Lowassa kuzunguka nchi nzima kuanzia kesho

Lowassa kuzunguka nchi nzima kuanzia kesho

Mtegowanoti

Member
Joined
Oct 25, 2015
Posts
36
Reaction score
27
Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa ataanza ziara ya kuzunguka nchi nzima kuwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 na kesho atakuwa Tanga.

Katika ziara hiyo, Lowassa ataambatana na viongozi waandamizi wa Chadema na Ukawa kuwashukuru wananchi kwa namna walivyounga mkono upinzani na ajenda nzima ya mabadiliko katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene imesema kiongozi huyo atatoa shukrani zake kwa wananchi kwa jinsi wanavyoendelea kuweka matumaini yao kwa upinzani.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba wananchi bado wanaamini kwamba upinzani ndiyo nguzo imara wanayoitegemea katika kuwaletea mabadiliko ya kweli kwa ajili ya maendeleo yao na ustawi wa Taifa kwa ujumla.

"Wananchi wanastahili shukrani kwa imani hiyo kubwa ambayo ni ishara ya wazi kuwa matumaini yao kwa miaka mingine mitano yatasimamiwa na kuongozwa na upinzani imara kupitia Ukawa," alisema Makene katika taarifa hiyo.

Alisema mbali na kupiga kura nyingi katika nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu uliopita, wananchi waliwachagua wabunge wengi wa upinzani wanaotokana na Ukawa. Alisema wabunge hao wameongeza nguvu kubwa ndani ya Bunge hususan kupitia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambayo itakuwa serikali mbadala.

Pia, alisema wananchi wameviamini vyama vya upinzani ili kusimamia na kuongoza halmashauri 34 nchi nzima, ikiwa moja ya misingi imara katika kupigania mabadiliko ambayo Watanzania wanayataka.

Chanzo:
Mwananchi
 
Ili tujue magufuli ni jembe akianzisha mahakama ya mafisadi aanze na first of shame ndg laigwanani lowasa asipompeleka mahakamani basi lowasa ni mtu safi
 
hizo pesa za kuzunguka nchi nzima naamuru zielekezwe kuchimba visima kule Monduli, wananchi wanachangia maji na Ng'ombe kwenye mito.
 
Ili tujue magufuli ni jembe akianzisha mahakama ya mafisadi aanze na first of shame ndg laigwanani lowasa asipompeleka mahakamani basi lowasa ni mtu safi

Lowassa mwenyewe kishajifia, mnataka Magufuli awe sababu ya kifo chake? basi subirini Tingatinga, nalo haliogopi
 
ndani ya mioyo yenye kula rushwa.

Asisahau kuwaambie kile kinyago kilichochongwa na cc ya ccm kimejaribu kuwatisha lakini wameshakidhibiti. Hivyo mabadiliko ni mpaka 2020.
 
Bc ukweli ni kwamba magufuli hana ubavu wa kupeleka mapapa kwenye mahakama ya mafisadi atapeleka vidagaa tu
 
Pamoja na mambo mengi yanayozungumzwa dhidi yake na yasiyo na ushaidi

nadiriki kusema kwamba lowassa ni mfano wa kuigwa tanzania na duniani kote

1.ana hekima

2.ana busara

3.ana maono

4.ni mtu mtaratibu sana lakini mwenye mipango ya kuona mbali

5.baba mwenye familia inayojiheshimu sana,mfano mzuri ni kwenye kampeni,pamoja na matusi yote yale si yeye wala familia yake imewahi kujibu mapigo

6.anao uwezo na mwenye uthubutu

7.zaidi na zaidi ni mtulivu wa fikra

my take:naunga mkono kuzunguka mikoani kuwashukuru wananchi,kura miliono 6 si haba

watanzania wenzangu,especially wanajf:yapo mengi ya kujifunza toka kwa huyu mzee lowassa
 
kwa nini hizo hela asisaidie wamasai wenzake kule monduli wanaoishi kwenye dhiki iliyokithiri ambao wamempa heshima ya kuwa kiongozi wao karibu robo karne?
by the way kama hatasikia huu ushauri huko kuzunguka kwake atatumia chopa tena au gari? au meli? treni? bodaboda, baiskeli, bajaji ......
 
nakubaliana kabisa na wewe katika andishi lako lakini umesahu moja tu. kuwa mzee kwa madili yote yanayohusu hela sio haba! hili liwe namba 8.

Pamoja na mambo mengi yanayozungumzwa dhidi yake na yasiyo na ushaidi

nadiriki kusema kwamba lowassa ni mfano wa kuigwa tanzania na duniani kote

1.ana hekima

2.ana busara

3.ana maono

4.ni mtu mtaratibu sana lakini mwenye mipango ya kuona mbali

5.baba mwenye familia inayojiheshimu sana,mfano mzuri ni kwenye kampeni,pamoja na matusi yote yale si yeye wala familia yake imewahi kujibu mapigo

6.anao uwezo na mwenye uthubutu

7.zaidi na zaidi ni mtulivu wa fikra

my take:naunga mkono kuzunguka mikoani kuwashukuru wananchi,kura miliono 6 si haba

watanzania wenzangu,especially wanajf:yapo mengi ya kujifunza toka kwa huyu mzee lowassa
 
Gharama za hiyo safari zinatoka wapi atatumia fedha zake au ruzuku ya CHADEMA?au marafiki zake kina Rostam,Karamagi na Bashil mwizi wa Stanbic watamchangia?

nafikiri atakuwa na Sumaye yeye akihutubia dakika 2 kama kawaida yake,Sumaye amsaidie dakika 30.
 
hizo pesa za kuzunguka nchi nzima naamuru zielekezwe kuchimba visima kule Monduli, wananchi wanachangia maji na Ng'ombe kwenye mito.

Hii si inaitwa serikali ya Magufuli? Kwanini mnakimbia majukumu yenu mmekwishashindwa majukumu ndani ya mwezi mmoja tu. Maana mmeanza kuwapangia hadi ada shule binfsi wakati mmesema serikalini bure, boresheni shule za umma wananchi hawatakwenda shule binafsi na si kuwapangia ada maana wakishusha ada itawagharimu wafanyakazi wengi sana, watapunguzwa kazi sdana. Tekelezeni majukumu yenu na si kumsakazia Lowassa. Serikali hii ni ya CCM
 
Pamoja na mambo mengi yanayozungumzwa dhidi yake na yasiyo na ushaidi

nadiriki kusema kwamba lowassa ni mfano wa kuigwa tanzania na duniani kote

1.ana hekima

2.ana busara

3.ana maono

4.ni mtu mtaratibu sana lakini mwenye mipango ya kuona mbali

5.baba mwenye familia inayojiheshimu sana,mfano mzuri ni kwenye kampeni,pamoja na matusi yote yale si yeye wala familia yake imewahi kujibu mapigo

6.anao uwezo na mwenye uthubutu

7.zaidi na zaidi ni mtulivu wa fikra

my take:naunga mkono kuzunguka mikoani kuwashukuru wananchi,kura miliono 6 si haba

watanzania wenzangu,especially wanajf:yapo mengi ya kujifunza toka kwa huyu mzee lowassa

Umesema vyema mkuu...

Lowassa ni mtu makini sana....

vipi ratiba ya kanda ya ziwa ikoje? Mara ni lini atakuja. Tunamsubiri kwa ham tele
 
Back
Top Bottom