Lowassa hana huruma tena na CCM

Lowassa hana huruma tena na CCM

Hata mimi sitawahurumia kabsa, tar25 Oct ntaungana na wanamabadiliko kuichinjia mbali!!
 
Kidude cha like Ni Mara moja. Nilitaka kutoa nyingi kama spread sheet.
 
nifah: wewe ni mshabiki mkubwa wa EL, omba matokeo yawe upande wako, la utafadhaika maishani. Ila jua kwamba yeye umshabikiaye hivyo, ninimani yangu iuna kitu unategemea. Kila la kheri.

TAFAKARI CHUKUA HATUA

mmh! we hata kutongoza huwa unapata tabu, ndo unamsomesha hapo au?
 
Last edited by a moderator:
nifah: wewe ni mshabiki mkubwa wa EL, omba matokeo yawe upande wako, la utafadhaika maishani. Ila jua kwamba yeye umshabikiaye hivyo, ninimani yangu iuna kitu unategemea. Kila la kheri.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Picha ya nifah imekuchanganya, sasa unajifanya kumwonea huruma...Changia Thread ya Youngsharo bana. Wewe unadhani watu waliopo hapa wana ushabiki wa kitoto pasipo mategemeo? Tegemeo la kila mwenye kumshabikia Lowassa ni " Mabadiliko " Kama ulikuwa hujui ujue sasa.
 
Maajabu ya waltz ccm imeshindwa kuwapa Mani huko Temeke Jana wanajazana Mwembeyanga
 
nifah: wewe ni mshabiki mkubwa wa EL, omba matokeo yawe upande wako, la utafadhaika maishani. Ila jua kwamba yeye umshabikiaye hivyo, ninimani yangu iuna kitu unategemea. Kila la kheri.

TAFAKARI CHUKUA HATUA

Sikatai,nampenda Lowassa sana tena sana,sitegemei chochote....nimejitolea kumpigania na kuyapigania mabadiliko ambayo tukishinda itakuwa faida ya wengi. nifah sio mbinafsi,napenda mafanikio ya wengi kuliko yangu mimi binafsi.
Nitakuwa mwendawazimu kama sijui kuna kushinda na kushindwa,nikishinda Alhamdulillah nikishindwa kheri pia.
Wewe unanijua hadi useme nitapata mfadhaiko maishani?Nimepitia mengi zaidi ya hili,niko strong.....zaidi SITEGEMEI KUSHINDWA.
 
Last edited by a moderator:
Ama kweli nimeamini Lowassa alikuwa na msimamo wa pekee ndani ya CCM.

Lowassa amepania kuwaokoa watanzania, hana huruma tena na chama chake cha awali.

Nathubutu kusema kwa namna nyingine/kwa tafsiri ya kisiasa, Lowassa alikuwa "MSALITI" wa CCM tangu akiwa waziri mkuu.

Nini maana ya msaliti? msaliti ni mtu anayejifanya kuwa yuko na wewe ilihali anatumika na mtu/watu wa upande mwingine.

Lowassa alikuwa msaliti kwa sababu alisimama kama mwanaCCM lakini alitumika na wananchi, CCM haikuwa na nia ya kuwapa maendeleo watanzania, Lowassa akatumia nafasi hiyo akakusanya siri zote na kuwapatia wananchi.

Lowassa alitaka watanzania wafaidi matunda yao, CCM walitaka kuendelea kushibisha matumbo yao, na ndipo Ccm baada ya kugundua kuwa Lowassa yuko tofauti na malengo yao walianza kugoma kumpa kipaumbele, lakini kwa kuwa alipoamua kujitosa, sasa Ccm wanajuta maamuzi yao na Lowassa hana huruma nao tena kama wao walivyokuwa hawana huruma na wananchi wao.

Viva Edward Lowassa

youngsharo

Maswahiba wakuu wa Lowassa ni CCM na wale wanaohama CCM bila kusema wanaenda chama gani.

Ukweli pia ni kwamba Lowassa anawategemea sana wana ccm katika kuunda serikali.
Wewe unadhani kina Kamanda Lema, Sugu, Vincent na dogo janja kwa mfano wanaweza ongoza vipi kwa ufanisi wizara muhimu kama Fedha, ulinzi, mambo ya ndani, Afya, mawasiliano, ujenzi, sayansi na tech??

Hili swala liko wazi mno.
Makamanda wengi watapiga kiwango cha chini ya Mlugo, navuta picha Lema wizara ya Fedha au ya Ulinzi. Kha! Mungu aepushie mbali.
Kwanza Mungu tunampa kazi ya bure.
Kazi kikatio tu.
 
Back
Top Bottom