiwa changanya na zako kisha Tafakari
mkuu funza ni bora kukaa kimya katika hili maana humu jamii forums watu wengi tunatumia id feki (na mim ni mmoja wapo) huwezi kujua aliyeandika ni nani na anajua nini katika hili.
 
Last edited by a moderator:
Lakini picha haionyeshi kama Lowassa alikuwa ana act hayo mazoezi; labda kama ali kuwa ana act na akachukuliwa pic wakati yuko kwenye peak

hiyo mikono na body language na huyo mtu wa nyuma anayemfuatia havionyeshi kuwa ana act!!!

plz come with another story
Tambua Kuwa Membe kazimega zile Pesa za Marehemu Gadafi kawekeza kwenye Mladi wa kumchafua Lowasa kwa gharama yeyote ile , membe yupo tayari kufirisika ili mladi ahakikishe Lowasa hapati Urais , hivyo Lowasa ajiandae na vita ya mtandaoni ambayo membe yupo busy akibuni mbinu za hapa na pale.
 
Tambua Kuwa Membe kazimega zile Pesa za Marehemu Gadafi kawekeza kwenye Mladi wa kumchafua Lowasa kwa gharama yeyote ile , membe yupo tayari kufirisika ili mladi ahakikishe Lowasa hapati Urais , hivyo Lowasa ajiandae na vita ya mtandaoni ambayo membe yupo busy akibuni mbinu za hapa na pale.
Mbona Lowasa na Membe ni walewale tu? Au mmesahau! Mmoja ni pacemaker tu hapo ili kuwachosha wapya wanaouwania Urais wetu.
 
Mngeweka hiyo picha gazetini halafu mngeacha wasomaji waamue kama ni kampeni ya 2015 au la.
 
tatizo ya nchi zinazoendelea hatuwazi mbadala.....kana kwamba bila EL Hakuna TZ
 
Huyu bwana ameiharibu tasnia ya habari. Kwa sababu ya uroho wake na kutojiamini amewanunua karibu wahariri wote. Pc kubwa ya waandishi 'matajiri' ni 'wake' wa Ngoyai! Lowasa ni dude la kuogopwa kama ukoma hafai!
 
Mleta mada nasikitika kwa kuwa na wewe hujasema umepewa shilingi ngapi na huyo mwanaharamu mwenzio ili uje kuandika huu uharo hapa jf
 
Back
Top Bottom