OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 437
Ukiangalia nchi yetu jinsi ilivyo na changamoto tulizonazo kuhisiana na ustawi na wa Taifa letu vi vema tukawa na kiongozi mwenye hulka ya maamuzi magumu sana zaidi awe mchapakazi hodari wa kupigiwa mfano hata record yako iwe inamshuhudia hivyo,Kati ya wote waliotangaza nia mtu ambaye watanzania wameonyesha kuwa anaweza kubeba jukumu hilo si mwingine bali Edward Lowassa,Huyu ni mchapakazi anayejipambanua kwa namna yake na kizuri ni ambaye anaamini sana kile ambacho anakisimamia pasi na mashaka yoyote ile.CCM inatakiwa iwatendee watanzania haki yao ya msingi kwa yule ambaye tumeona anaweza kutuvusha ng'ambo ya maendeleo na zaidi wazingatie ushauri wa mwenyekiti wao JK kuwa wasifikiri kwamba eti mgombea akichaguliwa na CCM basi amepita zama hizo zimeshapita kitambo sana na wananchi sasa wanaelewa vilivyo kwani wanaopiga kura wanafika zaidi ya watu million 19 au 20 kama wote wakijiandikisha na kupiga kura.Tafakari