Lowassa hayumo 5 bora ndani ya CCM

Lowassa hayumo 5 bora ndani ya CCM

Huyo ni MwanaChadema anampenda sana Lowasa,, Yuko radhi kufa kwa ajili ya Lowasa,,Hongera sana Mmawia kwa kuutambua utapeli wa Chadema

lakisipesa
una mambooo,,,mara yuko upande wa lowasa,,mara anaponda tena,,
kweli ww ni kanga moko ndembendembe
 
Muhogo ndo mpango mzima na mkubari sana huyu jamaa ni mzee wa action akosema ndio au hapana ni hivyo hivyo akikosa endapo ccm itashinda wampe uwaziri mkuu anafaaa

Hata mimi huyu jamaa namkubali sana.Sema Watz kama wamepagawa kiasi kwamba hata ukiwa barabarani unatembea, mtu/watu wakakuzushia mwizi huyoo, raia watakushambulia kwa mawe na petroli na hatimaye kukuua.Hawatataka hata utetezi wako.Muhongo is a real man to sail our boat.
 
Jamaa ana longolongo ni kazi kwa kwenda mbele kipindi yupo wizarani tulishaanza kusahau mgawo wa umeme na alijitahidi umeme kufika vijijini pia akuwa mnafiki pale aliposema watanzania awana uwezo wakuwekeza kwenye gesi ni kweli kuwekeza kwenye gesi si mchezo ndo chanzo cha kugombana na mengi
 
Membe - Huyu ni mtu ambae ukimuona huwezi kumdhani, hajafanya ukorofi wowote wa kutaka urais, amejipanga kivyake na watu wake ambao hakutaka kuweka makundi ndani na nje ya CCM.

Uzoefu wake ndani na nje ya nchi na sifa ya kuwa shushushu wa muda mrefu vinamfanya kamati kuu ya CCM kumwamini.

Membe nadhani ni chaguo la JK.

Hatakuwa na madhara na JK baada ya kuingia Ikulu, hana kashifa ya kumletea madhara, ni vyema mkajua Membe ana nafasi kubwa sana kuwa Urais, nampa 70% kupenya ndani ya kamati kuu.

Makongoro - Kitakachombeba zaidi ni jina la baba yake na upole wa familia ya mwl Nyerere toka baba yao akiwa Ikulu hadi leo anapojitokeza Makongoro kuutaka urais.

Kimsingi Makongoro atawashangaza watu, kuhamia NCCR Mageuzi ni sehemu tu ya kujifunza kwake siasa za upinzani na CCM, hili siyo kosa.

Wapo akina Wassira walihama ila leo ndio wanaibeba CCM, umakini na kujishusha kwa Makongoro kutamuweka pazuri. Nampa 60 %.

Wassira - Turufu yake ni kubwa ndani ya CCM, kama CCM inahitaji kulinda UCCM wake, mtu sahihi ni Wassira, huyu ni mfia CCM kwa sasa, ulinzi wa CCM unamtegemea sana Wassira,anapenda sheria kandamizi.

Hili siyo tatizo kwa CCM ila ndo vitu amabavyo chama tawala hasa Afrika wanapenda.Wassira ni maridadi sana wa kutetea hata visivyo na maana.CCM wanapenda hivyo, ana ushawishi ndani ya CCM. Nampa 67%

Muhongo - Achilia mbali ESCROW ambayo kimsingi ahusiki, hawezi game chafu za kisiasa, anaweza kuitendea vyema nafasi ya Urais.

Huyu anabebwa na umakini wake, watu wa aina ya Muhongo mara nyingi jamii haiwataki, jamii inapenda watu wa porojo sana.

Ukiwa kama pro Muhongo unatakiwa uwe na team ya kukuchezea mpira vyema na mara nyingi iwe ni timu ya watu maarufu, usitegemee Muhongo anaweza kukuangusha kwa lolote. Nampa 55%

Mwandosya - hana tofauti kubwa na Muhongo, tofauti zao zipo kwenye muda wa kudumu kwenye siasa.

