Lowassa kufutiwa uanachama wa CCM?

Lowassa kufutiwa uanachama wa CCM?

uwemba1

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
987
Reaction score
718
Tetesi kutoka chanzo kimoja kilichopo Dodoma katika kikao cha CCM ni kuwa Waziri mkuu huyo wa zamani atafutiwa uanachama na hivyo hatagombea Urais hapo 2015.

Inasemekana awali wajumbe waliomhoji walipendekeza apewe adhabu ya kutokugombea kwa muda wa miezi 18, jambo ambalo lingemfanya kushindwa kugombea katika uchaguzi ujao.

Naendelea kufuatilia details nitazileta mapema nikithibitisha maana kikao kilikiwa bado kinaendelea.
 
mkuu fanya kama ulivyo ahidi watu tumepotelewa na usingizi hapa fanya haraka na hizo dito
 
Atakuwa ameingia hasara kubwa sana. Bora wafumbe macho tu wamfukuze maana hasafishiki. Ila kama atang'ang'ania na hatimae akpitishwa na maccm wenzake kampeni zetu mwakani zitakuwa rahisi sana kama itakavyokuwa huko Kalenga.
 
Hakuna wa kumfukuza EL, CCM wanajuana sana ndo maana unaona wanaitwa hafu hakuna maamuzi yyoyte ya maana utakayoyasikia. Ndo maana walisema "Yalikuwa mazungumzo ya chai"
 
Mbona Lowasa alisha sema kuwa hataondoka peke yake wakitaka kumuondoa ni lazima na mwenyekiti aondoke.Lakini hata hivyo ni mwelekeo mzuri kwa CCM kwani somo la CHADEMA litakuwa limeanza kuwaingia.
 
Sidhani kama hayo mapendekezo yatatekelezeka kwa CCM....twasubiria taarifa zaidi....
 
Nasikia Lowassa aliwahi kusema kuwa yeye atakuwa rais wa Tanzania 2015 hata kwa chama "jiwe", si lazima CCM.
Though sidhani kama ccm wana uwezo wa kumtimua lowassa.
Anywayz, niwaache wafu wawazike wafu wao....
 
Back
Top Bottom