Lowassa kutumia sh bilioni 70 kujenga gorofa 25 Dar City Centre!


Anayetoa taarifa dira Isije ikawa alipataka halafu kazidiwa...Ningewaelewa Dira kama wangetuambia na mchakato mzima wakupatikana hilo eneo..inawezekana kapata katika njia halali kabisa...na kuhusu suala katoa wapi Bil 70/= nadhani suala la financing kwenye mabenki au joint venture ni very possible..lets not discuss something on the face lete kitu detailed ili tu analyze sio cut and paste with your biased comments
 

Watanzania tunamalizana wenyewe tunawaachia wageni wantamba kwenye uchumi...........that is being hypocrtic at the highest level.....chukulia mfano Pale kuna Invester anajenga uhuru peak ...ghorofa 30...wale jamaa walikuja hapa wakaaza kununua pamba ....kwa kukopeshwa na benki ...wakajenga maviwanda ..sasa wamepata mkopo nje na ndani na pesa zao wanajenga lile ghrofa refu kuliko yote tz.......so kwa kuwa ni wahindi ...no body cares....
wengine wamekuja wakimbizi toka somalia ...tumewapa mitaji haapa hapa ...wameinuka..,tatizo pesa akiishika mbantu ..kila mtu ana haha....tuacheni utumwa wa fikra!!!!.......naamini kabisa kwa mradi wa size ya nyumba ya sanaa na kwa dunia ya leo ..yenye intergrated actions against ufisadi lazima ni mkopo...tu!!!...na kama ni mkopo sioni ajabu!!!!

kwenye nchi za wenzetu you can own any asset you want kupitia mkopo ..ili mradi uwe na defined repayment strategies and plans!!
 

Nashukuru kwa elimu nzuri uliyotoa!vipi pale kwako kuna mikopo mikubwa kama hii?Nakuaminia mzee wa BAF!!!
 

Bongolander,

Ni sawa kuna sheria lakini sio rahisi kuwashitaki hao wakubwa wanaomiliki magazeti yanayoongoza kwa kuchafua watu. Labda kama unaongelea watu kama Lowassa tu. Lakini pia na yeye ni mwanasiasa na kwa wanasiasa hakuna kosa kubwa kama kwenda mahakamani hata kama haki iko kwako.

Imagine ni wewe umechafuliwa, ukiamua kulipeleka gazeti la Mengi mahakamani, jiandae kupoteza muda wako, pesa zako na mwishoni si ajabu kushindwa case on technicalities. Ndio maana watu wengi wanaamua kuachana na hayo magazeti na kuendelea na maisha yao.

Leo tunaweza kushangilia kwasababu yanamhusu mtu mwingine, lakini wakati wote ni bora kununua insurance wakati huihitaji. Haya magazeti hayana maadili kabisa. Mhariri anatumwa na wenye pesa kwenda kuchafua wengine na anafanya hivyo bila hata aibu. Hiyo fani imevamiwa na watu wa ajabu kweli kweli.
 

Please kama kitu hujui kaa kimya..umengangania suala la kukopa nani kakuambia kakopa????? inawezekana thamani ya eneo ndio shares zake...please uliza kabla hujaandika upupu humu..mnachosha na umbea
 

Tatizo la "great thinkers" wengine humu ndani ni mafundi sana wa kujaribu kupotosha hoja za msingi. Sote tunajua Membe na Lowassa zamani walikuwa ni maswahiba wakubwa baadae wakakosana. Wenyewe wanajua sababu za kukosana kwao, ila zinapoibuka tuhuma zozote zile kuhusu Lowassa na kusema eti zimeanzishwa na Membe ni jambo la kitoto hilo. Tupime kila hoja/tuhuma kwa uzito wake.

Ni dhahiri kuwa ni kweli huenda Lowassa amekopa hizo shilingi bilioni 70 kujenga hilo gorofa ila ukweli unabaki palepale, benki hawawezi kukukopesha kwa kuangalia makaratasi tu. Lazima wacheki cash flow yako, bank statement na track record yako kuhakikisha kuwa wewe mwenyewe una mabilioni benki ndiyo wakupe hizo $45.5 million.

Swali la msingi liko palepale, Lowassa ambaye maisha yake yote amekuwa ni kiongozi wa umma, ametoa wapi utajiri wake huu wa kutisha? Je, yeye ni mwekezaji au ni kiongozi wa umma? Kwa nini serikali haichunguzi chanzo cha utajri wake ambao hata Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kuuhoji?
 
