Lowassa: Kuitwa gamba, fisadi kuliniondoa CCM

Lowassa: Kuitwa gamba, fisadi kuliniondoa CCM

Magamba povu linawatoka ile mbaya! Kwani ni uongo hawakutumwa watu kumtukana Lowassa?
Povu lenyewe hili hapa. Lowassa anatafuta pa kutokea. Mwambie kwa sasa watu walitaka kumsahau na asijitokeze kutukumbusha kabisa.
 
Bora angesema " kitendo cha CCM kumkata kilimuumiza sana! kilimdhalilisha sana! alionewa sana! alidhihakiwa sana!. Hivi huyo mzee anadhani watanzania hawana akili? Ila CCM imejiletea uhai kumkata huyo babu!
 
Mzee wangu Lowassa waswahili wanasema "ukiwa mwongo uwe na kumbukumbu". CHADEMA wamekuita fisadi kwa miaka 8, leo uko wapi? Uko kwenye record mzee wangu ukisema kuwa CCM is your life, na asiyetaka ahame, lakini leo uko wapi?
 
Huyu fisadi Lowassa kumbe ana tatizo kubwa zaidi hata ya nilivyokuwa nikifikiria!

CHADEMA wana kazi ya ziada kukaa na mtu aina ya Lowassa kwenye chama chao.

Sikutegemea kama Lowassa angeshindwa kueleza ukweli wa nini hasa kilichomtoa CCM...Sikutegemea hata ujasili huu mdogo tu HANA!
 
Yaani alijua anauza sura kwenye gazeti kumbe anachafuka zaidi...

Toka 2008 anaitwa fisadi na Chadema 2015 amefurushwa CCM halafu 2016 unasingizia wanaCCM kukuita fisadi....

Mungu anampiga upofu wa fikra na kumbukumbu huyu mzee
 
Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema chini ya mwavuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amesema kusakamwa kwa maneno ya kejeli, vijembe na vitisho, kuitwa gamba na fisadi ndani ya CCM ndiko kulikomfanya kukihama chama hicho na kwenda upinzani.

Lowassa aliyekuwa na nguvu ya ushawishi ndani na nje ya CCM, alihamia Chadema baada ya jina lake kukatwa katika mchakato wa kumsaka Rais wa Tanzania, katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.

Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Lowassa alisema licha ya kuitumikia CCM kwa zaidi ya miaka 30 tangu mwaka 1977, chama hicho kiliamua kutumia watu kumsakama kwa kila aina ya maneno jambo lililomfanya achoke na kuamua kuondoka.

“Nakifahamu Chama cha Mapinduzi, nakiheshimu kwani ndicho kilichonilea, lakini, kwa hali tuliyokuwa tumefikia, inafika mahali unasema imetosha,” alisema Lowassa.

Alitaja sababu nyingine iliyomfanya kuihama CCM kuwa ni kutaka mabadiliko na aliamini mabadiliko ya kweli yatapatikana nje ya chama hicho tawala na akisema hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alisema mabadiliko yatatafutwa hata nje ya CCM.

Alisema kwa namna yoyote, kamwe hana mpango na hawezi kurudi CCM na akasema jukumu lililopo mbele yake kwa sasa ni kuijenga Chadema ambayo yeye ni Mjumbe wa Kamati Kuu.

“Sina mpango na wala siwezi kurejea CCM, mimi ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, na jukumu lililoko mbele yangu ni kukijenga na kukiimarisha chama changu hiki kiwe imara tangu katika ngazi ya matawi,” alisema na kuongeza kuwa kazi iliyoko mbele yake sasa ni kukiimarisha chama hicho na wamejipanga kuzunguka nchi nzima kufanya kazi hiyo pamoja na kuwashukuru nwananchi kwa imani waliyoionyesha kwake na chama chake.

Lowassa alidai kuwa kama si kura kuchakachuliwa, alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwa sababu wananchi walishaichoka CCM na wakawa wanataka mabadiliko.

Alisema kazi nyingine kubwa waliyonayo sasa ni kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana na Tume ya Uchaguzi inaundwa upya kwani iliyopo si huru hata kidogo.

Alisema kama isingekuwa busara na ukomavu waliouonyesha Ukawa, basi hata hali ya siasa Tanzania Bara isingelikuwa shwari kama ilivyo sasa.

