Lowassa: Kuitwa gamba, fisadi kuliniondoa CCM

Lowassa: Kuitwa gamba, fisadi kuliniondoa CCM

na sasa anaugua 'upungufu wa madaraka mwilini' naona kanywa dawa za maumivu (kura milioni kadhaa) kapata nafuu namuona yuko fiti mungu ampe nguvu
 
KilichomwondoA CCM sio kuitwa gamba.Aliitwa Gamba sana tu akiwa CCM hakuondoka.Kilichomwondoa CCM ni baada ya Jina lake Kukwatwa asiwe mgombea Uraisi CCM.Mzee Lowasa kweli anapoteza kumbukumbu.Akawadanganye CHADEMA.PANGA LA KUMKATA LILIPOPITA NDIO AKATIMKA MKUKU KUKIMBILIA CHADEMA.Lowasa wanasema hawezi kukimbia hana mbio lakini lilipokatwa jina CCM mbio alizokimbia kwenda CHADEMA sijawahi ona.Angeweza pata hata medali ya OLYIMPIC

You are right. Huyo ni gamba kweli kweli hata Chadema walipiga pesa tu na wala hawakutaka awe rais. Hivi karibuni hiyo mahakama ya mafisadi ikianza kumshughulikia Mbowe naye atamtosa ili chama kirudishe hadhi na miiko yake.
 
Haiingii akilini hata kidogo,atakayemwamini inabidi apimwe akili.ukiangalia kwa makini Chadema ndio walikuwa WAASISI wa kumsema vibaya na ndio wamemsema vibaya zaidi ya CCM na kwa muda mrefu.

Iweje sasa atoke CCM na kukimbilia huko huko ambako ndiko waliasisi na kuongoza kumchafua(tena hata bila kumuomba radhi!)halafu aseme ametoka kwa kuwa ameitwa gamba na fisadi na CCM?Au kuitwa fisadi na CHADEMA ni sahihi lakini kuitwa na CCM ndio makosa?na je kwanini asingetoka mapema badala yake akasubiri mpaka WALIPOMFYEKA kule Dodoma?

Kwenye hili maswali ni mengi kuliko majibu.
Marehe mtikila sasa maneno yake naanza kuyaamini huyu mzee anaugonjwa wa akili sasa umemtuma kuota urasi ndipo nafuu kwake inapokuja
 
manyumbu tu ndo watakaoamini hizo sababu,ukweli ni kwamba aliondoka baada ya kukatwa jina
 
Roho yake iko ccm ila kimwili yuko chadema kuisaka Ikulu
 
Yaani nyie watu msio elewa wa ccm,tutafutane baada ya miaka mitatu.ni heri hata mngemlasimishaga membe.
 
Naona viongozi wote wa vyama vya CUF na CDM taifa wakienda kkolokoloni kwa kuratibu ugaidi Zanzibar na bara kwa kulazimisha kutaka kutawala nchi.

My take: jiepusheni na suala hili kwani linawapeleka pabaya siku si nyingi.

Ref: Kauli ya Lowasa Jana mgogoro wa uchaguzu Zanzibar unakaribisha magaidi.
 
natamani katika ule mkutano angekuwepo yule mwandishi wa BBC Zahra Yunus kwani angemuumbua kwa maswali ya data mpaka angeahirisha mkutano.Waandishi wa Tanzania ni vilaza wa kutupwa hivi hakuna anayejua kilichomtoa Lowasa CCm au zile senti wanazopewa ndio zinawafanya kuandika huo upotoshaji, wangemuuliza kauli yake aliyoitoa Arusha wakati wakutangaza nia kuwa yeye angekuwa wa mwisho kuondoka ccm na wanaotaka aondoke watangulie wamwulize wakati anatoa ile kauli alikuwa ameishaitwa gamba au fisadi na ccm pia wamwulize kwenye ile list ya shame iliyotangazwa na chadema kama ilitoka kabla au baada ya ccm kujitangaza kujivua gamba pia wangemwuliza neno mafisadi limeanzia ccm au chadema nashangaa gazeti kama mwananchi linavyoandika unafiki
 
Alivumilia mpaka mwisho ili acheze kete yake ya mwisho yani Urais,support alikuwa nayo ya kutosha ss CC ilipomchinja bila kutarajia bac ikawa hamna namna tena zaidi ya kusepa
 
Ndo siasa hiyo mjomba huwezi kutishia kuondoka wkt unagombania nafasi nyeti kama hiyo utawavunja moyo hata supporter,so ilikuwa ni kauli ya kuwapa ari supportes ndani ya CCM ..
 
ki msingi edo nimejua kweli anataaluma ya usanii, tena kwa kiwango cha masters, ila tatzo usanii haumlipi maana anaufanyia kwenye siasa, mangekuwa kaole sanaa group, au kule kwingine angeweza

nmkumbushe tu kuwa ingekuwa nchi kama china sa iv edo asingekuwa habari, ila huku mgombea, tatzo kubwa anajifanya kuwa hana akili wakati anazo,

yy ni FISADI FISADI FISADI, na hlo halibadiliki mpka mwisho ila akitaka alisafishe akili na kisha atudishe pesa hapo msamaha amepata,

hakutoka ccm kwa kuitwa gamba, ila aibu, na kukatwa jina...
 
Na ule mpango wa kwenda monduli kuchunga mifugo yake umeishia wapi

😛😛😀😀😀ana assistant wake kamwachia hiyo kazi ya kuchunga mbeeee..wakati yy huku anaendelea kula bata kwenda mbele
 
mzee kahamia sehemu ambayo hajawahi itwa fisadi, ha ha ha rais wa nje ya ikulu bana...
 
Mzee Edo anaanza kuwa genious sasa, na washindwe wote wanaochelewa kumuelewa.

Anachomaanisha Mzee wetu ni kuwa kelele zilikuwa kona zote ila zile za ndani ya chama chake zilikuwa zikimaanisha na kutisha zaidi, tofauti na nyumba ya pili (Chadomo) ambapo kila alipokuwa akiwaangalia usoni hakupata shida kuelewa kuwa hawamaanishi bali ni njaa tu inawauma.

Akatibu njaa yao, sasa hivi anaishi raha mustarehe.
 
Lowasa ni MTU saaafi sana siyo kama Vasco,mzinz na mpiga dili Wa. M...so...ga
 
Back
Top Bottom