Amekuwa katika siasa muda sana, anaijua CCM, anajua sana ubaya wa CCM kuliko uzuri, Muhongo na Mwandosya wanaingia kwenye siasa kwa sababu tu serikali inashindwa kuwatumia kwingine, serikali za kiafrika huwa zinapanga team kwa ajili ya kujilinda na siyo kuwalinda wananchi. Nampa 60%

Pinda - huyu ana udhaifu mkubwa sana ila advantage yake ni kwamba system ya nchi inamtaka kwa sababu ya udhaifu wake ili waweze kumwamulia, ukiwa na rais kama Pinda tegemea vurungu za kila siku ndani ya nchi na hii inatokana nembo yake ya urais kupwaya.

Ameprove failure sana kwenye nafasi ya uwazri mkuu, ana nafasi kubwa ya kushinda, hii inatokana na kuwa Pinda hana madhara kwa mtu yeyote ile ndani ya nchi..hawezi kulipiza kisasi. Nampa 65%
 
Sisi tunasubiri mmalize ligi yenu then tumjue kibonde wa kupambana na sisi wana ukawa ni nani
 
Ule umati wa Arusha ulitoa majawabu...... saizi tunajikita kuwaeleza wananchi nini tutawafanyia na siyo kulumbana tena.....
 
sirjohn

Hizo Asilimia zinaendanje naona kama sikuelewielewi make mwisho wa siku zinakuwa jumala 377% au kuna mfumo tofauti umeutumia hebu iweke sawa pleae kwa maelezo huru!
 
Last edited by a moderator:
Naheshimu mawazo yako. Ila wana CCM ndio wanaojua yupi awe mgombea wao
 
Ule umati wa Arusha ulitoa majawabu...... saizi tunajikita kuwaeleza wananchi nini tutawafanyia na siyo kulumbana tena.....
Kwa kawaida kwenye fiesta kunakuwa na watu wengi sana. Huwezi kuwaita akina Diamond, Khadija Kopa nk then usitegemee kuona umati mkubwa wa watu
 
Hizo Asilimia zinaendanje naona kama sikuelewielewi make mwisho wa siku zinakuwa jumala 377% au kuna mfumo tofauti umeutumia hebu iweke sawa pleae kwa maelezo huru!

Rudi darasani ndugu..
 
Mkuu tunafurahi kwa uchambuzi wa mawazo yako,ila tukukumbushe kuwa marks zote zinakuwa na jumla ya 100% ,hii ni hesabu huwezi kugawa watu na wote unawapa 50% + or 60%+ .Ili record zako ziwe information yenye maana unatakiwa kuwapa wote marks ndani ya 100%,kwa kuwa hakuna option ya kuwa na watu zaidi ya mmoja wakaingia ikulu kwa pamoja.
 
Hii no kama darasani wanapata kila mtu marks zake. Huwa hazijumlishwi hivyo. Yuko saw a kabisa
 
Mkuu tunafurahi kwa uchambuzi wa mawazo yako,ila tukukumbushe kuwa marks zote zinakuwa na jumla ya 100% ,hii ni hesabu huwezi kugawa watu na wote unawapa 50% + or 60%+ .Ili record zako ziwe information yenye maana unatakiwa kuwapa wote marks ndani ya 100%,kwa kuwa hakuna option ya kuwa na watu zaidi ya mmoja wakaingia ikulu kwa pamoja.

Rudi darasani ndugu..

Thanks GT Donybeny naomba muleze na huyu Ulimakafu!!!
 
Hata mimi huyu jamaa namkubali sana.Sema Watz kama wamepagawa kiasi kwamba hata ukiwa barabarani unatembea, mtu/watu wakakuzushia mwizi huyoo, raia watakushambulia kwa mawe na petroli na hatimaye kukuua.Hawatataka hata utetezi wako.Muhongo is a real man to sail our boat.

Huyu si alisema Watz saizi yao kuuza juice na maji.....
umekula maharage ya wapi wewe ndo umpe nchi etiii eeh...........
Mh haya!
 
Back
Top Bottom