“Mara baada ya matokeo ya uchaguzi, niliwashauri vijana watulie, wasifanye fujo, nashukuru walinisikiliza.”

Alisema katika uchaguzi huo yeye na Ukawa walishinda kwa kishindo isipokuwa matokeo yalivurugwa makusudi ili CCM iendelee kubaki madarakani.

“Nilishinda na Ukawa ilishinda, kilichotokea kura zilichakachuliwa kwa kiasi kikubwa… wao wanajua, Watanzania wanajua na kila mtu anajua, tulishinda kwa kura nyingi sana na tulipokonywa ushindi wetu,” alisema.

Vijana wa Chadema kukamatwa
Alisema miongoni mwa mambo yanayomuumiza na ambayo hatayasahau katika uchaguzi huo ni kitendo cha polisi kwa maagizo ya watendaji wa Serikali kuwakamata vijana waliokuwa wanakusanya matokeo na kuwadhalilisha ikiwa ni pamoja na kuwaweka mahabusu.

Alidai kuwa kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuvuruga kituo chao walichokuwa wakijumuisha matokeo na kuacha kile cha CCM kilikuwa kibaya na kilichoonyesha wazi kuwa hawakuwa tayari kukubali kuona wakishindwa.

Alisema: “Ni aibu kubwa kwa Serikali kuwaumiza na kuwaweka ndani vijana wadogo wasiokuwa na hatia eti kwa sababu tu walikuwa wakiunga mkono mabadiliko."

Uhuru wa NEC
Lowassa alisema miongoni mwa mambo yanayozorotesha chaguzi nchini ni NEC ambayo alisema siyo huru na badala yake ni chombo kinachotumika na watawala.

Alisema chombo hicho hakitendi haki na kwamba ingekuwa mamlaka yake baada ya uchaguzi kwisha angekiondoa madarakani.

Alisema wakati umefika kwa Watanzania kuungana kudai Katiba Mpya na tume huru ya uchaguzi kwa maelezo kuwa bila Katiba mpya na tume huru kamwe hakuwezi kufanyika uchaguzi ulio huru na wa haki.

Demokrasia bungeni
Akizungumzia mwenendo wa Bunge, alisema linakwenda vizuri lakini ni mapema kulizungumzia kwa sasa.

“Katika Bunge hili wameingia vijana madhubuti bungeni, lakini hatua ya Serikali kuzuia Televisheni ya Taifa (TBC) kurusha matangazo ya Bunge moja kwa moja, hiyo ni dalili ya kuminya demokrasia.”

Alisema ni aibu kubwa kwa Serikali kutumia polisi kuingia ndani ya Bunge badala ya kujenga hoja na akasema hali hiyo ikiachwa ikaendelea italitia aibu Taifa.

Alisema moja ya mambo yaliyohimizwa na ambayo Watanzania waliachiwa na Mwalimu Julius Nyerere ni utaratibu wa kujenga hoja na kutumia nguvu ya kushinda na akaongeza kuwa kitendo cha polisi kuingia na kupiga wabunge ni kuminya na kudidimiza demokrasia.

“Tanzania tunasifika duniani kote kwa kuheshimu na kufuata demokrasia, lakini Serikali imeamua kutumia polisi kuminya demokrasia, hii ni aibu kubwa kwa Taifa… Watanzania tukiacha demokrasia ikaminywa tutalitia aibu Taifa,” alisema.

Shukrani kwa Watanzania
Lowassa anasema licha ya kupokonywa ushindi, anajivunia mafanikio makubwa aliyoyapata kutoka kwa Watanzania walio wengi ambao walimuamini na kumuunga mkono.

“Watanzania waliniunga mkono kwa wingi sana, hali ile ilinipa faraja kubwa…nilifarijika pia nilipowaomba watulie wakanielewa na kutulia… nawashukuru sana Watanzania walionielewa na kutulia,” alisema.

Alitoa wito kwa Watanzania kuilinda amani ya nchi huku akisema anasubiri Rais Magufuli kutimiza siku 100 ndipo atoe tathmini yake kuhusu utawala wake.

“Marais wanapimwa kwa siku 100, nasubiri siku hizo, nitasema.”

Hali ya kisiasa Zanzibar
Akizungumzia hali ya kisiasa ya Zanzibar na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kutangaza kurejewa uchaguzi upya, Lowassa alisema suala hilo ni zito na gumu na linahitaji maombi maalumu na umakini wa hali ya juu katika kulitatua.

