Lowassa kumzuia Serukamba Ubunge

Lowassa kumzuia Serukamba Ubunge

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,367
Reaction score
27,773
WAZIRI Mkuu mstaafu Edward Lowassa amesema huenda akamzuia Mbunge wa Jimbo la Kigoma, Peter Serukamba kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu ili amsaidie jukumu muhimu kwenye safari yake ya matumaini.

Akizungumza wakati wa kuomba udhamini kutoka kwa wanachama wa CCM mkoa Kigoma katika ofisi kuu ya CCM mkoa, Lowassa alisema Serukamba ni mmoja wa wanakamati katika safari hiyo ya matumaini.

Lowassa, anayewania kuteuliwa kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM alisema katika safari hiyo kama mwanakamati Serukamba anayo majukumu muhimu ambayo anapaswa ayatekeleze zaidi ya kugombea ubunge."Ndugu zangu wananchi wa Kigoma nimekumbuka jambo moja ninaye mwana kamati ambaye ni mtoto wenu hapa Kigoma, Mbunge wenu Serukamba, yeye ni mmoja wa wajumbe katika kamati yangu alikuwa na dhamira ya kugombea tena ubunge, lakini mnaweza msimuone maana atakuwa na majukumu makubwa ya kunisaidia kwenye kamati," alisema Lowassa.

Pamoja na kutogombea ubunge kiongozi huyo alisema Serukamba anayo dhamira ya dhati katika kuwatumikia wananchi wa mkoa Kigoma na ili kutimiza lengo hilo ameomba wasali na kumuombea sana ili aweze kupitishwa na chama chake kugombea Urais, lakini pia kushinda katika uchaguzi mkuu.

Serukamba ambaye kwa sasa anamaliza muhula wake kama Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini anatarajia kugombea tena ubunge katika jimbo la Kigoma Kaskazini.

Chanzo: Habari Leo
 
Lowassa hana kipaji cha uongozi ila anakipaji cha uongo.

Uwezo wake ni kuongoza ng'ombe sio watu.

Lowassa ni jipu, ukitumbua vibaya utachafuka wewe, linahitaji timing sana
 
Jamaa ameanza kushtuka kwa upinzani mkubwa atakaopata Serukamba kwa michezo watatu hao wanayocheza. ZZK, Serukamba na EL. Mtakuja kuyaona haya maana anaogopa tu kusema hata ZZK ni mwanakamati na walishakaa wakakubaliana na ZZK kuhusu mchezo huo mchafu. Hapa napata wasiwasi kuamini watu wa Kigoma zaidi kwa usaliti
 
Ili litimie lile neno kua ACT ni ya EL
 
matayarisho ya kugawa vyeo kama njugu hasa kwa wanamtandaí yameanza...
 
Mtaka yote kwa pipa huskosa yote kwa pupa subiri wakati ufike watalia sana.

CCM wakimpitisha Lowasa kama ndio mgombea wao, mi ntasubiri majukwaani tu kwenye kampeni.
Watamnadi vipi?watamsafisha Kwa njia ipi?, maana wenyewe ndio walisema yeye mchafu (Fisadi). Sasa nasubiri kuona kama atapitishwa na CCM, njia ipi itatumiwa kuwaambia wananchi (kumsafisha) kuhusu yeye.
Na akipitishwa na CCM, basi hapana Shaka CCM itakuwa imefanya dharau kubwa kwa wananchi wake.
Maana wenyewe walisema hafai, baadae wanakuja kuwaambia wananchi wao kuwa anafaa na kutaka kumpa nchi aongoze, BONGE LA DHARAU HILO. Na akipitishwa na CCM, halafu wananchi wakamchagua kushika madaraka, basi patakuwa hapana shaka yoyote tukiingizwa kwenye GUINESS BOOK.
Maana kitachotokea Tanzania, kwa nchi zilizo makini na wanachokifanya hakiwezi kutokea kamwe.
 
umetumwaa ee aliyekuambia lowasa fisadi ni nani.uliona escrow ili mtaja waziri mkuu na nani?
 
Je mnakumbuka ZZK anampango wa kugonbea Kg mjini kuna dalili kuwa ACT ni ya mzee?
 
CCM wakimpitisha Lowasa kama ndio mgombea wao, mi ntasubiri majukwaani tu kwenye kampeni.
Watamnadi vipi?watamsafisha Kwa njia ipi?, maana wenyewe ndio walisema yeye mchafu (Fisadi). Sasa nasubiri kuona kama atapitishwa na CCM, njia ipi itatumiwa kuwaambia wananchi (kumsafisha) kuhusu yeye.
Na akipitishwa na CCM, basi hapana Shaka CCM itakuwa imefanya dharau kubwa kwa wananchi wake.
Maana wenyewe walisema hafai, baadae wanakuja kuwaambia wananchi wao kuwa anafaa na kutaka kumpa nchi aongoze, BONGE LA DHARAU HILO. Na akipitishwa na CCM, halafu wananchi wakamchagua kushika madaraka, basi patakuwa hapana shaka yoyote tukiingizwa kwenye GUINESS BOOK.
Maana kitachotokea Tanzania, kwa nchi zilizo makini na wanachokifanya hakiwezi kutokea kamwe.

Hakuna kitu kibaya Kama kutoka kundi la wasionamatumaini. Hata mbinguni ni safari ya matumaini. Ole wao wasiyonamatumaini maana kilichobaki kwao ni kufanya kila hila waifupishe safari za wengine!

Lowassa haitaji kusafishwa kwa uchafu UPI alionao? Mapokezi anayoyapata mikoani ni tosha kuonyesha Watanzania wana Imani naye. Wengine wangetamani kupata hayo mapokezi lakini yanashindikana. Hapo ndipo tumetofautiana karama!
 
utaendelea kusubiri hivyo hivyo wenzako wakifanya yao.
 
Hakuna kitu kibaya Kama kutoka kundi la wasionamatumaini. Hata mbinguni ni safari ya matumaini. Ole wao wasiyonamatumaini maana kilichobaki kwao ni kufanya kila hila waifupishe safari za wengine!

Lowassa haitaji kusafishwa kwa uchafu UPI alionao? Mapokezi anayoyapata mikoani ni tosha kuonyesha Watanzania wana Imani naye. Wengine wangetamani kupata hayo mapokezi lakini yanashindikana. Hapo ndipo tumetofautiana karama!

Unamaanisha yale mapokezi ya kununua au?
 
lowassa ni mwanasiasa by nature anachokifanya ni political manuva! hapa kwa political scientist wananielewa and its allowed any where for seeking legitimacy and acceptability of the majority!
 
EL akipata urais atamteua Serukamba kuwa mbunge, halafu atamteua kuwa waziri wa uchukuzi.

EL akikosa urais atamuombea kazi ya uhasibu Serukamba kwenye kampuni ya Caspian.
 
Kwa hiyo ameshajiaminisha asilimia miamoja kuwa tayari kawa rais wa Tanzania,kuna hatari watu wakaja kupoteza maisha hapa watakapo kuja kupata matokeo kinyume na yale waliyotegemea.

Mrema nae ilikuwa hivihivi lakini mpaka sasa urais ana usikia kwa wenzake tu.
 
Back
Top Bottom