Lowassa kuzungumza na Taifa Jumapili hii

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
WIKI moja baada ya kuwa gumzo kuu katika mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu ambaye aligombea urais katika uchaguzi mkuu mwaka jana, Jumapili 31 Julai 2016 saa 3.00 asubuhi atafunguka juu ya mengi yanayosemwa juu yake.

Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mwanasiasa maarufu zaidi nchini kwa sasa atazungumza kupitia kipindi cha “Funguka” kinachoendeshwa na mwandishi wa habari nguli Tiddo Mhando kupitia kituo cha televisheni cha Azam 2.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Azam 2 inasema “Lowassa atafafanua na kueleza mengi kuhusu maisha yake marefu kisiasa

Aidha, Lowassa ambaye aligombea urais kwa tiketi ya Chadema, huku akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) amekuwa kimya kwa muda mrefu licha ya kuzungumzwa, kuandikwa kuelezwa na kutendewa mengi yanayomhusu bila yeye binafsi kujitokeza hadharani na kujibu.

Gumzo la Lowassa ndani ya mkutano mkuu wa CCM lililoenda sambamba na baadhi ya viongozi na wazungumzaji kumshambulia wazi wazi huku wakishidwa kujadili kwa kina mambo yanayohusu chama, linatajwa kuwa ni hofu ya CCM dhidi ya Lowassa.

Hayo yatajiri ikiwa ni siku tatu tangu aadhimishe mwaka mmoja tangu kuhama CCM na kuwataka wanaomuunga mkono wakiwa CCM waendelee kumpa siri za mambo yanayojiri CCM ikiwemo mikakati ya Rais Magufuli.
 
Watanzania wengi watakuwa wanamsubiri kwa hamu kubwa sana kumsikia Mhe.Edward Lowasa akiongea na watanzania kupitia kituo cha TV Azamu 2 kuanzia saa tatu asubuhi asante sana kwa taarifa mkuu Molemo
 
WIKI moja baada ya kuwa gumzo kuu katika mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu ambaye aligombea urais katika uchaguzi mkuu mwaka jana, Jumapili 31 Julai 2016 saa 3.00 asubuhi atafunguka juu ya mengi yanayosemwa juu yake.

Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mwanasiasa maarufu zaidi nchini kwa sasa atazungumza kupitia kipindi cha “Funguka” kinachoendeshwa na mwandishi wa habari nguli Tiddo Mhando kupitia kituo cha televisheni cha Azam 2.

Katika taarifa iliyotolewa leo na Azam 2 inasema “Lowassa atafafanua na kueleza mengi kuhusu maisha yake marefu kisiasa

Aidha, Lowassa ambaye aligombea urais kwa tiketi ya Chadema, huku akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) amekuwa kimya kwa muda mrefu licha ya kuzungumzwa, kuandikwa kuelezwa na kutendewa mengi yanayomhusu bila yeye binafsi kujitokeza hadharani na kujibu.

Gumzo la Lowassa ndani ya mkutano mkuu wa CCM lililoenda sambamba na baadhi ya viongozi na wazungumzaji kumshambulia wazi wazi huku wakishidwa kujadili kwa kina mambo yanayohusu chama, linatajwa kuwa ni hofu ya CCM dhidi ya Lowassa.

Hayo yatajiri ikiwa ni siku tatu tangu aadhimishe mwaka mmoja tangu kuhama CCM na kuwataka wanaomuunga mkono wakiwa CCM waendelee kumpa siri za mambo yanayojiri CCM ikiwemo mikakati ya Rais Magufuli.

Who Cares?
 
Lowasa anazungumza na Taifa ama anazungumza na Tido Mhando kupitia Azam Two? Acheni kujitowa ufahamu, Lowasa hana wadhifa wowote kiasi cha kusema anaongea/anahutubia taifa, yeye na Dovutwa au Hashim Rungwe ni sawa sawa.
Atazungumza na taifa kupitia kituo cha TV Azam 2
 
Nina hofu na frequencies za Azam 2 siku hiyo. Pia dharura ya umeme inatarajiwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom