Elections 2015 Lowassa: Je, alikosea wapi? Akiamua kuendelea, arekebishe wapi?

Mkuu Pasco

Uko vizuri sana kuchambua na kubashiri mwelekeo wa siasa zetu. Hongera tena kwa kuwa na kiburi cha kuamini kwamba 'it is not over till it's over'.

Karama yako ya kuchambua na kubashiri ni karama adimu. Hongera mno kwa karama hii. Mwenyezi Mungu akujalie ujasiri ili utumie karama hii kwa faida ya nchi yetu hasa hasa kwenye kupigania ustawi wa watu masikini na wanaotengwa na jamii (socially excluded) kwa sababu mbalimbali.

Nikutakie heri na fanaka kwa mwaka 2016.

Inshallah.
Mkuu 50thebe, Asante. P
 
Kabla sijapitia hoja naomba nichangi.
e hoja inayosema haiwezekani mtu kuhonga watu milioni moja.

Tunasema inawezakana, kina matter ni definition ya hongo. Imesemwa hongo inaweza kuwa ya pesa, nafasi au upendeleo

Haiwezekani kutoa hongo kwa watu milioni 1. Inawezekana kuhonga watu milioni 1 kwa njia za ahadi, upendeleo, mafao n.k.

Katika kutekeleza hilo mtu hahitaji watu 100. Wanahitajika watu 50 wenye ushawishi katika jamii.

Hawawanaweza kuitwa influencial leaders au ‘KOL' ikimaanisha key opinion leader.
Ndivyo lobbying ya taasisi inavyofanyika


Kuchukua wenyeviti wa mikoa, wajumbe wa NEC na CC wenye command katika maeneo yao inatosha kuhonga watu M1 .Ukiwawezesha kwa pesa, nao watawezesha wenyeviti wa Wilaya, tarafa had ikata.

Huko ni ahadi tu, mzee akifanikiwa utapanda na kuwa DC, mkuu wa mkoa, au waziri. Hivyo hongo ipo katika mfumo huo

Hoja za maswali ya Mchambuzi


1 Akiamua kwenda upinzani, Edo atafungua milango ya kuanikwa.Kumbuka, atakuwa ‘Rai' na CM ikiwana dola.
Mwisho wa siku atachafuka kisiasa na kijamii. Anaweza kujikuta Kisutu kama walivyofanyiwa wawili walioko magereza


2 Akihama CCM kwenda upinzani, chama kitakacho mpokea kitaingia katika mgogoro mkubwa na umma.
‘Nembo' yake inahusishwa na udanganyifu , ufisadi n.k Chama husika kitapoteza uhalali wa kusimamia maadili ya nchi.


Chama hicho hakitakuwa na platform ya kukemea achilia mbali kuzungumzia uovu kitanasibishwa na uovu.
Unawezaje kuoga maji safi ukajifuta na taulo chafu na kusema umetakata?


3 Akihama CCM, athari itakuwa chanya. CCM itakuwa imejitakasa kwa kuvua gamba bila mawaa.

Hata leo inajifaragua kuvua gamba,seuse akiondoka. Hakuna athari ya kisiasa au wanachama.

Ataondoka na kundi dogo lenye waaminifu, si kama inavyodhaniwa. Ni kundi la ‘KOL' ambalo halina muda wakujipanga.


Kwa hofu hiyo, tayari tumeona wajumbe wa CCM walioku wakaribu wengine walibaki kumshangilia Mzee Pombe.

CCM inaomba aondoke na watu wake wachache ili iweze kujijenga kupitia yeye na wenzake
Mkuu vipi unazungumziaje hii coment yako hapo juu tena kuhusu chama kilichompokea EL?
 
Lowassa atafaa sana kuwa ama litNerature figure study or political science study. Na silisemi hili kwa masihara, bali nikiwa very serious kuwa tunavyoendelea mbele, kuna watu katika jamii yetu na vizazi mbali mbali watatokea kuwa wa pekee na ni wasifu tosha wa kusoma na kujifunza kwa wigo mkubwa sana: Lowassa kama binaadamu, Lowassa kama mzazi, Lowassa kama mume, Lowassa kama mwanasiasa.

Labda na sisi tutaacha kusoma ya Socrates, Marx na Adam Smith, tumwongeze Lowassa pamoja na kina Kinjekitile, Nyerere na Mkwawa!
Nakubaliana na wewe mkuu.

