youngsharo
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 2,491
- 500
Ama kweli nimeamini Lowassa alikuwa na msimamo wa pekee ndani ya CCM.
Lowassa amepania kuwaokoa watanzania, hana huruma tena na chama chake cha awali.
Nathubutu kusema kwa namna nyingine/kwa tafsiri ya kisiasa, Lowassa alikuwa "MSALITI" wa CCM tangu akiwa waziri mkuu.
Nini maana ya msaliti? msaliti ni mtu anayejifanya kuwa yuko na wewe ilihali anatumika na mtu/watu wa upande mwingine.
Lowassa alikuwa msaliti kwa sababu alisimama kama mwanaCCM lakini alitumika na wananchi, CCM haikuwa na nia ya kuwapa maendeleo watanzania, Lowassa akatumia nafasi hiyo akakusanya siri zote na kuwapatia wananchi.
Lowassa alitaka watanzania wafaidi matunda yao, CCM walitaka kuendelea kushibisha matumbo yao, na ndipo Ccm baada ya kugundua kuwa Lowassa yuko tofauti na malengo yao walianza kugoma kumpa kipaumbele, lakini kwa kuwa alipoamua kujitosa, sasa Ccm wanajuta maamuzi yao na Lowassa hana huruma nao tena kama wao walivyokuwa hawana huruma na wananchi wao.
Viva Edward Lowassa