Lowassa hatachaguliwa kupeperusha bendera ya CCM urais 2015!

UNDENIABLE

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2013
Posts
2,326
Reaction score
1,315
Wakuu! Heshima mbele!

Ipo hivi:
Lowassa hatapeperusha katu bendera ya CCM urais 2015. Ma don wa chama wameshaafikiana tayari kuhusu hili. Tathmini makini iliyofanywa na chama imebaini kuwa CCM wanaweza kushinda urais 2015 kwa namna yoyote ile iwe kwa kutumia mkono wa chuma ama mbinu yeyote ile haramu, lakini kushinda watashinda.

Kinachowaumiza kichwa ni je kama wakishinda kwa uharamia kama walivyozoea vipi kuhusu amani ya Taifa? Nchi itaendelea kuwa tulivu kwa kiwango cha kuridhisha ama itakuaje? Hili la amani ndilo linaloleta utatanishi kwa sasa, lakini si kuhusu kushinda uchaguzi!

Lowassa atakatwa jina kwa sababu hizi hapa:

1. Mahasimu wake waliopo ndani ya chama wamejipanga vilivyo

2. Kauli ya Mbowe kuwa Lowassa ni bubu hawezi kuongea kwenye ulingo wa siasa

3. Kauli ya Dr Slaa kuwa hawezi kula sahani moja na fisadi.

Hizi kauli za Mh Mbowe na Dr Slaa zimetoa kiashiria kuwa Lowassa hawezi kupokelewa UKAWA, na hata akienda ACT hatakuwa na madhara makubwa maana chama kimeamua kushinda uchaguzi kwa mbinu yeyote ile iwe haramu ama halali

4. Ukwasi wake mkubwa unaotumika kupata urais wa JMT hili litaadhiri taswira ya chama (jembe na nyundo) na sasa kuonekana ni chama cha matajiri. Ikumbukwe wapiga kura wengi ni wa kipato cha kati na cha chini na sio matajiri. Hivyo chama kitavaa koti la ufisadi mchana kweupee kama huyu ndugu akiteuliwa kugombea urais

5. Lowassa alichelewa kujisafisha, sasa hivi hasafishiki tena akiwa kwenye ulingo wa mapambano, amechelewa. Ni kweli kuwa ndani ya chama hakuna msafi lakini yeye kakosea strategy za kujisafisha

6. Lowassa hajaweka hadharani mpango wake wowote wa kushawishi wananchi kuhusu urais wake kama atateuliwa.

Mfano: Lowassa anazungumzia ajira lakini hajaweza kutoa muelekeo wowote wa namna ajira hizo zinavyopatikana kiasi cha kuwashawishi wananchi.

Hajatoa mpango kazi wowote wa namna ya kuimarisha elimu kama anavyotanabaisha kuwa elimu kwake ndio kipaumbele, yeye anaongea tu kuhusu umuhimu wa elimu lakini hajaeleza waziwazi kuhusu udhaifu wa mfumo wa elimu iliyopo sasa hivi na nini atakachokifanya kuboresha. (watu wengi watasema sasa haya si atatoa wakati wa kampeni? ukweli ni kuwa alipaswa kuweka mipango yake wazi mapema sana ili kupata ushawishi kutoka kwa wananchi kiasi cha kuwatishia ma don wa chama kukata jina lake).

Tuendelee kusubiri kuna plans B dhidi ya Lowassa. Plan B hii ni kwa ajili ya kunusuru chama ndani ya chama
 
Hili jamaa linajisumbua tu nchi ishaenda UKAWA tayari ila kwa ushauri tu nazan mumfanye mgombea mwenza wa Jaji Augustine kidogo itasaidia maana hata Dr. Gharib Bilal mlimfanyia hivi
 
Mkate msikate jina lake haitusumbui, tunachojua ccm lazima waangukie pua october 2015!
 
CCM kuna machafuko makali kama yale ya Misri c.c Ritz
 
Last edited by a moderator:
Wakuu! Heshima mbele!

