Lancashire
JF-Expert Member
- Sep 20, 2014
- 14,045
- 10,329
Wakuu habari zenu!
Nimejaribu kutafakari kwa kina sababu za Lowassa kuanza kujisogeza katika utawala huu ambao kwa Chadema ni sawa na paka na panya.
Zipo sababu kadhaa ambazo naweza kudhani ndio zimemfanya mzee wetu Edward lowassa kujisalimisha katika Chama Cha Mapinduzi kama ifuatavyo:-
1. Lowassa kwa sasa hana Cha kupoteza ndani ya Chadema kwa kuwa tayari nafasi yake imepita ilikuwa ni 2015 last chance.hana matumaini ya kuendelea tena kugombea uraisi kupitia chama hicho hasa ukizingatia Chadema kuwa na hazina ya vichwa kama Tundu Lissu na wengine.
2. Lowassa mpaka sasa ameandamwa na vikwazo vingi katika mali zake na baadhi ya biashara zake kutoka serikalini hivyo kumuweka katika hatari ya kufilisiwa na ni wazi hata familia yake imemshauri ajisalimishe mapema kwa Rais magufuli ili kulinda maslahi yake na familia kwa ujumla.
3. Suala lingine ambalo kwa kiasi fulani nadhani limechangia Lowasa kukutana na Rais magufuli na kuweka mambo sawa ni suala la Mkwe wake Sioi sumari kuwekwa lock up mpaka sasa kwa makosa ya uhujumu chumi .tukumbuke huyu sioi amemuoa binti wa lowassa aitwaye Pamela.sasa kwa hili hakuwa na namna zaidi ya kuwasiliana na Bwana mkubwa.
Hizi ni baadhi ya sababu kwa mtazamo wangu zilizomfanya Bwana Lowassa kusurrander katika Utawala wa CCM.na nikiangalia siku si nyingi Lowassa atatangaza kujiunga na CCM.
Ningependa kila mtu hapa aweze kutoa sababu ambazo anadhani zimempelekea Lowassa kuunga mkono Utawala wa rais kinyume na msimamo wa Chadema.
NB. Moderators nawaomba msiunganishe uzi huu ili watanzania tuweze kuchambua kwa kina sababu za msingi za Lowassa kukutana na Rais Magufuli na Kuunga Mkono Juhudi za Rais wetu mpendwa.