Njilembera, we have a problem somewhere, kuna watu wangependa kuwaona viongozi wastaafu wa seriakuli wakifuga ngombe wawili au watatu wa maziwa.

Amini usiamini, kama huyo developer angekuwa Patel, wala usinge sikia kelele yoyote, lakini kwa vile ni jina la kibantu tena alikuwa PM wetu, basi imekuwa issue kubwa!.

Watu wanapiga kelele sana, huku hakuna anayejua financier ni nani, developer kazi yake kudevelop, pesa amekopa benki kwa makubaliano maalum, hivyo sioni tatizo liko wapi.

Kauli yangu ni ile ile siku zote, mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!.
 
sa sijui ndo mjue JF imeingiliwa.
 

Nimekugusa eh?

.....miradi kama ile benki wanabaki na ownership hadi mkopo uishe na ni lazima uwe na insurance...ya ku cover hili jengo.....
wanatoa pesa ,wanazidhibiti ...jengo likiwa tayari wanafuata business plan yako....wanaweka property manager ...kila senti inapitia kwa wanalamba percent yao ...unapewa yako kulingana na mkataba.....mkopo ukiisha unarushiwa hati...[ownership]....

Mimi binafsi ninayo project kama hiyo ya milion..1$......na hutaamini zaidi ya kuwa na prime plot sina pesa ...na ndio condition niliyopewa ...nikope against mali...na karibu nitapata..ila as i said ma contractor wote wanalipwa na benki..hawakupi pesa ...wanaogopa uta divert project.
 
Lowassaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaanafurahisha sana huyu fisadi.
 
mkuu unaloongea ni kweli nakuunga mkono ni bora fisadi anaye wekeza nchini kuliko anayewekeza kwenye visiwa na kuendeleza nchi zingine! Lowasa we tumia pesa zako za wizi hapahapa nchini!
 
Nashukuru kwa elimu nzuri uliyotoa!vipi pale kwako kuna mikopo mikubwa kama hii?Nakuaminia mzee wa BAF!!!

Excuse me ..what is BAF??

Mimi sitoi mikopo...ila nakopa..mzee...naishi kwa kukopa na kulipa,.....ila kwa kukusaidia ni vigumu kupata a single bank tanzania wakakupa..ndioo maana nikaongelea kuwa kwa mkopo mkubwa wa hivi kwa huzi local bank ..una discuss na bank kama tatu hivi wanakupa kitu kinaitwa syndicate loan...wenyewe wanakubaliana..ILA pia nimekueleza kuwa mikopo ya size hii hutolewa kirahisi na kwa terms nzuri na oversea investments banks....or finace institutions....kwani intrest rate ya local banks ni kubwa mno kuweza kumpa faida mwekezaji wa jengo la $45........
 
Wanaomtetea Lowasa ni walewale wasioionea huruma jamii ya kitanzania inayoteseka kutokana na maamuzi mabovu ya watedaji wa serikali.

Tukubali kwamba KIKWETE anahusika ktk hili ndo maana pamoja na taarifa alizofikishiwa na wasanii ameamua kuwapuuza.

Hivi huyu Lowasa analindwa na nani???
 
Yero subai jenga utupe ajira maana huku mtaani hapafai. Wajinga ndo waliwao
 

Jamani hata kama anajenga msikiti ama kanisa, suala hapa je, ni halali, maana viongozi wetu hawana huo utajiri halali wa kuwekeza, Mkapa alifanya jambo jema kununua Kiwira lakini mazingira yalikua na kila aina ya utata. Tusiwe vipofu na kuwa kama watoto wa kijiweni mtu akiuza madawa ya kulevya anasifiwa kuw ani mjanja na amefanya vyema, jambazi akiiba na kuwa tajiri anaitwa 'mjanja' na mfano wa kuigwa hali kadhalika fisadi. Jamani tufumbue macho. Hata huyo Manji ana vitega uchumi kibao nchini pamoja na kupeleka nje, Rostam naye ana vitega uchumi kibao nchini, tusiwasema sababu ni weupe na kumtetea Lowassa sababu ni mweusi. Wizi hauna rangi, dini wala kabila jamani.
 

Wasanii anao wajua yeye ni wale waliompigia kampeni sio hawa wa SINDIMBA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…