Nimejifunza vitu vingi sana kupitia EL tangu akiwa ccm,na pia akiwa nje ya ccm.
 
2 Akihama CCM kwenda upinzani, chama kitakacho mpokea kitaingia katika mgogoro mkubwa na umma.
‘Nembo' yake inahusishwa na udanganyifu , ufisadi n.k Chama husika kitapoteza uhalali wa kusimamia maadili ya nchi.


Chama hicho hakitakuwa na platform ya kukemea achilia mbali kuzungumzia uovu kitanasibishwa na uovu.
Unawezaje kuoga maji safi ukajifuta na taulo chafu na kusema umetakata?


3 Akihama CCM, athari itakuwa chanya. CCM itakuwa imejitakasa kwa kuvua gamba bila mawaa.
 
Je, sicho kinachotokea sasa hivi? Je, sicho kilichotokea wakati wa kampeni?

Ahsante
Je, sicho kinachotokea sasa hivi? Je, sicho kilichotokea wakati w.a kampeni?

Ahsante
Ndicho kinachotokea sasa hivi.

Ndicho kilichotokea wakati wa kampeni.

Je unashauli nini ili hali hiyo isiendelee?.

Tunahitaji upinzani imara unao weza kuikemea serikali.Je wafanyaje sasa?.
 
Ndicho kinachotokea sasa hivi.

Ndicho kilichotokea wakati wa kampeni.

Je unashauli nini ili hali hiyo isiendelee?.

Tunahitaji upinzani imara unao weza kuikemea serikali.Je wafanyaje sasa?.
Kuna mahali nimeandika na kuudhi baadhi ya watu
Nilisema hivi 'huwezi kumfundisha mbwa mzee mzee mbinu mpya'
Nikimaanisha ni wakati wa ku ''rejuvenate''

Hapo ni kuanzia uongozi wa vyama husika. Kambi ya upinzani n.k. Na mkazo ni katika kambi ya upinzani
 
Kuna mahali nimeandika na kuudhi baadhi ya watu
Nilisema hivi 'huwezi kumfundisha mbwa mzee mzee mbinu mpya'
Nikimaanisha ni wakati wa ku ''rejuvenate''

Hapo ni kuanzia uongozi wa vyama husika. Kambi ya upinzani n.k. Na mkazo ni katika kambi ya upinzani
Kwa hiyo mkuu Nguruvi3,vyama vya upinzani vinatakiwa kujichuna ngozi upya(kama nyoka)? kama imechukua miaka takribani 20 kufikia walau kasi hii huoni kuwa itachukua muongo mwingine kupata strong upinzani?
Mie nadhani:
1: Vyama vya upinzani kwa kupitia vijana wake ie BAVICHA, ACT,nknk wajipambanue upya bila kuwategemea the so called"mbwa wazee"
2: Viongozi wazee wa upinzani wawaandae vijana kuendesha chama au vyama hivi .vijana kama Mnyika, salum Mwalim, Halima Mdee, Zitto, nknk.
Pamoja na "uchovu"wa CCM lakini ninawasifu kwa kuwaandaa vijana wao(Makonda, Nape, Januari Mavunde, Mwigulu nknk).
Siasa ni sayansi na sayansi ni Mfumo.
 
Mkuu Mchambuzi, kwanza asante kwa uzi huu, pia asante kwa mchango kutoka kwa Mkuu Nguruvi3.

Baada tuu ya jina la Lowassa kukatwa kwenye 5 bora, nilipandisha uzi huu, Kukatwa Kwa Lowassa, Jee Ndio Mwisho wa Ile Safari, Au..., nikishauri ahame CCM safari iendelee, huku nikitaraji atakayepita ni Membe!.

Lakini baada ya kupitishwa Magufuli, nilifanya about turn na kumshauri sasa atulie tuu, kwa sababu Magufuli ni jembe zaidi ya Lowassa!. Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali yaishe, vunja kambi na kujisalimisha!.

Katika uzi wangu wa posibility ya kupitishwa kwa Magufuli nilioupandisha humu Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli, nilitoa angalizo kuwa jina la Magufuli limetajwa for a reason!. Mpaka sasa kuna watu wanaamini kupitishwa kwa Magufuli kumetokea tuu by chance na sio plan or pre meditated move!.

