Lowassa hayumo 5 bora ndani ya CCM

Lowassa hayumo 5 bora ndani ya CCM

sirjohn

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2014
Posts
767
Reaction score
679
Membe - Huyu ni mtu ambae ukimuona huwezi kumdhani, hajafanya ukorofi wowote wa kutaka urais, amejipanga kivyake na watu wake ambao hakutaka kuweka makundi ndani na nje ya CCM.

Uzoefu wake ndani na nje ya nchi na sifa ya kuwa shushushu wa muda mrefu vinamfanya kamati kuu ya CCM kumwamini.

Membe nadhani ni chaguo la JK.

Hatakuwa na madhara na JK baada ya kuingia Ikulu, hana kashifa ya kumletea madhara, ni vyema mkajua Membe ana nafasi kubwa sana kuwa Urais, nampa 70% kupenya ndani ya kamati kuu.

Makongoro - Kitakachombeba zaidi ni jina la baba yake na upole wa familia ya mwl Nyerere toka baba yao akiwa Ikulu hadi leo anapojitokeza Makongoro kuutaka urais.

Kimsingi Makongoro atawashangaza watu, kuhamia NCCR Mageuzi ni sehemu tu ya kujifunza kwake siasa za upinzani na CCM, hili siyo kosa.

Wapo akina Wassira walihama ila leo ndio wanaibeba CCM, umakini na kujishusha kwa Makongoro kutamuweka pazuri. Nampa 60 %.

Wassira - Turufu yake ni kubwa ndani ya CCM, kama CCM inahitaji kulinda UCCM wake, mtu sahihi ni Wassira, huyu ni mfia CCM kwa sasa, ulinzi wa CCM unamtegemea sana Wassira,anapenda sheria kandamizi.

Hili siyo tatizo kwa CCM ila ndo vitu amabavyo chama tawala hasa Afrika wanapenda.Wassira ni maridadi sana wa kutetea hata visivyo na maana.CCM wanapenda hivyo, ana ushawishi ndani ya CCM. Nampa 67%

Muhongo - Achilia mbali ESCROW ambayo kimsingi ahusiki, hawezi game chafu za kisiasa, anaweza kuitendea vyema nafasi ya Urais.

Huyu anabebwa na umakini wake, watu wa aina ya Muhongo mara nyingi jamii haiwataki, jamii inapenda watu wa porojo sana.

Ukiwa kama pro Muhongo unatakiwa uwe na team ya kukuchezea mpira vyema na mara nyingi iwe ni timu ya watu maarufu, usitegemee Muhongo anaweza kukuangusha kwa lolote. Nampa 55%

Mwandosya - hana tofauti kubwa na Muhongo, tofauti zao zipo kwenye muda wa kudumu kwenye siasa.

Amekuwa katika siasa muda sana, anaijua CCM, anajua sana ubaya wa CCM kuliko uzuri, Muhongo na Mwandosya wanaingia kwenye siasa kwa sababu tu serikali inashindwa kuwatumia kwingine, serikali za kiafrika huwa zinapanga team kwa ajili ya kujilinda na siyo kuwalinda wananchi. Nampa 60%

Pinda - huyu ana udhaifu mkubwa sana ila advantage yake ni kwamba system ya nchi inamtaka kwa sababu ya udhaifu wake ili waweze kumwamulia, ukiwa na rais kama Pinda tegemea vurungu za kila siku ndani ya nchi na hii inatokana nembo yake ya urais kupwaya.

Ameprove failure sana kwenye nafasi ya uwazri mkuu, ana nafasi kubwa ya kushinda, hii inatokana na kuwa Pinda hana madhara kwa mtu yeyote ile ndani ya nchi..hawezi kulipiza kisasi. Nampa 65%
 
Wakati kura yangu ikiwa haina shaka kuwa itaenda Upinzani, leo ofisini mfanyakazi mwenzangu anasema kuwa 'CCM hata wasipomweka chaguo lake Mh. ENL, wakamweka Ng'ombe tu, yeye bado atachagua Ng'ombe'. Such die hard fans ndio stronghold ya Ushindi wa CCM. Sidhani kama wao hupima kwa criteria yoyote ile.
 
Muhogo ndo mpango mzima na mkubari sana huyu jamaa ni mzee wa action akosema ndio au hapana ni hivyo hivyo akikosa endapo ccm itashinda wampe uwaziri mkuu anafaaa
 
Jamani nyie mnaongea tu kwa kubwabwaja maneno,hakika hakuna mwenye ushawishi hapo ccm kama Lowasa....ninawaambia Rais ajaye ni Edward Lowassa....nashangaa kila siku watu wanamsema yeye tu...lakini mti wenye matunda ndo hupigwa mawe
 
Mtakuja kuyapasua moyo haya mateam ya simba na azam
 
Mi upinzani hata kama wakimuweka SELEMAN MSINDI a.k.a Afande sele bado kura yangu ndo itakapoenda huko
 
Kwi! Kwi! Kwiiii!!!! Maskini Pasco ! kwahiyo safari ya matumaini ndio imeisha ? kuna ujumbe nimeona mahali fulani unasema hivi , panya akiingia kwenye chungu basi usikivunje chungu ili kumuua , inamisha chungu taratibu mmwage na muue kwa kumkanyaga , okoa chungu .
 
sirjohn

Mkuu nimepitia bandiko lako na kulielewa sana,ila kwa habari za ndani ya chama na serikali ni kuwa kuna uwezekano wa rais akatoka zanzibar,ili kukwepa lawama za wabara waliotangaza nia na wanaotegemea kutangaza nia,uwezekano wa Dr shein akapitishwa kugombea ni mkubwa,ila tusubiri maana hakuna mwenye uelewa wa jambo Hilo 100%, zaidi wakubwa wa nchi.
 
Last edited by a moderator:
Jamani nyie mnaongea tu kwa kubwabwaja maneno,hakika hakuna mwenye ushawishi hapo ccm kama Lowasa....ninawaambia Rais ajaye ni Edward Lowassa....nashangaa kila siku watu wanamsema yeye tu...lakini mti wenye matunda ndo hupigwa mawe

Mkuu,lowasa ni kweli anapendwa na watu wa kawaida ila kwenye system,kwa lowasa ni pagumu sana kumpitisha lowasa.
 
Kwi! Kwi! Kwiiii!!!! Maskini Pasco ! kwahiyo safari ya matumaini ndio imeisha ? kuna ujumbe nimeona mahali fulani unasema hivi , panya akiingia kwenye chungu basi usikivunje chungu ili kumuua , inamisha chungu taratibu mmwage na muue kwa kumkanyaga , okoa chungu .

Mkuu kwa nyepesi zilizopo lowasa hata kwenye 5 Nora haingii kabisa,tuombe usalama tushuhudie hii mechi.
 
Lowasa anakubalika kwa wasaka tonge na mafisadi wenzie.Hana maono zaidi ya kudhani pesaa inaweza mnunulia urais.Mwaka huu ni wa UKAWA tu , sioni MTU huko fisiem wa kupambana nao
 
Back
Top Bottom