Alitoa wito kwa Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM na Rais Magufuli kulishughulikia suala hilo mapema kabla ya Machi 20.

“Wasikubali tufike pabaya. Bado naamini tunaweza kulimaliza kwenye meza,” alisema na kuongeza:

“Nawasihi sana viongozi hawa wasilipuuze hili suala, jambo hili likiendelea litaleta shida kubwa kwa nchi yetu, magaidi wanaweza kulitumia na kuleta madhara makubwa, wasisubiri kufika pabaya, waanze kulishughulikia sasa.”

Alitoa wito pia kwa wanaoshughulikia suala hilo kuvishirikisha na vyama vingine badala ya kulifanya kuwa ni suala la CCM na CUF pekee.

Alisema ni imani yake kuwa Watanzania ni wamoja na hakuna mtu wa kuwagawa kwa namna yoyote na kuwa wasikubali uchaguzi huo wa marudio kuwa sababu ya kuivuruga amani ya nchi.
 
inawezeka wafuasi wa chadema kuingia kwenye Guinness worl record book kwa kua watu wa ajabu zaidi dunia...hawa jamaa hisia mbele akili nyuma.....lowasa hakuwahi kua mleta mabadiliko na hatoweza kua hata siku moja..alifukuzwa kwenye karamu ya mafisadi wenzake na hao hao mafisadi lengo lake ni kulipiza kisasi....chadema ilikua chama kizuri chini ya slaa...chini ya lowasa hakuna matarajio yoyote...hii inaonesha CHADEMA hawana uwezo wa kusimama wenyewe wanategemea candidates kutoka CCM ili wapate kick
 
Wakati akiongea na vyombo vya habari, Lowassa amesema aliondoka CCM na kujiunga na CHADEMA kwa sababu ya kusakamwa kwa maneno ya kejeli, vijembe na vitisho na kuitwa gamba na fisadi.

Lowassa alisema licha ya kuitumikia CCM kwa zaidi ya miaka 30 tangu mwaka 1977, chama hicho kiliamua kutumia watu kumsakama kwa kila aina ya maneno jambo ambalo lilimfanya pia achoke na kuamua kuondoka CCM.

‘’Ninakifahamu Chama cha Mapinduzi, ninakiheshimu kwani ndicho kilichonilea lakini kwa hali tuliyokuwa tumefikia, inafika mahali unasema imetosha,’’ Alisema Lowassa.

Alisema sababu nyingine iliyomfanya kuondoka CCM ni kutaka mabadiliko na aliamini mabadiliko ya kweli yatapatikana nje ya CCM.

Lowassa alidai kuwa kama si kura kuchakachuliwa alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwa sababu wananchi walishaichoka CCM na wakawa wanataka mabadiliko.

Alisema ana marafiki ndani ya CCM ambao walimsaidia wakati wa Uchaguzi ambapo baadhi yao walitishwa na utawala na kuamua kujiweka kando kwa ajili ya usalama wao.

Alienda mbele zaidi na kusema, kwa namna yoyote ile kamwe hana mpango wa kurudi CCM na kudai jukumu lililopo mbele yake kwa sasa ni kuijenga CHADEMA ili ishike dola.
kwa hiyo amekimbilia kwa waliokuwa wanamkejeli na kumtukana akina lisu, mnyika na mbowe . mbona alisubiri mpaka alipokatwa ndo akakimbilia huko
 
Atawadanganya hao hao wajinga,
Jina lake lisingekatwa angeondoka CCM???
Huyu mzee anajipa moyo tu ila kiukweli kishapoteza dira.
mnajadili mtu aliyepoteza Dira? basi uliyepoteza dira ni wewe
 
naona lowasa amekuwa ajenda mpya ya ccm...ajabu kweli kweli!kwani kuna wengine mlisema kuwa baada ya uchaguzi lowasa atasahaulika katika siasa za tz!ajabu kweli kweli!ila ona sasa mnavyo mpaisha sasa hv...!kwa mtindo wa kulitajataja jina la lowasa kla siku...kuna uwezekano wa watz kumsahau?dah!kweli lowasa noma!
 
Lowassa bado anaendelea na usanii wake. Anajaribu kudanganya kwa nguvu!

Kusema aliondoka CCM kwa sababu ya kuitwa fisadi na gamba ni kuwafanya watanzania kama wajinga!