Nikirudi kwenye hoja hizi
1. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwake kisiasa?-mpaka hapo tuu baada ya kukwa, Lowassa sasa kwisha!, baada ya kupita kwa Magufuli, hata akihamia upinzani bado atakwisha tuu!.


2. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama atakachohamia?, athari zitakuwa kama zile za Mrema tuu, atahama na wafuasinwake wawili watatu, chama atakachojiunga kitainuka kwa nguvu ya soda tuu, then atajifia na kitajifia zake!.

3. Akiamua kuhama ccm na kwenda upinzani, Nini itakuwa athari kwa chama chama cha mapinduzi?- mgombea angekuwa Membe kisha Lowassa akahama, CCM kingeathirika sana kwa sababu angekata pande kubwa la Kanda ya Ziwa, na CCM ingepigwa chini jumla!.

Tukubali tukatae, kwenye siasa zetu kuna karata mbili za turufu ambazo huwa zinatembea, hatuzikubali lakini zipo!.
Hii ni turufu ya Udini na Ukanda. Katika kumchagua Magufuli, hizi zote mbili zimezingatiwa. Ukinisoma hapa utanielewa
[h=3]Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote?.
[/h][h=3]Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real?
[/h]Kuna uzi niliwahi kuupandisha humu kuuliza "Rais wa Tanzania akiwa Mkristu "Jee ni lazima awe Mkatoliki?!", mode waliifuta fasta na mimi kunyooshewa kidole cha "mdini mkuu!". Nilipopandisha huu uzi Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli, based on sababu nilizozisikia, na hili likaja kutokea, hivyo nime confirm kile nilichokisikia, lakini sio lazima kukisema kila unachokisikia, haswa ikitokea unaposikia jamba ambalo una disbelief halafu linatokea!.


Tuna siasa za Ukanda, niliwahi kusema humu, kuna Kanda fulani ndizo determinant ya nani anakuwa rais wa Tanzania!. Nikasema humu kuwa lakini hata Kaskazini yote wawachague wapinzani, bila kuishika Kanda ya Ziwa, mtu wao hawezi kuwa rais!. Kanda ya Ziwa ndio determinant. Kama ulinote hata Lowassa aliweka msisitizo Kanda ya Ziwa, mtu kama Mgeja ndizo zilikuwa nguzo zake!, siku ile akitangaza nia pele Sheikh Amri Abeid, Lowassa aliinuka kitini kuja kumpokea M/Kiti wa CCM Geita, Joseph Msukuma!. Hata kama umefuatilia kwa karibu nyendo za Kinana kwenye Kanda ya Ziwa, utanielewa!. Kanda hii ndio yenye the biggest chunk ya population kubwa Tanzania. Wazukuma ndilo kabila kubwa kuliko kabila jingine lolote nchini Tanzania na ndilo kabila pekee linalomiliki mkoa mmoja mzima wenye kabila moja bila kuchanganya na kabila jingine lolote!.

Baada ya kuchaguliwa Magufuli kutoka kanda ya Ziwa, damu ni nzito kuliko maji, hivyo ile support yote ya Kanda ya Ziwa ambayo Lowassa angeitumia kama mtaji, sasa imerudi nyumbani!.

Ila Chadema/Ukawa, kama ndio bado itamtegemea kwa Lowassa kwa 2020, watakuwa watu wa ajabu sana, kwa sababu by 2020, Lawassa atakuwa by passed by events, he will be too old to cop. Chadema watafute damu change ambaye ni charismatic, kwa ajili ya kujipanga tuu kwa 2025, kwa upande wangu, uchaguzi wa 2020 kwenye urais, ni igizo tuu la uchaguzi!. Hivyo the best thing kwa sasa Lowassa to do, ni kutulia, kukubali matokeo na kustaafu kwa amani, akajichungie ngombe wake kwenye zile ranchi zake, na kwenda akajipumzikie kwenye kasri lake kule London maisha yake yaliyobakia!.

Paskali
Baada ya Edward Lowassa kusifiwa na rais Magufuli kuwa ni Superman, namdurufu kidogo Lowassa kwa kujikumbusha niliwahi kusema nini kuhusu mtu huyu.
P
 
Back
Top Bottom