fikirikwanza
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 7,452
- 3,073
Hatuwezi kuwa na ushirika ktk masuala kama haya ya wizi wa mali ya umma, Job Ndugai
Wananisikitisha sana watz hata wanaume kuwa wasahaurifu kiasi chakurubuniwa na huyu mtu loh!!
CCM oyeeeeeeeeeeeee ndicho chama bora Tanzania.
Wakuu! Heshima mbele!
Ipo hivi:
Lowassa hatapeperusha katu bendera ya CCM urais 2015. Ma don wa chama wameshaafikiana tayari kuhusu hili. Tathmini makini iliyofanywa na chama imebaini kuwa CCM wanaweza kushinda urais 2015 kwa namna yoyote ile iwe kwa kutumia mkono wa chuma ama mbinu yeyote ile haramu, lakini kushinda watashinda.
Kinachowaumiza kichwa ni je kama wakishinda kwa uharamia kama walivyozoea vipi kuhusu amani ya Taifa? Nchi itaendelea kuwa tulivu kwa kiwango cha kuridhisha ama itakuaje? Hili la amani ndilo linaloleta utatanishi kwa sasa, lakini si kuhusu kushinda uchaguzi!
Lowassa atakatwa jina kwa sababu hizi hapa:
1. Mahasimu wake waliopo ndani ya chama wamejipanga vilivyo
2. Kauli ya Mbowe kuwa Lowassa ni bubu hawezi kuongea kwenye ulingo wa siasa
3. Kauli ya Dr Slaa kuwa hawezi kula sahani moja na fisadi.
Hizi kauli za Mh Mbowe na Dr Slaa zimetoa kiashiria kuwa Lowassa hawezi kupokelewa UKAWA, na hata akienda ACT hatakuwa na madhara makubwa maana chama kimeamua kushinda uchaguzi kwa mbinu yeyote ile iwe haramu ama halali
4. Ukwasi wake mkubwa unaotumika kupata urais wa JMT hili litaadhiri taswira ya chama (jembe na nyundo) na sasa kuonekana ni chama cha matajiri. Ikumbukwe wapiga kura wengi ni wa kipato cha kati na cha chini na sio matajiri. Hivyo chama kitavaa koti la ufisadi mchana kweupee kama huyu ndugu akiteuliwa kugombea urais
5. Lowassa alichelewa kujisafisha, sasa hivi hasafishiki tena akiwa kwenye ulingo wa mapambano, amechelewa. Ni kweli kuwa ndani ya chama hakuna msafi lakini yeye kakosea strategy za kujisafisha
6. Lowassa hajaweka hadharani mpango wake wowote wa kushawishi wananchi kuhusu urais wake kama atateuliwa.
Mfano: Lowassa anazungumzia ajira lakini hajaweza kutoa muelekeo wowote wa namna ajira hizo zinavyopatikana kiasi cha kuwashawishi wananchi.
Hajatoa mpango kazi wowote wa namna ya kuimarisha elimu kama anavyotanabaisha kuwa elimu kwake ndio kipaumbele, yeye anaongea tu kuhusu umuhimu wa elimu lakini hajaeleza waziwazi kuhusu udhaifu wa mfumo wa elimu iliyopo sasa hivi na nini atakachokifanya kuboresha. (watu wengi watasema sasa haya si atatoa wakati wa kampeni? ukweli ni kuwa alipaswa kuweka mipango yake wazi mapema sana ili kupata ushawishi kutoka kwa wananchi kiasi cha kuwatishia ma don wa chama kukata jina lake).
Tuendelee kusubiri kuna plans B dhidi ya Lowassa. Plan B hii ni kwa ajili ya kunusuru chama ndani ya chama
watu wasingesahau dhambi zako leo usingekuwa hapa unanyooshea wengine vidole kwa makosa yaliyopita.
haya kateni muone mziki wake!! kama mlizoea kukata ya wengine hapa mmekwama!!!
Lowassa atakatwa jina kwa sababu hizi hapa:
Sijasema dhambi tafadhali usiniwekee maneno kinywani, hata hivyo sijafanya dhambi yakumuathiri binadamu mwenzangu ndio maana nipo na amani tele.
Ila huyo unayemtetea aliathiri mamilioni ya watu, na kuturudisha nyuma kiuchumi hasa baada yakutuletea mgao fake wa umeme usio elezeka. dogo labda wewe ulikuwa mdogo hujaanza maisha ndio maana hujui namna gani watu tulisuffer na ishu ya richmond.
una lingine??????
nina mengine na sio lingine ila uache kwanza tabia za kiswahili za kuita watu "dogo" una uhakika gani kama mimi ni dogo au sio, mbona mimi sijakuita "kilema"?
All in all you have no any justification that EL had his hands in richmond saga ni propaganda tu za kisiasa ambazo wewe kwa kutoijua siasa ung'akang'aka.
Uliza uelezwe kinagaubaga
nina mengine na sio lingine ila uache kwanza tabia za kiswahili za kuita watu "dogo" una uhakika gani kama mimi ni dogo au sio, mbona mimi sijakuita "kilema"?
All in all you have no any justification that EL had his hands in richmond saga ni propaganda tu za kisiasa ambazo wewe kwa kutoijua siasa ung'akang'aka.Tabia za kidhungu ndio zipi dogo??????
Mimi ni mswahili atii, hivo nakideal kiswahili vilivyo upo hapo dogo????
Pia neno dogo halikuweki kwenye kundi fulani bali linakuonyesha tu kuwa mimi ni dada yako, yaani mkubwa kwako.
Kuhusu EL hapo haihitaji justification yoyote, alituibia basi, mmechelewa kumsafisha na pia yeye kachelewa kujisafisha.
Sina swali maana sitapata jibu jipya, over