Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 52,171
- 162,618
Waziri mkuu ajiejiuzulu na ambae anawania kuteuliwa kuwa mgombea uraisi kupitia CCM amesema mtu masikini hafai kuwa raisi na amehoji itakuwaje mtu masikini aongoze wananchi masikini?
Pia,amesema yeye hana njaa ila mwenyezi mungu amemjalia uwezo mdogo hivyo hatafuti kwenda Ikulu kwasababu ana shida ila anataka akapambane na umasikini
.==========================
Pia,amesema yeye hana njaa ila mwenyezi mungu amemjalia uwezo mdogo hivyo hatafuti kwenda Ikulu kwasababu ana shida ila anataka akapambane na umasikini
.==========================
Chanzo: Habari leoMGOMBEA anayewania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu, Edward Lowassa jana alifanikiwa kupata wanachama 22,750 wa kumdhamini mkoani Singida na kusisitiza anaomba kwenda Ikulu ili amalize umasikini unaowakabili Watanzania, huku akisema Watanzania wasichague kiongozi masikini.
Alisema idadi hiyo kubwa imevunja rekodi ya wanachama waliomdhamini hadi sasa kwenye mikoa 15 ambayo amepita kuomba udhamini kwa ajili ya nafasi hiyo.
Alisema mapokezi makubwa aliyopata pia ni dalili nzuri kuelekea kwenye safari yake ya matumaini."Umati huu mkubwa unanitia faraja kwani ndio mtaji wa wanasiasa.
Kama ni mchezo wa mpira ningehesabu nimefunga goli," alisema Lowassa huku akishangiliwa. "Na kwa wale walionidhamini nawaambia kuwa Imani huzaa imani nami naahidi sitowaangusha kwenye safari yangu hii ya matumaini."
Mgombea huyo ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu aliendelea kusisitiza kuwa anachukia umasikini na kamwe endapo atapewa ridhaa na Chama chake kugombea nafasi ya Urais na kuingia Ikulu atahakikisha umasikini unakuwa historia katika nchi hii kwa kuongeza ajira kwa vijana.
Alisema Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi sana hivyo watu wake hawapaswi kuwa masikini. "Nikiingia Ikulu nitaendesha nchi kwa mchakamchaka....siombi nafasi hii kwenda Ikulu tu, Ikulu mimi napafahamu," alisema na kuongeza;. "...Wala sina njaa, Mwenyezi Mungu amenijalia kuwa nacho kidogo kwa hiyo siendi pale Ikulu kujitafutia bali ni kwenda kupambana ili wananchi waondokane na umasikini….
umasikini umekithiri, nami nauchukia sana umasikini," alisema Lowassa na kusisitiza kuwa, kiongozi masikini hafai kuingia Ikulu kwani hatakuwa na jipya.
"Nashangazwa na baadhi ya wagombea wanaojinadi kuwa eti wanaweza kuongoza nchi kwa kuwa wao wanatoka kwenye familia masikini. Kiongozi anayesujudu umasikini msimchague," alisema na kuongeza; "...Nchi hii inakabiliwa na changamoto nyingi; sasa kama kiongozi naye atakuwa masikini atawaongozaje watu masikini?" Alihoji Lowassa.