Hii ni ya motomoto kabisa kutoka jikoni (mods acheni huu uzi hapahapa msiunganishe)

Ipo hivi:
Lowassa hatapeperusha katu bendera ya CCM urais 2015. Ma don wa chama wameshaafikiana tayari kuhusu hili. Tathmini makini iliyofanywa na chama imebaini kuwa CCM wanaweza kushinda urais 2015 kwa namna yoyote ile iwe kwa kutumia mkono wa chuma ama mbinu yeyote ile haramu, lakini kushinda watashinda.

Kinachowaumiza kichwa ni je kama wakishinda kwa uharamia kama walivyozoea vipi kuhusu amani ya Taifa? Nchi itaendelea kuwa tulivu kwa kiwango cha kuridhisha ama itakuaje? Hili la amani ndilo linaloleta utatanishi kwa sasa, lakini si kuhusu kushinda uchaguzi!

Lowassa atakatwa jina kwa sababu hizi hapa:

1. Mahasimu wake waliopo ndani ya chama wamejipanga vilivyo

2. Kauli ya Mbowe kuwa Lowassa ni bubu hawezi kuongea kwenye ulingo wa siasa

3. Kauli ya Dr Slaa kuwa hawezi kula sahani moja na fisadi.

Hizi kauli za Mh Mbowe na Dr Slaa zimetoa kiashiria kuwa Lowassa hawezi kupokelewa UKAWA, na hata akienda ACT hatakuwa na madhara makubwa maana chama kimeamua kushinda uchaguzi kwa mbinu yeyote ile iwe haramu ama halali

4. Ukwasi wake mkubwa unaotumika kupata urais wa JMT hili litaadhiri taswira ya chama (jembe na nyundo) na sasa kuonekana ni chama cha matajiri. Ikumbukwe wapiga kura wengi ni wa kipato cha kati na cha chini na sio matajiri. Hivyo chama kitavaa koti la ufisadi mchana kweupee kama huyu ndugu akiteuliwa kugombea urais

5. Lowassa alichelewa kujisafisha, sasa hivi hasafishiki tena akiwa kwenye ulingo wa mapambano, amechelewa. Ni kweli kuwa ndani ya chama hakuna msafi lakini yeye kakosea strategy za kujisafisha

6. Lowassa hajaweka hadharani mpango wake wowote wa kushawishi wananchi kuhusu urais wake kama atateuliwa.

Mfano: Lowassa anazungumzia ajira lakini hajaweza kutoa muelekeo wowote wa namna ajira hizo zinavyopatikana kiasi cha kuwashawishi wananchi.

Hajatoa mpango kazi wowote wa namna ya kuimarisha elimu kama anavyotanabaisha kuwa elimu kwake ndio kipaumbele, yeye anaongea tu kuhusu umuhimu wa elimu lakini hajaeleza waziwazi kuhusu udhaifu wa mfumo wa elimu iliyopo sasa hivi na nini atakachokifanya kuboresha. (watu wengi watasema sasa haya si atatoa wakati wa kampeni? ukweli ni kuwa alipaswa kuweka mipango yake wazi mapema sana ili kupata ushawishi kutoka kwa wananchi kiasi cha kuwatishia ma don wa chama kukata jina lake).

Tuendelee kusubiri kuna plans B dhidi ya Lowassa. Plan B hii ni kwa ajili ya kunusuru chama ndani ya chama

Hoja dhaifu sana, afadhali lowassa kaweka wazi vipaumbele vyake, hao wengine hata hatujui wanautaka urais kwa ajili gani.
 
Cdm na ccm mmeungana kumchafua lowassa kisa kusikia anaenda act wazalendo
 
lowassa atakatwa, nchi haituwa na amani tena, mara Mbowe na Slaa wamesema hili na lile, nini? hivi wewe ulitaka kusema nini?
 
matope yamewajaa watanzania hawasikii kitu against lower sir,ni ujinga wa hali ya juu kuchagua lowasa

Hili ni tatizo kubwa sana, watu hawana muda wa kufikiri huyu ni mtu wa aina gani badala yake wameangukia tu. Tulipaswa kuangalia matatizo tuliyo nayo ambalo si ukweli uliojificha kuwa ni maadili ya watumishi wa umma (rushwa). Mambo ya elimu ni suala la kuimarisha tu km pesa itakuwepo
 
inatia matumaini kuona wengi sasa tunajitambua na tunapinga kwa juhudi zote huyu fisadi kuutaka urasa.
 
Back
Top Bottom