Lowassa aliondoka CCM kwa sababu jina lake lilikatwa na kama lisingekatwa, leo hii angekuwa bado ni mwanachama hai wa CCM.

Hata hivyo nimpongeze Lowassa kwa kuwa na vision ambayo inachagizwa na fani yake ya usanii.

Baada ya kukatwa jina lake ndani ya CCM na ndoto zake za kuwa Rais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM zikayeyuka. Aliamua kupiga ndege wawili kwa kutumia jiwe moja.

Kwanza, aliamua kujiunga CHADEMA ili wamsafishe na kulitua zigo la kuitwa fisadi ambalo wao wenyewe CHADEMA walimtwika kwa zaidi ya miaka minane.

Pili, Kwa kulishusha zigo ambalo walimtwika, aliwapa pia Viongozi wa CHADEMA kazi ya kumnadi kwa Watanzania ili wamchague kuwa Rais wa Tanzania.

Kazi hiyo ya kumsafisha mpaka sasa wanaendelea nayo!
Haiingii akilini hata kidogo,atakayemwamini inabidi apimwe akili.ukiangalia kwa makini Chadema ndio walikuwa WAASISI wa kumsema vibaya na ndio wamemsema vibaya zaidi ya CCM na kwa muda mrefu.

Iweje sasa atoke CCM na kukimbilia huko huko ambako ndiko waliasisi na kuongoza kumchafua(tena hata bila kumuomba radhi!)halafu aseme ametoka kwa kuwa ameitwa gamba na fisadi na CCM?Au kuitwa fisadi na CHADEMA ni sahihi lakini kuitwa na CCM ndio makosa?na je kwanini asingetoka mapema badala yake akasubiri mpaka WALIPOMFYEKA kule Dodoma?

Kwenye hili maswali ni mengi kuliko majibu.
 
Wakati akiongea na vyombo vya habari, Lowassa amesema aliondoka CCM na kujiunga na CHADEMA kwa sababu ya kusakamwa kwa maneno ya kejeli, vijembe na vitisho na kuitwa gamba na fisadi.

Lowassa alisema licha ya kuitumikia CCM kwa zaidi ya miaka 30 tangu mwaka 1977, chama hicho kiliamua kutumia watu kumsakama kwa kila aina ya maneno jambo ambalo lilimfanya pia achoke na kuamua kuondoka CCM.

‘’Ninakifahamu Chama cha Mapinduzi, ninakiheshimu kwani ndicho kilichonilea lakini kwa hali tuliyokuwa tumefikia, inafika mahali unasema imetosha,’’ Alisema Lowassa.

Alisema sababu nyingine iliyomfanya kuondoka CCM ni kutaka mabadiliko na aliamini mabadiliko ya kweli yatapatikana nje ya CCM.

Lowassa alidai kuwa kama si kura kuchakachuliwa alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwa sababu wananchi walishaichoka CCM na wakawa wanataka mabadiliko.

Alisema ana marafiki ndani ya CCM ambao walimsaidia wakati wa Uchaguzi ambapo baadhi yao walitishwa na utawala na kuamua kujiweka kando kwa ajili ya usalama wao.

Alienda mbele zaidi na kusema, kwa namna yoyote ile kamwe hana mpango wa kurudi CCM na kudai jukumu lililopo mbele yake kwa sasa ni kuijenga CHADEMA ili ishike dola.

kwni ni uongo hata ukimuuliza mtoto mdogo atakuambia kuwa ni fisadi, pongezi kwa kubenea na gazeti lake kwa mana kila toleo lazima limtaje fisadi mkuu na gamba lake ha ha haaaaaa
 
  • Thanks
Reactions: nao
Achaneni na huyu mzee kama hana impact yoyote kwenu. Ya nini kumjadili wakati "kumbe ni mwongo?"

Sisi wengine ndiye Rais wetu, ndiye tuliyemchagua. Ninyi mnaye Rais wa Tume ya uchaguzi (NEC) huyu msanii JPM.....jipu kuu la ufisadi wa barabara na nyumba za serikali linalotumbua majipu na vipele vidogo vidogo!!
 
Lowasa angeendelea kukaa kimya kama sumaye na akna kingunge heshima yake ingeongezeka kwa 0.01%,lakini ameamua kujidhalilisha.
 
Back
Top Bottom